Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Falklands
ni visiwa vilivyoko kwenye ukanda wa pwani ya Argentina. Visiwa hivi vilikuwa vya Argentina hadi miaka ya 1833 vilipochukuliwa na Uingereza inayovimiliki mpaka leo. Mwaka 1982, Argentina ilivamia visiwa hivyo vya Falklands kutaka kuvichukua kwa nguvu. Wakati huo uchumi wa Uingereza ulikuwa katika hali mbaya sana na Argentina ilidhani kuwa Uingereza haitavitetea kutokana na kuwa viko mbali sana na Uingereza. Kwa bahati mbaya sana Argentina ilifanya kosa ambalo lilikuwa kuwafedhehesha sana katika historia ya hivi karibuni kwani Uingereza ilivitetea na kuyashinda majeshi ya Argentina ambayo yalikuwa mengi na yana base za karibu sana kutoka nchi kavu.
Pamoja na ushindi huo, uchumi wa Uingereza uliharibika sana baada ya vita hiyo, ni kama ambavyo uchumi wa Tanzania ulivyoharibika baada ya vita ya kutetea Kagera dhidi ya Uganda. Bendi ya UB40 ambayo jina lake linalotokana na form ya Unemploymenet Benefit Number 40 iliundwa kipindi hicho kwa vile vijana walikuwa hawana kazi tena bali walikuwa wakiishi kwa posho ya Unemploymenet Benefit (dole).

Last edited by a moderator: