Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima kwenu wanajamvi,
Kumekuwa na vita vya muda sasa baina ya kampuni mbili kubwa zinazojihusisha na usindikaji na usambazaji wa juice katika soko la Afrika Mashariki.Del Monte ya Kenya inatuhumiwa kuzuia juice za Azam zisiingie Kenya lakini wakiti huo huo wanasambaza bidhaa zao katika soko kubwa la Tanzania.Azam kwa upande wake baada ya kubaniwa soko la Kenya kwa muda mrefu imefanikiwa kuzuia bidhaa za Del Monte kuingia soko la Tanzania [haikufahamika mara moja njia walizotumia].
Zipo taarifa kwamba bidhaa za Azam zimezuiliwa kuingia nchi Kenya kwasababu ya kutokidhi viwango vya ubora nchini Kenya.Jambo hili lilipingwa na wataalam wa Azam ambao walitoa vielelezo vyote kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.Ifahamike Kenya imekuwa na utamaduni wa kulinda soko lake lisivamiwe na bidhaa toka mataifa mengine ya EAC.Mfano mzuri ni pombe aina ya Konyagi imezuiliwa kuingia soko la Kenya kwa kisingizio cha aina ya chupa inayotumika.
Nimefanya utafiti mimi mwenyewe Supermarket kubwa hapa jijini Ausha bidhaa za Del Monte (Juice) hazionekani na nilipowauliza wahusika nilijiwa hiki nilichokiandika.
Naomba kuwasilisha.