Vita ya biashara Del Monte Kenya na Azam Bakhresa Group of companies

Del monte chanzo chake hasa ni kampuni ya wamarekani ambayo ilianza kazi miaka ya 1960s' hivyo ni watu waliokwenye game ya kutengeneza juice na kusindika vyakula mbalimbali kwa kiwango cha kimataifa na kwa muda mrefu sana,baadaye waliuza share zao nchi mbalimbali kenya ikiwemo,soko la del monte na ubora wake ni wa viwango vya juu sana ata ukinywa juice iliyotengenezwa na del monte ya usa au nchi nyingine formular yao ni moja..ni sawa na unapokunywa coca ya china na ya tz ni kitu sawa tu...del monte juice ya kenya wawezaiona kwenye supermarket dunia nzima..so azam juice haiwezi shindanishwa na del monte juice katika ubora..juice zao nyingi del monte ni organic yaani hawategemei zaidi madawa katika uzalishaji wao
 
Ukweli ni kwamba: Azam biashara zake ujanja ujanja, de monte - Mkweli. Bidhaa za azam tunakunywa wa tz tusiokuwa na TBS na waburundi na wakongo nadhani
Tengeneza za kwako sasa maana hapa bongo mtu akipiga hatua ha2pendi kuinuana,kitumbua akiuza mama chaupele mnaita kichafu ila akiuza mzungu mnadai ki2mbua cha kizungu!!tuacheni majungu tusapotiane!!


Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Watanzania kwa kawaida hatuna uzalendo hivyo sishangai sana. Kenya wana kawaida ya kuweka vizuizi mbalimbali kwa bidhaa za mataifa mengine ya e.a.c kwa vijisababu vya ajabu ajabu hasa bidhaa za viwandani. Halafu unakuta mijitu imekaa tu inashangilia. Azam ameajiri watz wangapi kuanzia wakulima, vibarua kiwandani, wachuuzi wa bidhaa zake nk. Mfano mzuri maziwa yaliyosindikwa toka tz, nyama, juice, vinywaji baridi, vinywaji moto hivyo ni baadhi peleka kenya vitazuiwa mpakani. Nenda na mahindi, maharage na mchele wala hakuna neno. Siwapendi wakenya kwa hii tabia kwa kweli. Sorry kwa wafuasi wa kenya.
 
Ikumbukwe kuwa Utamaduni wa kusindika vyakula tz imeanza karibuni sana wakati wenzetu walianza miaka 50 hadi 100 iliyopita. Tofauti inaweza kuweza kuwepo ila si kubwa kiasi hicho. Ebu check bidhaa hizi zilipoanza kutengenezwa na maendeleo yake kwa sasa
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1362681111.003777.jpg
    3.2 KB · Views: 599
  • ImageUploadedByJamiiForums1362681122.613260.jpg
    6.8 KB · Views: 600
Hazina ubora na ukitaka kujua kama una watoto wadogo kwako wape wanywe kwa week moja tu utapata majibu. Zina lots of allergies, tumbo kuuma watoto, vitu vingi saana. Nilipo wastop baada ya kupata ushauri toka kwa rafiki yangu sasa hivi shwari
nyingi ni kemikali tupu na kama juice halisi ipo kwa baadhi ni kidogo sana. Wanaopenda kuzitumia waendelee LAKINI kiafya hazifai.Kwa juice hizo Kuwa na nembo ya TBS au hata TFDA haina maana yoyote
 


AZAM ameajiri Watanzania wangapi au waislamu wangapi??
 
Ukweli wenzetu wanalinda sana soko lao la ndani, kuweza kupenya soko la Kenya mara nyingi ni mpaka kuwe na upungufu wa hiyo bidhaa. Na mara nyingi vitu ambavyo vina kuwa na masoko Kenya ni vile ambavyo haviko processed kama mazao ie. mahindi, vitunguu, jamii ya kunde n.k.

Kuna kipindi nilisikia hata unga wa mahindi packed kutoka tanzania walikuwa wanazuia usiingia Kenya, at the same time wao wanataka wauze Tanzania. Wapo wanaoshabikia kwamba bidhaa za Azam hazijakidhi ubora but cna uhakika na utetezi huo. Wakenya wanalinda soko lao na katika kujilinda lazima waweke mizengwe, na mizengwe yenyewe ndo kama hvyo..

Watanzania tujitahidi kupenda vya kwetu tuache kushabikia bidhaa za nje. Hamna kitu kibaya alichokipanda MKOLONI katika vichwa vyetu kama kujiona sisi siyo kitu. Pamoja na kwamba tupo huru lakini kuna Watanzania wengi sana ambao ni watumwa kifkra, wakiteswa mno na colonial legacy.

Babu zetu walitawaliwa directly but kizazi cha sasa kimebakia kutawaliwa indirectly kwenye fahamu zao. Na hapa ndipo unapohitajika mtaala wa elimu kuwafungua watoto kuanzia chekechea ili watakapo kuwa watu wazima wawe na ufahamu wa kujitawala wenyewe bila kuwa na utegemezi wa watu wa nje.

Nawakilisha.
 
Hazina ubora na ukitaka kujua kama una watoto wadogo kwako wape wanywe kwa week moja tu utapata majibu. Zina lots of allergies, tumbo kuuma watoto, vitu vingi saana. Nilipo wastop baada ya kupata ushauri toka kwa rafiki yangu sasa hivi shwari

Acha majungu kijana, ni watoto wangapi wanakula bidhaa za ssb na hawasumbuliwi na kitu? we haujiulizi kwa ukubwa wa soko la azam ikitokea tatizo katika bidhaa yake si jambo la kuficha! walee wanao inavyotakiwa, unaona mtoto anaumwa MPELEKE HOSPITALI AKAPIMWE!!
 
ebana jombaa nakubaliana na wewe nina niece wangu mdogo analalamika tumbo tumbo anapenda sana juice ya embe kumbe ni tatizo hilo
 

Huyo ni mtumwa ,mimi nikiingia dukani juice made in kenya sinunui
 
ajila kwa azam unajitambulisha kwa dini. nenda pale usikie majina yao. nafuu hata seminari za kiislam. mia
Acheni majungu wekeni utaifa mbele pale azam kuna wazungu wameajiriwa je na wao waislam?na hata kama waislam kwani sio watz acha udini wewe hapa tunapambana na wakenya wao pia wana ukabila mbona wanaungana kuzitetea bidhaa zao tanzania kwanza
 
Nimeisoma post mwanzo mwisho. Kinachojitokeza hapa kinatia wasiwasi. Awali ya yote ni uelewa mdogo na tabia ya dharau iliyojengeka miongoni mwetu. Hili la Bakhresa ni sehemu ndogo tu ya tatizo. Bakhresa nayo pia inatakiwa kubeba lawama ya kupuuzwa na Watanzania. Mbali na matangazo mengi kwenye radio, tv, mabango na vipeperushi, bado wengi wetu hatujui Bakhresa anafanyaje mpaka juisi na soda zake zinatufikia. Kila linalozungumzwa ni 'nasikia' hiki nasikia kile. Sidhani yupo Mtanzania ambaye anaweza akaitetea BFP awapo nje ya nchi. Haijui. Ukisema kaajiri waTZ wengi, sikatai. Lakini asilimia kubwa ya waajiriwa ni Wahindi na cha kusikitisha wengi wanajifunza kazi hapo hapo na kwa vile ni 'expatriate' ni wanyanyasaji wakubwa. Kwa wale walioingiza dhambi ya 'udini', uhakika na hili sina ila tunazungumza jambo zito kama hilo, tusilifanye kana kwambo ni gumzo la kawaida. Tulipe uzito unaostahili ikiambatana na takwimu au matukio yatakayo tia uzito tamko lako. Mwisho, naomba Watanzania wajitokeze na kupinga wazi wazi ama kwa kutaka maboresho ya bidhaa yafanyike au kususa bidhaa zenyewe. Nguvu ya soko itamrekebisha au kunuondoa sokoni. Penye sifa pasifie, ingawa inauma na pabovu pabainishe sote tujuwe.
 
Duh, kuuuuumbe!!! Basi Azam anisahau, kuanzia timu yake ya mpira, boat mpaka maji yake!
 
nina concern moja tu ..... sidhani kama bakhresa anakunywa maji ya uhai ambayo anatengeneza yeye mwenyewe .... if that is true then why?

siku njema
 
Kuna uwezekano juice za Azam hazina ubora hili sina uhakika lakini mbona bidhaa kibao za Tanzania zinazuiliwa.Nimetoa mfano wa Tyres za General Tyre 750 - 16 HCT 10ply zimefanya vuziri sana Land Cruser zote zilizokuwa zinashiriki mapigano Somalia zilikuwa zimevalishwa hizi tyres.Hapa Tanzania Land Cruiser au Land Rover zote za porini (utalii) zilikuwa zinatumia hizi tyres mifano ni mingi.Kiwanda cha kusindika nyama SAAFI kinazalisha nyama zenye ubora wa hali ya juu bidhaa zake zimekubalika Malawi,Comoro,Zambia,UAE na nchi kibao kwanini Kenya zinazuiliwa ?.
 
Udini mwingi sana Azam. Na azam embe ni mbya kwa watoto hata watoto wangu hulala mika sana tumbo leo baada ya kusoma maoni ya watu nimenunua azam kubwa ya mango watoto wameanza kulalamika tumbo. Ningeshauri wafanyie kazi haya maoni ya wat. Mbona bidhaa nyingine tunazitumia na ni nzuri? Mfano unga wa ngano, nazi, maji makubwa nk. Ila udini duhh nadhani azzam inaongoza kwa kuajiri watu wa dini moja kwa zaidi ya 99%. Mpaka huwa najiuliza hii ni taasisi ya kiislam?
 
mhhh Delmonte zilikuwa nzuri bwana mie nilikuwa mteja wao mkubwa, yeah ni kweli sijaziona mda mrefu sana madukani kama ndo hivyo ni poa, ingawaje na azam waounguze masukari kwenye juice zao
 
Sababu kubwa mi kuilinda shilingi yao isije ikadhuka thamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…