Vita ya biashara Del Monte Kenya na Azam Bakhresa Group of companies

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima kwenu wanajamvi,

Kumekuwa na vita vya muda sasa baina ya kampuni mbili kubwa zinazojihusisha na usindikaji na usambazaji wa juice katika soko la Afrika Mashariki.Del Monte ya Kenya inatuhumiwa kuzuia juice za Azam zisiingie Kenya lakini wakiti huo huo wanasambaza bidhaa zao katika soko kubwa la Tanzania.Azam kwa upande wake baada ya kubaniwa soko la Kenya kwa muda mrefu imefanikiwa kuzuia bidhaa za Del Monte kuingia soko la Tanzania [haikufahamika mara moja njia walizotumia].

Zipo taarifa kwamba bidhaa za Azam zimezuiliwa kuingia nchi Kenya kwasababu ya kutokidhi viwango vya ubora nchini Kenya.Jambo hili lilipingwa na wataalam wa Azam ambao walitoa vielelezo vyote kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.Ifahamike Kenya imekuwa na utamaduni wa kulinda soko lake lisivamiwe na bidhaa toka mataifa mengine ya EAC.Mfano mzuri ni pombe aina ya Konyagi imezuiliwa kuingia soko la Kenya kwa kisingizio cha aina ya chupa inayotumika.

Nimefanya utafiti mimi mwenyewe Supermarket kubwa hapa jijini Ausha bidhaa za Del Monte (Juice) hazionekani na nilipowauliza wahusika nilijiwa hiki nilichokiandika.

Naomba kuwasilisha.
 
Mkuu wangu Lastname unawezza kufafanua kidogo.Ina maana juice za Azam hazina ubora ?.


Ukweli ni kwamba: Azam biashara zake ujanja ujanja, de monte - Mkweli. Bidhaa za azam tunakunywa wa tz tusiokuwa na TBS na waburundi na wakongo nadhani
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu Lastname unawezza kufafanua kidogo.Ina maana juice za Azam hazina ubora ?.


Ukweli ni kwamba: Azam biashara zake ujanja ujanja, de monte - Mkweli. Bidhaa za azam tunakunywa wa tz tusiokuwa na TBS na waburundi na wakongo nadhani
 
Last edited by a moderator:
Ukweli ni kwamba: Azam biashara zake ujanja ujanja, de monte - Mkweli. Bidhaa za azam tunakunywa wa tz tusiokuwa na TBS na waburundi na wakongo nadhani


Mkuu wangu Lastname unawezza kufafanua kidogo.Ina maana juice za Azam hazina ubora ?.
Ngongo isome vizuri sentensi yake ndiyo utajua ubora wa Lastname kwa maana ya uwezo tu wa kujieleza achilia mbali kujua ubora wa bidhaa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu Lastname unawezza kufafanua kidogo.Ina maana juice za Azam hazina ubora ?.
Hazina ubora na ukitaka kujua kama una watoto wadogo kwako wape wanywe kwa week moja tu utapata majibu. Zina lots of allergies, tumbo kuuma watoto, vitu vingi saana. Nilipo wastop baada ya kupata ushauri toka kwa rafiki yangu sasa hivi shwari
 
Mkuu wangu Lastname unawezza kufafanua kidogo.Ina maana juice za Azam hazina ubora ?.

Usihangaike naye huyo ni typical Mtanzania! Hawa ndio watu waliokuwa wanashaangilia timu ya Brazili na kuwazomea Taifa Stars uwanja wa Taifa!

Ni mtaalamu wa kila kitu, anaongea tu ili mradi hata kama hana majibu! Adui wa Mtanzania ni sisi wenyewe badala ya kuwa Upande wa Azam, tunabaki kuteteta wageni!

Kwa kifupi ni hivi, Uchumi wa Kenya umeshikiliwa na Makampuni ya Kizungu hasa Waingereza, na hao wana lobi kubwa sana Serikalini, ndio wako nyuma wa kila aina ushindani kutoka nje, kuanzia Maua ya TZ mpaka Konyagi, na hayo ni makampuni makubwa lkn pia kuna makampuni madogo ya Watanzania waliojaribu kuwekeza Kenya wakapata upinzani wa ajabu mpaka wengine walitumiwa majambazi kama yule jamaa maarufu Tz duka la vipodozi nafikiri HM... kitu kama hicho mpaka alifunga virago, lkn pia kuna waliofanikiwa kupenya na wanafanya biashara kama COSEKE!
 
Wee Del monte hampati Azam hata mara moja Kenya wanatumia ujanja tu.Hizo del Monte mie niliacha kuzitumia kitambo hata Azam alikuwa hajaanza.ukifungua zile monte lazima kifuniko kitokee tena wanaweka sijui ngudi ya minyaaa maana haishiki kifuniko.Puuuuuuuu afadhali Azam na yeye kawaweza.
 
Ngongo isome vizuri sentensi yake ndiyo utajua ubora wa Lastname kwa maana ya uwezo tu wa kujieleza achilia mbali kujua ubora wa bidhaa

Sio kila kitu kinataka shule kwani darasani tulisomea juice za azam? Ila pia kumbuka bidhaa zake zina sukari nyingi sana na kama mnavyojua mnaotaka kujua sukari sio nzuri kwa afya ya watu na ndio maana wengine kama akina Ceres wanaandika kwamba no sugar added ili kuonesha ni jinsi gani product zao zina risk kidogo. Kwa matatizo kwa watoto asiyekubari ajaribu azam embe, utakuja kutuambia humu
 
Wakuu,

Ipo mifano mingi sana ambayo inadhihirisha wazi Kenya soko la EAC ni kwaajili ya kuuza bidhaa zao tu hawataki bidhaa za nchi nyingine mwanachama ziingie katika soko lao.

Niliwahi kufanyakazi General Tyre,tulikuwa tunapeleka tyre Kenya ambazo zilikuwa na soko kubwa sana na walijitokeza deals waliokuwa wakizpeleka mpaka Somalia.Warasimu wa serekali ya Kenya walipogundua wakaanza kuweka vikwazo,kuna wakati mzigo ulikuwa unakaa mpakani Namanga mwezi mzima.Pata picha General Tyre ni shirika la umma.

Kampuni ya kusindika nyama SAAFI ya Dr Mzindakaya Maji ya tanga aliwahi kukumbana na urasimu nyama nyingi iliharibika.Jiulize hili soko la EAC liko kwaajili ya nchi ya Kenya kuuuza bidhaa zake na si kununua toka nchi nyingine ?.
 

Siwezi kukusifu eti ni Mtanzania mwenzangu hata kama bidhaa zako feki, by the way Mtanzania yuko wapi pale? bakhresa? hahhahaha
 

Unajua Serikali yetu nadhani kuna mahala imebweteka katika kuwalinda wazalishaji wa ndani, nchini Kenya wanaziwekea zengwe bidhaa za Tanzania lakini sisi tumelala tu tunaacha mibidhaa yao inaletwa kila kukicha, hebu angalia alijitokeza jamaa mmoja alikuwa anachukua maziwa mtindi, yogart na bidhaa zoote za Maziwa ya Mara, alikuwa anapeleka Kenya na zilianza kupendwa sana aliwekewa fitna mpakani kipindi fulani na Serikali ya Kenya mpaka mzigo wake uliharibika na from then mpaka leo swala lake halijawahi kuzungumzwa na Serikali ya Tanzania na hata kama ukiona juice za Del monte haziji Bongo ujue ni juhudi binafsi za ushindani za Bakhressa na sio kwamba kuna namna serikali imempa chapuo
 
Mkuu wangu Mvaa Tai nimekupata unachosema ndiyo hali halisi nadhani ifike mahali serekali na wizara ya EAC ziweke mkakati wa uwazi namna itakavyokabiliana na vikwazo vya kibiashara vinavyowekwa na Kenya.

 
Last edited by a moderator:
Bakhresa njoo hapa JF ujibu hoja za msingi
najua ni Member hapa .
 
Kenya wanafanya hila kuzuia bidhaa bora za tz kuingia soko lao sie serikali yetu imelala haitoi support kwa watz wajasiriamali kuna wakat kenya airways walikua wanawazingua watz wanaopeleka bidhaa za horticulture dubai wanawaambia wazisafirishie through nairobi ili ionekane zimetoka kenya na si tz na thanx to ethiopia airline iliokoa watz ndo kq wakabadilika
 
Ukweli ni kwamba: Azam biashara zake ujanja ujanja, de monte - Mkweli. Bidhaa za azam tunakunywa wa tz tusiokuwa na TBS na waburundi na wakongo nadhani

Wanasema bakresa hanywi maji ya azam anatumia george weah brand ... Nakubaliana na wwwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…