''Vita ya Barafu'' 1939 na fundisho kubwa kwa madikteta

''Vita ya Barafu'' 1939 na fundisho kubwa kwa madikteta

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Habari za jioni wanajukwaa nataka tusome uzi huu kwa umakini alafu mwishoni mtaelewa ujumbe naokusudia.
images (85).jpg

UTANGULIZI
Mnamo mwaka 1939 vuguvugu la vita kuu ya pili ya dunia lilishika kasi ambapo nchi hazikuaminiana na kulikuwa na kila sababu ya kuamini vita ingeanza wakati wowote hivyo nchi zote hasa za ulaya zilikuwa kwenye Alert ya juu sana. Ni wakati huu ambapo pande mbili kinzani yaani Axis powers za ujerumani,italy,japan n.k zilikuwa zinajipanga kuvamia mataifa ya Allies yaani USA,UK,USSR n.k hivyo ilikuwa ni muhimu kwa kila nchi kuzimeza vinchi vidogo ili kuongeza ulinzi kwenye mipaka yake hivyo Ujerumani ikavamia mataifa kadhaa madogo ya jirani ili yawe chini yake kama Poland,Austria,Hungary,Bulgaria n.k hivyo kutanua himaya yake na kuweka utawala unaosupport agenda ya NAZI ili kujiandaa na vita kuu. Ni katika wakati huu ambapo Urusi pia (USSR) chini ya DIKTETA Stalin ilipotaka kumeza nchi za jirani pia ili kutanua himaya na kujiandaa na kupambana na Hitler na ikameza vinchi jirani vidogo vidogo na katika wakati huu ndipo wakapanga kuivamia Finland yaani jirani yao upande wa magharibi ili wapate upenyo scandinavia wa kupambana na Hitler pia kulinda mji wao wa leningrad ambao ulikuwa kilometer chache tu kutoka mpaka wa Finland.

Kabla hatujafika mbali embu tupate data za Finland na urusi kidogo upande wa jeshi.

Nchi ya finland ilikuwa na wakazi million 3 pekee hivyo kuwa na jeshi la watu 180,000 wakiwa na jeshi la anga lenye ndege 130 za kizamani na vifaru 30 pekee. Upande wa Urusi walikuwa na jeshi linalovamia la watu 450,000, ndege 4000 na vifaru na gari vita 6000!!! Ni wazi kabisa nguvu hii ya mrusi ilizidi kwa mbali sana jeshi la Finland na hivyo matokeo ya vita yalifahamika hata kabla haijaanza.

VITA YAANZA
Novemba 30, 1939 ndipo jeshi la Urusi likaanza uvamizi wake upande wa mashariki wa nchi vifaru zaidi ya 1000 viliingizwa ili kuimaliza mapema vita na kuifanya finland kuwa taifa la kicommunist. Mwanzoni mwa vita ilikuwa ni ushindi mweupe kwa vikosi vya wavamizi lakini kama tujuavyo kwenye uwanja wa vita ukubwa wa jeshi,silaha na teknolojia sio uhakika wa ushindi bali MBINU ndio huamua matokeo ya mechi kama tu mpira ambapo Timu A inaweza kuwa na wachezaji dhaifu kuliko timu B ila wakatumia mbinu ya kukaba na counterattack unashangaa Timu A inaibuka na ushindi mzito bila kutarajiwa. Kwa muktadha huu pia finland walijua kwenye vita ya uso kwa uso hawana nafasi ya kumshinda wavamizi maana wamezidiwa jeshi zaidi ya mara 3 hivyo wakasugua kichwa ni mbinu gani waje nayo.

STRATEGY
Finland ni nchi yenye barafu na milima kwa wingi hivyo wakaamua kuitumia kama fursa ya kupata mbinu hivyo wakaja na jeshi dogo la ski-troopers ambao ni askari wa miguu wanaotumia vifaa vya kuteleza kwenye mabarafu kwa spidi kubwa sana hivyo kuwawezesha kufanya mashambulizi kwa haraka na ufanisi mkubwa bila kuonekana mapema na walivaa uniform nyeupe ambazo ziliwafanya wawe kama theruji hivyo kutoonekana kabisa kwenye uwanja wa vita.
8ddaf73f005292d40b195d120991971e.jpg

Mission ya kwanza ilikua kuzuia Vifaru zaidi ya 1000 vilivyotumika kuvamia. Kikosi hiki kilitumia formation ya kuzingira mbele na nyuma ya msafara wa vifaru kadhaa ambapo wakiwa na spidi yao waliweza tega mabomu kwenye upenyo wa kifaru nacho kulipuka hivyo walifanikiwa kuzuia shambulizi la vifaru vya wavamizi. Mnamo december 9 Stalin akaamua kuongeza vifaru ili kuimaliza finland lakini tactic ile ilitumika ambapo walijibanza vizuri kwenye milima kwa uchache wao na kuweza kulenga vifaru wakiwa mbali moja baada ya kingine vilizamishwa kwenye theruji hadi ikabidi warusi watulize mashambulizi kwa muda.

Vita iliendelea mpaka mwisho wa december 1939 ambapo waliamua kutumia upande wa kaskazini zaidi wa finland kuvamia ila bado walikutana na kikosi kidogo cha hao ski troopers ambao walikuwa na kazi ya kupaki basi na kushambulia kwa counter yenye spidi ya radi mwisho wa siku vikosi zaidi ya 7 vya warusi ( wanajeshi 70,000 ) walimalizwa kwenye mtanange huu. Kufikia january 1940 vifaru zaidi na majeshi yaliongezwa ila yalipitia vichakani lakini ski troopers bado waliendeleza moto na this time wakiligawa jeshi la Urusi kutokea kati ambapo walishambulia mbele na nyuma ya msitu hivo kuacha vikosi vilivo katikati visiwe na pakwenda na wengi wao walichinjiwa hapo na mateka kuchukuliwa.
images (84).jpg

Ilipofika February 1940 Urusi iliongeza wanajeshi zaidi ya 750,000 ila wakaona bado Finland licha ya kuwa na jeshi dhaifu ila limewazuia wakaamua Yaishe na wakasaini makubaliano ya amani na matokeo yalikuwa hivi. Urusi walikufa wanajeshi 320,000 ilihali finland walipoteza wanajeshi 70,000 pekee!!! Hivyo licha ya kuzidiwa nguvu ila huu unatafsiriwa kuwa ushindi mkubwa kwa Finland sababu licha ya kuzidiwa nguvu ila waliweza linda uhuru wao na kuzuia uvamizi ndio maana haikugeuzwa kuwa taifa la kicommunist.

HITIMISHO
Nilichotaka tujifunze ni kwamba kuna baadhi ya watawala fulani wanaodhani kwakuwa wana jeshi kubwa,mavifaru na mandege basi wanaweza onea wenzao bila kujua hao wapinzani wake licha ya uchache wao na udhaifu kirasilimali wakiwa na ''ski-troopers'' wao wachache ila wenye ufanisi wanaweza angusha utawala wake asubuhi na mapema sio kwa mitutu kama Finland bali kwa mbinu mbadala.

Never underestimate your opponent....
images (83).jpg

Field Marshal Karl Mannerheim Jenerali wa Finland wakati wa uvamizi wa dikteta Stalin

Naomba kuwasilisha
 
Kuna sehemu umeonyesha uwezo wa jeshi la Russia kuwa ni askari 450,000, na hapa unsema ''Ilipofika February 1940 Urusi iliongeza wanajeshi zaidi ya 750,000 ila wakaona bado Finland licha ya kuwa na jeshi dhaifu ila limewazuia wakaamua Yaishe na wakasaini makubaliano ya amani na matokeo yalikuwa hivi. Urusi walikufa wanajeshi 320,000 ilihali finland walipoteza wanajeshi 70,000 pekee!!! Hivyo licha ya kuzidiwa nguvu ila huu unatafsiriwa kuwa ushindi mkubwa kwa Finland sababu licha ya kuzidiwa nguvu ila waliweza linda uhuru wao na kuzuia uvamizi ndio maana haikugeuzwa kuwa taifa la kicommunist.
 
Ndio mkuu Urusi walikuwa na jeshi la 450 K wakati vita inaanza ila baadae walikomba wanajeshi na raia kutoka pande zingine za urusi ndio hao 750,000 au lugha ingine tungewaita reserves na ndio hao bado walibanwa wakaona isiwe tabu.... Hata Tanzania Jeshi letu halina askari wanaozidi elfu 50 ila reserves na wakati wa vita usishangae namba ya jeshi ikafika hata laki 5 !! Maana uhitaji huwa mkubwa na mtu yeyote anapewa hata mafunzo ya wiki 1 anaanza kuitwa mwanajeshi na kupelekwa uwanja wa vita so isikupe tabu kuitafsiri hiyo paragraph ya hao wajeshi 750 k
Screenshot_2018-12-07-17-36-39-1.png
 
View attachment 959325
Hiyo ndiyo inaitwa kipigo cha mbwa koko
 
Back
Top Bottom