Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza


Soma vizuri hiyo historia yangu utaelewa mengi,Hata hivyo sijaelewa bada nini shida yako kuhusu vita vya kagera!!!!
 
Hiyo habahatishi, ni kweli alikwenda front. Mimi nilikuwa 10 majeshi toka Shy, sasa kuna WO 2 anaitwa Sancho alikuwa anachekesha sana, alikuwa mkurya halafu kiswahili kwake shida, hajasoma lakini alikuwa NATO kinoma. Akivaa Canadian combat na vimbwanga Vingi, SMG, pistol, hand grenade, panga, mkuki, steel element mbili, halafu mouse tache wa kutosha. Ulikuwa ukimuona lazima ucheke. Siku moja Arusha (baada ya kurudi front front) akiwa na MP patrol akalikamata bus Leyland LA Tawico kwa sababu tu rangi imefanana na ya jeshi.Siwezi kuelezea Zaidi lakini kama yuko anaemjua akolezee Zaidi. Ingawa kwa sasa ameshatangulia mbele ya hali.
 
Mkuu Echolima Kamanda wangu, umetupatia live history ya vita vya Kagera. Jamaa yangu anafanya utafiti kuhusu vita hii. I wish angekupata kwa akili ya interview angepata vitu vikubwa sana toka kwako.
 
Mkuu Echolima Kamanda wangu, umetupatia live history ya vita vya Kagera. Jamaa yangu anafanya utafiti kuhusu vita hii. I wish angekupata kwa akili ya interview angepata vitu vikubwa sana toka kwako.

Soma pia Historia hiyo sehemu ya pili imo humu humu JF
 
Vita haina macho mama Anna Mghwira. Nchi ikiingia vitani kitu kikubwa ni kujiweka sawa kisaikolojia.
Unachosema ni kweli. Hata mie nilikuwa darasa la 7. Tulifundishwa kuchimba mahandaki shuleni na askari wa Mgambo na jwtz. Kwa sababu hiyo hiyo tulisaidia kuchimba mahandaki majumbani kwetu.
Tulifundishwa ku crowl na kutahadharishwa kutoa taarifa tukimuona mtu ambaye tunamshuku.
Vita inarudisha maendeleo ya Taifa nyuma lakini inapobidi hakuna namna.
Unashangaa leo taifa kubwa kama marekani linatengeneza masilaha makubwa, ili iweje. Urusi ina kwenda Syria.
Kwa hiyo mama Anna, Vita hivi huletwa na kuchochewa na mataifa makubwa.
Mataifa hayo yangeweza kuzuia Vita ya Kagera kwa upatanishi kati ya mwl na Amin (Mungu awarehemu).
 
Triple w
 
kuna askari wengi walifanya kazi kubwa lakini huwa hawasikiki kwenye historia ya vita vya kagera kumbuka kipindi hicho askari wetu wengi walikuwa wamesomeshwa Cuba,Uingereza,China,Israel,Canada walikuwa na uwezo mkubwa sana wengi wametangulia mbele za haki
 

Wengi wa wanajeshi wetu baada ya vita walikufa kwa kukosa matunzo,Maana walitakiwa kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani walipaswa wapimwe ili kujua kama wameadhirika na Post-traumatic stress disorder (PTSD)Tatizo ambalo huwapata wanajeshi wengi wakiwa vitani au baada ya kutoka vitani.Baada ya vita wanajeshi wetu waliruhusiwa kurudi nyumbani bila kufanyiwa uchunguzi wa PTSD hivyo wanajeshi wengi walienda kuzua balaa kubwa kwa raia wema huko mitaani na kuna watu wengi sana waliadhirika sana na ujio wa hawa wanajeshi na hatimaye kusababisha wanajeshi wengi kuleta hali ya uvunjifu wa amani,Unywaji wa Pombe kupindukia,Ugomvi mbalimbali ambao wakati mwingine ulisababisha vifo kwa wanajeshi wetu hao!!!Binafsi nailaumu sana serikali yetu kwa kutotilia maanani maisha ya wanajeshi wetu hasa waliopigana katika vita vya kagera,Wengi wamekufa kwa msongo wa mawazo na bila msaada wowote.Na wengine walio hai sasa hivi hata ukiambiwa alipigana vita vya Kagera waweza kukataa maana ana hali mbaya kupindukia hawana mbele wala nyuma.Kinyume na nchi zingine wanajeshi wastaafu wanatunzwa vizuri na wanaheshimika.
 
Hii ya wanajeshi kutohudumiwa baada ya vita hatari sana sio hapa Afrika tu, popote pale duniani. Ninaye rafiki (UK) alipigana vita Iraq sasa hivi ameamua kuwa trainer (kufundisha mazoezi) yeye analalamika baada ya vita baadhi ya wanajeshi wenzake walipata matatizo vitani (hususani Psychologically) wameachwa bila msaada wa maana japo hawa ni wanajeshi wa nchi tariji UK sasa anasema wengi mawekuwa kama wendawazimu tu. Nimejiuliza hapa maswali nimegundua jeshi ni kazi ya kujitoa muhanga tu.....japo unapigana kwaajili ya nchi yako ukidhani mambo yatakuwa sawa baadaye lakini mwisho wa siku serikali inaweza isikujali kwalolote ikakuancha ukahangaika mwenyewe na kujifia.
 

Wenzetu wako vizuri sana kwa kuwahudumia wanajeshi waliotoka Vitani mimi nilichokuwa nasema ni kutoka vitani moja kwa moja kijijini kwenu bila kupatiwa uchunguzi wa kuwa umeadhirika na tatizo la kwa mawazo au la.USA wao wanavituo kabisa kwa ajili ya wahanga wa Matatizo yatokanayo na vita.Kuhusu kuhudumiwa wanajeshi waliotoka vitani hasa majeruhi kwetu ilishangaza sana baadhi iliamuriwa warudi makambini wakapewe kazi ndogondogo kweli inauma sana sana!!
 
Umefanya vizuri sana kutupa hizo narratives za vita hiyo ambazo hazina chumvi na zinatoka 'straight from the horses' mouth' umetuwezesha sisi tuwape permanent facts za vita hiyo kutoka kwa mpiganaji. Ahsante sana
 

Jee wale wanajeshi wenzako uliowakuta wamefariki waliuwawa wakati wa uvamizi au katika jitihada za kuvuka mto
 
Jee wale wanajeshi wenzako uliowakuta wamefariki waliuwawa wakati wa uvamizi au katika jitihada za kuvuka mto

Hapo uvamizi ulikuwa tayari umefanyika na hao waliuwawa wakati wa mapigano ya kutaka kuwatoa wanajeshi wa Amini katika maeneo ya nchi yetu mwanzoni kabisa mwa vita vya Kagera.
 
Hapo uvamizi ulikuwa tayari umefanyika na hao waliuwawa wakati wa mapigano ya kutaka kuwatoa wanajeshi wa Amini katika maeneo ya nchi yetu mwanzoni kabisa mwa vita vya Kagera.
Nasikia wakati huo ndege iliyokua imebeba askari wa libya mliweza idanganya ikatua Tanzania.
Napenda kujua kama ni kweli afu huo mkakati had ikatua tz ulikuaje yaan seems to be very interesting kama ni kweli. OVER
 
Nasikia wakati huo ndege iliyokua imebeba askari wa libya mliweza idanganya ikatua Tanzania.
Napenda kujua kama ni kweli afu huo mkakati had ikatua tz ulikuaje yaan seems to be very interesting kama ni kweli. OVER

Kunapotokea vita mara nyingi kunakuwa na viwanja vingi vya kupigania vita kama vile kuna askari wa miguu,Majini na Anga na idara nyingi tu kama vile Electronics Jamming walikuwa wanao uwezo wa kuvifanya vifaa vya ndege yeyote wakati ule visifanye kazi yake ipasavyo hatimaye kuweza kutupatia wageni wasiotarajiwa kwenye uwanja wa ndege wa kilimanjaro!!!Hiyo ni kweli ilitokea kabisa.
 
Kikwete alikuwa kamisaa Chuo cha maafisa na bosi wake Col Madaha
 
Ooooh hv hamnaga movies za hii kitu
 
Nimejifunza mengi, Nlikua siyajui Mungu akubariki ila ungeandika ktb kwa history ya baadae!!!
SWALI LA KIZUSHI : ulitumia siku ngp kuandka hii makala hadi kuikamilisha Hapa jukwaan
 
Hiyo Movie hakuna maana Jeshi letu lilikuwa bado limegubikwa na Usiri kila kitu wakati huo ilikuwa siri sijui sasa hivi mambo yakoje!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…