Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Ngoja wenye dini ya mbwa waje muone wanavyomtetea Idd Amin.
 
Nyie watu hata kesho muuwaji albashiri watu watasema sababu dini yake as if hii ni dini ya watakatifu tu nendeni mkawaulize waganda walipitia wakati much kiasi gani sio hizo story za kuskiaskia vijiweni
 
Hivi ilishindikana kabisa kuongea nae? Maana walokufa ni raia. Iddy Amini hakufa wala Nyerere
 
Hiyo balaa sana
Historia ya kuvutia sana. Nimeingia humu leo kuweka kile nimefikiri ni guso la kihistoria kumbe nakutana na historia hii ya kuvutia sana. Mwaka huo wa 1978 nilikuwa mwanafunzi wa kidato cha nne. Tuliandaliwa kwenda vitani pia, tulifundishwa mgambo kwa miaka 2 tangu tukiwa kidato cha 2, tulisoma kidogo nakumbuka na muda mwingi tulitumia katika mazoezi ya vita. hatukuelewa sana mpakasiku Mwalimu alipotangaza vita, kwa mara ya kwanza nikiwa kijana wa miaka 15 hivi nilimsikia Nyerere akitukana "Mshenzi" tutampiga! Enzi hizo tulizoea matusi ya mzee Kenyatta wa Kenya.

Licha ya historia hii nzri ambayoni matokeo ya uhuru kutoka wakoloni na ukoloni mambo leo...nina langu pia juu ya historia naliweka hapa:

 
 
Historia ya kuvutia haswaa. Pongezi za dhati kabisa kwa mashujaa wetu waliosimama mstari wa mbele kupigana.

Mama umesema ukiwa kijana mdogo mlitumia muda mwingi kufunzwa mafunzo ya mgambo zaidi ya masomo darasani, hili liliadhiri elimu yetuu? Kwasababu hiyo miaka miwili si haba. Hebu tujuze sisi ambao tulikuwa hatujazaliwa bado.....vita iliadhiri vipi elimu? Ukisimulia kama story hivi inakuwa fine.

Asante!
 
Ukiwa kidato cha pili ukapelekwa vitani amakupewa mafunzo ya kijeshi, unaweza kuumia kiakili na kimwili. Pia huna utashi wa kukubali ama kukataa, unapokea na kutii maagizo. Kielimu pia. Mimi niliumia kimwili zaidi: kubeba ile bunduki nzito, kufanya mazoezi ya shabaha nk nafikiri wengine tulikuwa bado. nakumbuka nilitoboka kidogo begani kwenye palekitako cha bundki kilikaa, chenye mduara. Wenzangu wengi waliathirika kielimu na kimaadili.Wengi walishindwa kumudu masomo, matokeo yetu ya kidato cha 4 hayakuwa mazuri, nafikiri niliendelea na kidato cha 5 peke yangu. Tulijifunza mambomengi juu ya usalama nk. Haikuwa bure ila mapema mno pengine.

Baadae nikisoma sheria nimejua kuwa kumbe mafunzo ya kijeshi yanahitaji utashi wa mtu. Suala zima la vita linarudisha sana maendeleo nyuma, kwa sababu pia gharama zake ni kubwa mno ikilinganishwa na elimu, maji na afya, miundombinu nk, ambayo nayo huharibiwa na vita. Kama inawezekana ni vizuri sana kuzuia vita nafikiri. Kuna uzi mwingine unahiji kama ilikuwa lazima, nitausoma nione mjadla ulivyo.
 


Mama Anna Mghwira hongera sana inaonyesha jinsi nchi zetu za kiafrika mara baada ya kupata uhuru jinsi zilivyotumia rasilimali zake katika mambo ya hovyo kabisa.Kama si hii vita nina uhakika Tanzania na Uganda zingekuwa zimepiga hatua kubwa sana katika nyanjan za uchumi,elimu,miundombinu na nk.

Samahani imebidi ni quote bandiko lako zima zima.
 
swali dogo tu nauliza...
hivi vita vya Tz na uganda nini haswa chanzo chake mpaka tumefikia kupigana?
maana kinachonishangaza!!! ukiangalia film ya vita hii kuna sehem wajeda wa tz walionekana kitaani Entebe wakiwa pamoja na wajeda wa UGANDA.
sasa ndo najiuliza tulikuwa tunapidgana na nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…