Loading failed
JF-Expert Member
- Sep 14, 2023
- 2,603
- 7,501
Ndugu zangu...
Tumekua tukishuhudia, kuona na kusikia huko Congo DRC kukiwa na vita kali kati ya M23 na majeshi matiifu ya serikali, halikadhalika M23 wakinukuliwa kuwa na silaha nzito kuliko majeshi ya serikali , kuwashinda nguvu na kuwafurusha vikali pamoja na kuua wanajeshi wa Congo , pia kunyakua miji kirahisi sana huku wakisababisha mtafaruku wa ukosefu wa amani pamoja na vifo baina ya raia wasiokua na hatia miaka na miaka.
Maswali;
1: Kama kweli vile vikosi vya kulinda amani vipo pale kulinda amani ni kwanini hawapigani na maadui moja kwa moja pindi wanapo hatarisha amani ya watu wa congo, ni kwanini basi wasiingie vitani rasmi kupambana na M23 moja kwa moja?
2: Kwanini vile vikosi vyote vya kimataifa visiondolewe alafu congo iundwe upya na wajitangazie uhuru wao mpya tofauti na wa hawali kutokana na M23 kuendelea kusumbua ili hali wao wapo pale kulinda amani?
3: Je, vita ya Congo ni laana, adhabu na mateso ya malipo wanayolipa raia wa Congo iliyotendwa na mababu zao kwa kumuua Patrice Lumumba na kama ni laana je, kwanini hizi imani zetu zisitumike kuwaombea toba / msamaha kwa Muumba wao ili wa kae kwa amani na kama hazina nguvu kwanini tunaendelea kuziamini na kushikilia imani zisizoweza kusaidia ndugu zetu kwa kuwatoa matatizoni?
4: Kama ni kweli Rwanda inawapa ushirikiano M23 kama inavyodaiwa ni kwanini basi Raisi wa Congo au mkuu wa majeshi wa Congo asitangaze vita rasmi ya moja kwa moja kuivamia kijeshi na kuipiga Rwanda kwa kuatarisha amani ya raia wa Congo?
5: Kama Serikali ya Congo na Jeshi lake limeshindwa kupambana na M23 ni kwanini basi wasione ni vyema kuuza mji wa GOMA na viunga vyake kwa waasi ili raia wawe salama ?
6: Kwanini Congo hawataki kuigawanya iwe nchi mbili kama ilivyogawanywa sudani?
7: M23 wanapata wapi silaha nzito , mafunzo ya kijeshi na kuzitumia na zinapitia wapi, na kwanini wasipige huko zinakopitia na kuweka kambi imara za jeshi la congo ili kufunga milango ya kuingiza silaha na misaada kwa M23?
8: Je, mataifa ndani ya AU, EAC na SADC wanamtazamo gani kuhusu kuikomboa Congo ili liwe taifa huru, je , kwanini wasiweke vikwazo kwa taifa litakalo sadikika kuunga mkono hawa M23 na ikibidi ilipige moja kwa moja ?
9: Kama serikali ya Congo imeshindwa kabisa kupambania amani ya raia wake , ni kwanini wasilitoe sadaka Taifa la Congo liwe chini ya M23 na wajiundie serikali ili raia wawe na amani?
10: Kama mataifa ya Afrika yameshindwa kuisaidia Congo kuwafurusha , kuwaangamiza na kuwateketeza kabisa hawa M23 na vikundi vinavyofanana na hivyo kwanini Raisi wa Congo asiombe msaada kwa Rais wa Urusi ( Putin) amsaidie kuwafurusha waasi vikali?
11: Kama shida ni rasilimali zinazo patikana pale , ni kwanini basi serikali ya Congo isikabidhi maeneo hayo rasmi kwa jeshi tiifu yasimamiwe kijeshi na kwanini isiweke kambi za kijeshi mipakani na kuzunguka maeneo yote zilizo na rasilimali za madini ili waasi na mafisaidi iwe rahisi kushughulikiwa kikamilifu?
12: Ni kwanini raia wa mataifa mbali mbali ikiwemo yale ya ughaibuni hawaiombei Congo amani na kufanya maandamano kama vile walivyokua wanafanya ya free palestina ili dunia isikie na iwasaidie wakongoman?
13: Ni ipi hatima ya raia wa Congo iwapo majeshi yote yatashindwa kupambana na M23?
Naombeni kuwasilisha . Ni yapi maoni yenu kuhusu haya yanayojiri huko Congo miaka na miaka..