Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

At least wewe una clue. Hiyo ya ndege ya Israel ndo tunapoweza kuanzia, issue ya dini weka pembeni

..lakini nyerere naye hakuwa na mahusiano mazuri na israel. Alivunja uhusiano na israel kwa sababu ya suala la palestina na uvamizi wa ardhi ya waarabu.

..kwa msingi huo sioni mantiki ya Israel kumtumia nyerere kumtoa amini.

..hoja nyingine ni mahusiano ya nyerere na nchi za magharibi us na uk included, hayakuwa mazuri kutokana na msimamo wa Tz kuhusu vita vya ukombozi vya Zimbabwe na Afrika Kusini.

..Obote naye hakuwa rafiki wa Waingereza. Alipinduliwa wakati akiwa ktk harakati zake na Nyerere na Kaunda dhidi ya Waingereza wakipinga utawala wa walowezi wa rhodesia/zimbabwe.

..zaidi, kuna tetesi kwamba Waingereza walituwekea vikwazo vya kununua silaha wakati wa vita vya kagera.

..binafsi naona theory ya Tz kutumiwa na Israel, Uk, na Us, kumpindua Amini siyo ya kuaminika. Kwa mtizamo wangu Mzee Jomo Kenyatta angefaa zaidi kwa mipango kama hiyo kuliko Julius Nyerere.
 
Jaribu kuingia ndani zaidi hasa kwa wapiganaji na makomando waliokuwa mstari wa mbele...unamjua John Warden? sina muda wa kutosha kumtafiti, kama unaweza kuwa na muda au kama kuna mtu anamjua aweke hapa, pamoja na majeshi yetu kurudi nyuma nani alisupply silaha nzito zilizosaidia kumdhibiti Idi
 
Jaribu kuingia ndani zaidi hasa kwa wapiganaji na makomando waliokuwa mstari wa mbele...unamjua John Warden? sina muda wa kutosha kumtafiti, kama unaweza kuwa na muda au kama kuna mtu anamjua aweke hapa, pamoja na majeshi yetu kurudi nyuma nani alisupply silaha nzito zilizosaidia kumdhibiti Idi
 
Yaani binadam hasa Wa tz tuko hivi

Likitokea suala la kiinchi kwanza tunajigawa kii region, kisha ki mkoa, then kikabila kama haitoshi tunakuja kumalizia na dini yaani hapa ndo tunasimamisha kabisa reasoning zetu zoote na hata kama ni PhD basi mawazo ya mwana imani mwenzako Wa lasaba yasio fahaa utayakubali tuu ingawa akili yako inakataa
 
huyo anaesema marekani ilishindwa vita vietinam na afghanistan 100% ni mwisilam maana waislam hata siku 1 hua hawaikubari usa kwa taarifa yako hao magaidi wako walifurushwa madarakani na usa kwa miki 2 tu na mwish wa siku kalzai ndio rais na sio mula
mambo ya kidini yanakusaidia nini...ongea vya mana
 

..silaha tulinunua kwa Mrusi tena tukaingia ktk deni kubwa.

..nyingine tulipewa na Algeria. Nadhani Angola pia walitusaidia.

..nimesoma vya kutosha kuhusu suala hili sijaona mkono wa Usa, Uk, au Israel, kutusaidia.
 
..silaha tulinunua kwa Mrusi tena tukaingia ktk deni kubwa.

..nyingine tulipewa na Algeria. Nadhani Angola pia walitusaidia.

..nimesoma vya kutosha kuhusu suala hili sijaona mkono wa Usa, Uk, au Israel, kutusaidia.

Mkuu JokaKuu pia baadhi ya nchi za Ulaya Mashariki kama Bulgaria na Poland zilitupatia silaha.Issue ya Algeria ni tofauti kidogo yenyewe litusaidia silaha bure kabisa.Msumbiji walitoa hadi askari wao walipigana bega kwa bega na TPDF.Hayati Comred Samora Micheal alikuwa Mtoto wa Nyerere alifahamu jinsi Tanzania ilivyojitolea mhanga kuhangaikia uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika.

Kenya ya Rais Daniel arap Moi iliisaidia Uganda kwa hali na mali,ilipitisha vifaa vya kivita bandari ya Mombasa na hata military inteligence.
 
Kama jambo lenye umri wa miaka 40 tu watu tunafikia hatua ya kudanganya namna hi basi hi ni Hatari sana kwa kizazi cha nchi. Kweli kabisa unaweza kudanganya watu kwamba Nyerere ndiye aliyekua mchokozi!!!!? Kwa taarifa yako Amini alianza kuichokoza Tanzania since day 1 anaingia madarakani, Nyerere alijizuia sana kupigana na Iddi Amin na hata baadhi ya watu walianza kumwona Nyerere ni mjinga. Shambulio alilolifanya Amin kwenye mashamba ya miwa kule Kagera kulitokea ukimya wa takribani miezi 6, kipindi hiki Nyerere alikua ndio kaazimia kuingiza Tanzania vitani. Kumbuka fujo za Amini zilianza tokea mwaka 1972 na tuliingia vitani mwaka 1978 nadhani it was December. Hicho kipindi cha miezi 6 Majeshi yetu yaliamua kujikita kwenye upelelezi wa kujua hasa nguvu za Amin zipo wapi. Tulipoingia vitani ndio tulipokuja gundua kumbe na Gadafi alikua nyuma yake. Hongera Nyerere kwa kuitetea mipaka ya Tanzania.
 
Nyerere alitaka kumrudisha rafiki yake Obote kwa gharama yoyote bila kujua wananchi wake hawamtaki..alimrudisha lakini baada ya muda mfupi sana wakamuondoa tena!Ilikuwa kazi ya bure..
 
Nyerere hakupenda Uganda itawaliwe na Muislam (Idd Amin)
Kweli????? Watu wengine na kufikiria kwao! Kwani Idd Amin ndiye alikuwa peke yake Rais Mwislamu wakati ule? 1971/72 Idd Amini alivamia Tanzania, alitishia Tanzania ndio kwa kuwa Obote alikimbilia Dar, lakini zile kauli za kejeli za Amin, yale mauaji ya kila siku ya wapinzani wake, kula viungo vya watu, kweli unataka kusema Amin angekuwa Mkatoliki basi Nyerere asingemfanyizia alichomfanya Amin????

Hebu fikiria kidogo. Na ile 30 Oktoba 1978 ni nani alimvamia mwingine? Uliza kule Mtukula na Minziro, kabla ya kuanza kushadidia mambo ya dini. Umeniuzi Sana wewe!
 
..siyo kweli kwamba Nyerere hakutaka Muislamu atawale Uganda.

..mkumbuke Iddi Amin alikuwa replaced na Muislamu Prof.Yussuf Kironde Lule.

..Nyerere hakuwa na control ya mchakato wa kumpata Raisi wa Uganda baada ya Amin.

..hapa Tanzania Nyerere alikuwa akitaka Salim Ahmed Salim aongoze Tanzania.
 

Mkuu JokaKuu unajua wakati mwingine unatakiwa kupuuza baadhi ya michango ya wanajamvi.Huyu Kiwango chake hakina tofauti na wauza ghahawa Kariako.
 
Nimejifunza mengi sana humu..mengi sikuyajua,,mtazamo wangu ni huu..
1.Ikiwa katika mkutano ule wa jumuiya ya madola mabepari walijua kabisa watakalomfanyia obote na hatimaye akapinduliwa, basi ni moja kati ya mikakati mikali yakumpunguza makali mzee kambarage na wenzake katika harakati za ukombozi.
2. Ni unafiki mkubwa sana kuwahi kutokea kama mwalimu asingempa hifadhi swahiba wake Obote mtu waliokuwa kwenye mapambano na lengo moja.
3. Uwepo wa Obote Tz ulichangia hasira ya nduli sana, lakini kwa tafakari ya ndani sana tujiulize kama amini alikuwa na backup ya mabepari kumuondoa Obote vipi kuhusu swahiba wake mwalimu? Ingewezekana kumuacha Obote aende huko switzerland lakini huyo aliyempindua angeweza pia kwa backup ya mabepari haohao kuja kuvamia Tz na kupindua serikali na tungekuwa na kilio kikubwa zaidi ya hiki kinachosemwa humu.Kwahilo naona mwalimu aliangalia mbali sana na kwa kumsoma Nduli alijua hili ni jipu linalokomaa, huwezi kumuona mtu anakuja kwa jirani yako wa karibu anataifisha mke na watoto kwa msaada wa watu fulani alafu ukachekelea tena usifikiri anaweza fanya jambo hilo kwako pia,,ni lazima uchukue hatua.
4. Kama Nduli alikuwa na sababu hizo za kumng'oa Obote basi alikuwa amemuweka Mwalimu kiporo. Hivyo maamuzi ya awali ya Mwalimu yalikuwa na usahihi mkubwa kwani pengine Obote asingekuwepo kusingekuwa pressure ya kumng'oa nduli na angekuja kutumiwa na mabepari kutuangusha.
5. Mwisho,naona sera za uchumi na maendeleo za mzee kunasehemu hazikuwa sawa ingawa dhamira yake kwa mtanzania ilikuwa nzuri na binadamu hakosi makosa,,anamazuri yake na baadhi ya mambo pia hayakuwa sawa.
 
Wapinzani wa Amini kina Obote, Museveni na Waasi walipewa hifadhi Tanzania miaka kibao kabla ya vita vya Kagera, Huo kama siyo uchokozi ni nini?
 
Vikao vya kuunda serikali ya mpito ya Uganda vilifanyika "Moshi", bila shaka Moshi hiyo ni ya Kilimanjaro, Tanzania. Obote alipenyeza makada wa Chama chake katika kikao hicho. Wakati huo huo inasemekana Obote alikuwa ni rafiki wa Nyerere.

Ukiunganisha "dots" hapo unapata jibu gani?

Kaka
 

..kama Obote alipenyeza makada wa chama chake UPC ktk vikao vilivyofanyika Moshi kwanini vikao hivyo havikumchagua yeye kuwa Raisi wa mpito badala yake vikamchagua Prof. Yussuf Kironde Lule??

..ni kweli makada wa UPC walihudhuria mkutano wa Moshi. Lakini hawakuwa na sauti kubwa ya kuweza kulazimisha maamuzi ya vikao hivyo.

..Obote alirejea madarakani kwa njia ya kura. Aliweza kushinda uchaguzi kwasababu UPC walikuwa na mizizi na wako more organized kuliko vyama vingine vichanga.

..hata leo hii Tz tukifuta vyama vya siasa na kuvirejesha miaka 10 baadaye uwezekano mkubwa CCM watakuwa na nafasi nzuri zaidi kushinda kutokana na ndiyo chama cha mwisho kikubwa kuliko vingine.
 
Mkuu lemutuz,kipindi unaandika haya maswali ulikuwa haujamezwa na ukada wa chama cha kijani,hopefully wakuu walikujibu
 

Hizi story za kwenye kahawa noma aisee
 
Wakuu huu ndio ukweli kuhusu Idd Amin, mkumbuke kwamba katika miaka ile ya 70, Tanzania chini ya Mwl Nyerere ilikuwa nchi mstari wa mbele katika ukombozi wa Afrika. Idd Amini Dada yeye ndiye aliyemsaidia Dk Milton Obote kuingia lkulu, baada ya kuchukua kikosi cha Jeshi na kwenda kumpindua Kabaka katika Ikuru ya Uganda ambapo Kabaka aliwekwa na waingereza na alikuwa kibaraka wao, baada ya Amin kuchukua ikuru alimkabidhi obote na yeye akawa mkuu wa majeshi ya Uganda kwa kuwa yeye obote alikuwa na shule wakati huo, na mjue kuwa Amini na Obote walikuwa ni marafiki wakubwa na Amini alikuwa anapendwa na wanajeshi wote, baada ya muda mwaka 71, Obote alimtuhumu idd Amin kwamba ni Mla rushwa, ndipo Amin alipohisi hatari na kwa kuwa jeshi lote lilikuwa mikononi mwake, alimvizia Obote alipokwenda kwenye mkutano wa Commonwealth country's akampindua. Obote alikuwa rafiki wa Nyerere sana, kitendo cha kupinduliwa Obote kilimuuzi sana Mwl na akampa hifadhi Obote, haikuishia hapo Mwl akawa anamsaidia Obote ku train askari gollilar fighters ili kwenda kumwondoa Amini, kitendo hiki kilimuuzi sana Amini mpaka akamwandikia Telegram Mwl ya kumtukana, hayo maneno siyasemi, chokochoko hiyo ilianza miaka hiyo ya 72, baada ya Amin kuchoshwa na vitendo vya Gollila fighters kuvamia Uganda kutokea Tz ndipo mwaka 78 alipotangaza kwamba atapiga mpaka DSM, na kweli alivamia Kagera kwa jeuri aliyopewa na Gadaffi kwamba atamsaidia mpaka mwisho, ikumbukwe pia mwaka 72 vita ilipiganwa kidogo na mkuu wa Polisi kituo cha mpakani TZ aliuwawa na kuchukuliwa na Amini na kuwekwa kwenye jokofu, mwili wake ulikuja kupatikana baadae...endelea kuwa na mimi kwa simulizi yote ya vita vya Kagera itaendelea.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…