Vita vya Marekani kudai uhuru kwa Muingereza vina funzo kwa Tanzania

Vita vya Marekani kudai uhuru kwa Muingereza vina funzo kwa Tanzania

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
MTIwNjA4NjM0MDA1MzkwODYw.jpg

Mwingireza Mlowezi George Washington
Mwanzilishi wa Taifa la Marekani

us-map.png

Muungano wa madola ya Marekani mwonekano wa siku hizi


UNITED STATES OF AMERICA / Muungano madola ya Amerrika

Muungano wa Madola ya Amerika (kwa Kiingereza: United States of America), inajulikana pia kama Marekani (kwa Kiingereza: United States, US, USA au America), ni nchi inayopakana na Kanada na Meksiko katika Amerika ya Kaskazini, hali kadhalika visiwa vya Hawaii katika bahari ya Pacific.

Mji mkuu wa Marekani ni Washington DC.


colonies.gif

Makoloni 13 ukanda wa Bahari ya Atlantic ndiyo yaliyounda serikali ya shirikisho,
imechukua karne tafu kufikia hatu aya leo
dola ya mwisho kujiunga ikiwa Florida katika karne ya 20


SABABU ZA VITA

Vita lilitokea kutokana na kutoelewana kati ya Dola la Uingereza na walowezi wake katika Amerika ya Kaskazini. Uingereza ilikuwa na koloni 13 zilizokaliwa na wahamiaji kutoka Uingereza penyewe.

Serikali ya London ilitawala maeneo haya kwa njia ya magavana na wanajeshi wake. Sheria zilitungwa London zilizokataza kuanzishwa kwa viwanda kwenye koloni na hivyo walowezi walilazimishwa kununua bidhaa nyingi kutoka Uingereza kwa bei za juu.

Baada ya Vita ya miaka saba Uingereza ilihitaji pesa ikaongeza kodi kwa bidhaa zilizosafirishwa kati ya koloni na nchi mama. Walowezi hawakupendezwa na kodi za nyongeza walidai kupewa wawakilishi katika bunge la London na nafasi ya kushiriki katika maazimio juu ya sheria zilizowaathiri.

Walitangaza wito wa "no taxation without representation" (hapana kodi bila kuwakilishwa). Mwaka 1767 bunge la Uingereza lilikataa maombi ya wakoloni na badala yake idadi ya wanajeshi iliongezeka katika koloni.

Map_of_Territorial_Growth_1790_sm.jpg
Kwa sababu hizo wakoloni wengi walijisikia vibaya eti walidharauliwa wakaongeza ukali wa upinzani. Mwaka 1773 umati ya watu walishiriki katika tukio la "Boston Tea Party" wakatupa mizigo ya majani ya chai kwenye bandari ya Boston kwa kuonyesha upinzani wao dhidi ya kodi ya Waingereza.

Waingereza walijibu 1774 kwa sheria kali mpya na wanajeshi wao walianza kukusanya akiba za baruti katika koloni. Hatua hii iliongeza uchungu na wanamgambo kati ya wakoloni walianza kufanya mazoezi ya kijeshi.

Viongozi wao wakaitisha mkutano wa kwanza wa wawakilishi kutoka koloni zote (Connecticut, Delaware, Georgia, Maryland, Massachusetts, New Hampshire, New Jersey, New York, North Carolina, Pennsylvania, Rhode Island, South Carolina, Virginia) wakaamua kwa pamoja kukataa biashara yoyote na Uingereza kwa muda wa mwaka mmoja hadi madai yao ya kupunguza kodi yatapokubaliwa, pia wakaanza kufanya mazoezi ya wanamgambo bila usimamizi wa Waingereza. Lakini hawakulenga bado kutafuta uhuru.


1775 Waingereza walitangaza koloni ya Massachusetts kuwa eneo la waasi na sheria ya kukataza wavuwi kutoka Marekani kuvua samaki katika Atlantiki.

Jaribio la wanajeshi wa kifalme toka Uingereza kukamata tena akiba za baruti kati ya walowezi lilisababisha mapigano ya kwanza ya kijeshi yaliyotokea tar. 19 Aprili 1775 karibu na mji wa Boston.

Wanajeshi waingereza walikutana na wanamgambo kwenye kijiji cha Lexington na baada ya kipindi cha kukutana walianza kurushiana risasi; wanamgambo 8 waliuawa.

Mapigano yalisamabaa pia kwenye vijiji vya karibu. Wanamgambo wengi walifika nje ya Boston wakawazingira Waingereza ndani ya mji.

Baada ya wiki mbili mkuu Mwingereza alijaribu kuwafukuza na mapigano ya Bunker Hill nje ya Boston yalitokea. Hii ilikuwa mapigano makubwa ya kwanza; waingereza walishinda lakini walipotea wanajeshi 226 waliouawa lakini wanamigambo walipotea wafu 140 pekee.

Sasa vita kamili ilisambaa. Mwanzoni Waingereza walikuwa na silaha na wanajeshi zaidi wakasogea mbele lakini wanamgambo wa walowezi wakioongozwa na George Washington waliendelea kuwashambulia.


KOLONI 13 ZAJITANGAZIA UHURU

July 4, 1776 koloni 13 (states) zilizo kando ya bahari ya Atlantic zilitangaza uhuru wa Muungano wa Madola ya Amerika.

Waingereza hawakukata tamaa, walisogea mbele wakatwaa pia mji wa New York. Lakini tangu 1777 Ufaransa ilianza kwa siri kutuma silaha kwa Wamarekani; mwaka 1778 Ufaransa, Hispania na Uholanzi ziliungana na kutangaza vita dhidi ya Uingereza. Manowari za Ufaransa zilishambulia meli za Waingereza zilizopeleka silaha na askari kwenda Marekani.

Mwaka 1781 sehemu kubwa ya jeshi la Uingereza ilishindwa kwenye mji wa Yorktown ikalazimika kujisalimisha. Tangu siku hii mapigano yalipungua na mwaka 1783 Uingereza ukakubali uhuru wa koloni zake za awali.

Wakazi wengi wa koloni walioendelea kusimama upande wa Uingereza walihamia Kanada iliyoendelea kuwa koloni.


United-states-territorial-acquistions-midcentury.png

KUPANUKA DOLA YA WAMAKANI

Nchi ilianza kama mkusanyiko wa makoloni 13 ya Uingereza kwenye pwani ya mashariki ya Amerika ya Kaskazini tangu karne ya 17. Walowezi kutoka Uingereza walijipatia ardhi wakipigana na wenyeji Wahindi wekundu.

Katika vita ya uhuru wa Marekani makoloni yalipata uhuru wao uliotangazwa mwaka 1776 na kukubaliwa na Uingereza baada ya vita mwaka 1783. Baadaye Marekani ilipanua eneo lake hadi bahari ya Pasifiki ikatwaa ardhi ya Wahindi wekundu wazalendo, ikapokea wahamiaji wengi kutoka nchi zote za Ulaya pamoja na watumwa walioletwa kutoka Afrika.

Tangu karne ya 19 wahamiaji walifika pia kutoka Asia,hasa China na Japani. Katika vita na Hispania na Meksiko Marekani ilipanua eneo lake kwenda kusini.

VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani vilipigwa kuanzia 1861 hadi 1865 kati ya majimbo ya kusini na majimbo ya kaskazini nchini Marekani.

Sababu mojawapo muhimu ya vita ilikuwa suala la utumwa. Majimbo ya kaskazini yaliwahi kupiga marufuku utumwa, lakini majimbo ya kusini yaliendelea na sheria zilizoruhusu utumwa na matajiri wengi wa kusini walitegemea kazi ya watumwa. Vita vilikuwa virefu na watu 650,000 walikufa, lakini mwishoni kaskazini ilishinda.
 
Haki inapokiukwa wananchi huwafanya waamke na kudai haki za msingi. Uingereza ilikuja kushtukia makoloni yake yakijitenga na kujitangazia uhuru mwambao wa bahari ya Attlantic tokana na:
  1. Shinikizo la Uingereza kutotaka makoloni kutokuwa na viwanda na hivyo viwanda vya uingereza viimarike na bidhaa kuuzwa kwenye makoloni yake.
  2. Kodi kubwa iliyotozwa ili kulipia gharama za uendeshaji serikali ya Uingereza na makoloni.
  3. Kutoruhusu makoloni kuwa na wawakilishi katika bunge la Uingereza.

Hao walikuwa ni waingereza walowezi wenzao waliokuwa wakikandamizwa na kunyimwa uhuru, baada ya kujitenga tumeshuhudia wimbi la wahamiaji toka nchi za Ulaya waliotaka uhuru zaidi na kuifanya Marekani kuwa ulimwengu wa ugunduzi wa makubwa mengi tunayofaidi sasa duniani.
 
Siku inakuja nayo I karibu sana.
 
Wanakuja tena kupigania tanzania baada ya uingeleza kuwapa pesa chadema ili wakishinda wapewe uwekezaji kwenye vitaru vya gesi,na wamarekani ambao wamefanya utafiti wa mafut wakitaka kuendeleza uwekezaji kwenye mafuta chi ni ya serikali ya ccm,shangilieni pasipo kujui kiini cha tatizo mtakuja kujua siku ya mwisho kama ilivyo kwa walibya sasa wameshutuka wakati sio wao tena,ndipo tutakapoona umuhimu wa kufatilia mamba au kuwa kasuku wasiasa.
 
Hayo ndiyo matatizo ya watanzania mnakubali kufunikwa na kinvuli cha amani wakati ndani yake kuna vita vikali jibu nikupambana
 
Back
Top Bottom