Vita ya Kiuchumi: Ningekuwa Rais wa Tanzania ningeanzisha ujenzi wa reli ya SGR kutokea Bandari ya Tanga hadi Kagera, Rwanda na Uganda

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Amani iwe nanyi wanabodi!

Kupitia Northen Corridor Kenya anataka kuingia DRC, Rwanda, Uganda na Sudan Kusini kwa Reli ya SGR.

Sisi Tanzania tunajenga SGR yetu kuingia Burundi na baadae Congo.

Kwa hesabu za haraka huko mbeleni SGR ya Kenya ndo itakayoleta faida zaidi kwa Kenya kuliko SGR yetu maana wao wataingia Congo pia tunapotaka kuingia sisi huku wakiingia Rwanda, Uganda na Sudan Kusini.

Kijiografia ni gharama ndogo sana kuingiza SGR Rwanda kutokea Tanzania compared na gharama zitakazotumika kuiingiza SGR Rwanda kutokea Kenya kupitia Uganda ambapo mpaka sasa ujenzi haujaanza.

Pia ni faida na rahisi zaidi kwa Rwanda kufanya biashara kupitia Tanzania endapo watatumia SGR yetu hasa pale tutakapoweza kuifikisha Rwanda.

Sio hivyo tu, ni rahisi kwetu zaidi kuipeleka SGR Kagera alafu ikaingia Uganda jambo ambalo linaweza kuishawishi zaidi Sudan Kusini kutumia SGR hii na kupitisha mizigo yake Tanzania

Mwisho haya yote yatazishawishi zaidi nchi za Uganda na Rwanda na baadae Sudan Kusini kupitisha mizigo yao Tanzania endapo tukianza sasa kujenga kipande cha SGR kutoka Bandari ya Tanga kuelekea Tabora-Geita- Kagera - Rwanda- Uganda ambapo ni rahisi kwa usafirishaji wa mizigo kuelekea na kutoka nchi za Asia na Australia kuliko ilivyo kwa Bandari ya Mombasa na hata Lamu.

Soma Pia:
Kwa Dunia ilipofika sasa hasa kiushindani katika kupata maendeleo ya kiuchumi ni lazima Tanzania ichukue hizi Drastic measures haraka sana ili kujihakikishia nafasi ya juu kiuchumi miaka mingi ijayo na kama the logistic hub for East and Central Africa.

Rais Samia
Rais wangu kipenzi. Itisha kikao cha Baraza la Mawaziri, ridhieni na anzisheni mambo yafuatayo;

1. Ujenzi wa kipande cha SGR kutoka Bandari ya Tanga kueleka Kagera- Rwanda na Uganda

2. Kuanzisha haraka mradi wa kupanua zaidi Bandari ya Tanga

3. Kuanza kuwashirikisha Rwanda, Uganda na Sudan Kusini mpango huu haraka sana.

Duniani hapa principle kuu ya maendeleo ni Ubaya Ubwela. Maximise your potentials mje kukumbukwa na vizazi vyote vya Tanzania hadi mwisho wa dunia kwa kufanya maamuzi ya maana yenye faida kwa nchi hii.

Lord denning Dar es Salaam!

Screenshot_20240810_095121_YouTube.jpg
 
Hapa uliponda SGR, je nani atachukua mawazo ya mtu kama wewe? Tol
 
Sio lazima uwe raisi

Jenga hoja uelweke
Kuna ngazi mbalimbali za kushirikisha
Maendeleo ni wote
 
Unayoyaongea yote yapo kwenye pipeline, tena zaidi ya hayo.

Upeo wako mfupi sana.
 
Kuongea ni rais sana hiyo miradi inahitaji hela
Kama reli ya dsm mpaka dodoma serekali imekopa mpaka ipo icu ndo sembuse mpaka uganda au rwanda
 
Hapa uliponda SGR, je nani atachukua mawazo ya mtu kama wewe? Tol
Hoja ya kuboresha Tazara ni ya msingi bado.

Mizigo mingi inayopita Tanzania inakwenda nchi za ukanda inapopita Reli ya Tazara!

Mawazo pia huwa yanaboreshwa. Kwa Wachambuzi makini na think tanks, Kenya anaonekana kajipanga kwa Reli kumletea faida zaidi kuliko sisi! Ndo mana mawazo mazuri katika kuboresha lazima yatolewe
 
mkuu, tayari bandari ishapanuliwa meli zinazotia nanga tanga ni sawa na zile za dar na tayari kuna ongezeko kubwa la meli. kuhusu sgr, kutoka tanga kwenda kagera kupitia wapi? geographia hairuhusu, kuna bonde la ufa, kuna mbuga ya serengeti na kuna lake victoria,

Lakini pia wazo lako lilishafanyiwa kazi kuna bomba la mafuta kutoka hoima kwenda Tanga nalo lina manufaa sawa au zaidi ya sgr.

ushindani na kenya hizo ni siasa tu strategycally kenya sio mshindani wetu mshindani wetu ni africa ya kusini na angola hilo somo nitaleta siku ingine.

Sgr ya tz na kenya kuwa katika ushindani, sgr yetu inatumia umeme ina rated speed ya 160mph, ya kenya inatimia diesel rated speed ni 120kph, hivyo yakwetu ipo kwenye best comperative advantage. treni ya kenya itatumia lita za diesel elfu 20 sawa na 70m za kitanzania wakati yakwetu itatumia umeme wa lakitano tu kugika kigali. niishie hapa kwa leo
 
Unayoyaongea yote yapo kwenye pipeline, tena zaidi ya hayo.

Upeo wako mfupi sana.
Yapi hayo yapo kwenye pipeline?

Yamesemwa wapi kuwa yapo kwenye pipeline?

Upeo unakuwaje mfupi kwa mawazo haya? Au chuki zako tu bibi?
 
Sio lazima uwe raisi

Jenga hoja uelweke
Kuna ngazi mbalimbali za kushirikisha
Maendeleo ni wote
Uwe unasoma vizuri. Kichwa cha mada kimesema hayo na kwenye content ameshauriwa Rais aliyepo afanye hayo!
 
Hapa uliponda SGR, je nani atachukua mawazo ya mtu kama wewe? Tol
Huoni kwa hilo wazo hapo Serikali wameanzisha mazungumzo na China kuboresha reli ya TAZARA kwa kiwango cha SGR. Au hujamsikia Rais Samia?
 
mkuu, tayari bandari ishapanuliwa meli zinazotia nanga tanga ni sawa na zile za dar na tayari kuna ongezeko kubwa la meli. kuhusu sgr, kutoka tanga kwenda kagera kupitia wapi? geographia hairuhusu, kuna bonde la ufa, kuna mbuga ya serengeti na kuna lake victoria,

Lakini pia wazo lako lilishafanyiwa kazi kuna bomba la mafuta kutoka hoima kwenda Tanga nalo lina manufaa sawa au zaidi ya sgr.

ushindani na kenya hizo ni siasa tu strategycally kenya sio mshindani wetu mshindani wetu ni africa ya kusini na angola hilo somo nitaleta siku ingine.

Sgr ya tz na kenya kuwa katika ushindani, sgr yetu inatumia umeme ina rated speed ya 160mph, ya kenya inatimia diesel rated speed ni 120kph, hivyo yakwetu ipo kwenye best comperative advantage. treni ya kenya itatumia lita za diesel elfu 20 sawa na 70m za kitanzania wakati yakwetu itatumia umeme wa lakitano tu kugika kigali. niishie hapa kwa leo
Kuna maeneo uko sawa ila kuna maeneo umepuyanga kihoja.

Hakuna shida yoyoye kwa SGR kupita kwenye bonde la ufa. Kama tenajenga mji wa Serikali kwa gharama kubwa Dodoma ambapo napo kuna njia ya tetemeko tunashindwaje lupitisha tu reli kwenye maeneo hayo?

Kuhusu nchi shindani za Tanzania hapo pia umekosea. Kenya ni mshindani wetu hasa maana hiyo mizigo ya nchi za Sudan Kusini, Rwanda, Congo Kaskazini na Uganda haziwezi kupita Afrika kusini au Angola.

Mwisho kwa ramani ya Tanzania reli ya SGR haina shida yeyote kufika Kagera. Inaweza kutoka Tanga, ikapita ikaingia Dodoma na kuungana na hii iliyojengwa.

Kutoka Isaka kuelekea Mwanza tunaweza kujenga njia nyingine ambayo itaingia Geita_ Kagera na Kisha Rwanda na Uganda

Ni mipango na matumizi tu.
Screenshot_20240810_121901_Adobe Acrobat.jpg
 
Watu wapo nyuma ya keyboard wanaongea tu kirahisi
Kama tunamwaga pesa namna ile kujenga Makao Makuu Dodoma tena hadi kwa vitaasisi kwa mabilioni ya pesa tunashindwaje hili?

Sema kama tumekosa vipaumbele tu ila kama TCRA tu ambao wana jengo la uhakika pale Dar es Salaam wnajengewa jengo jingine Dodoma ndo tushindwe kufanya hili?
 
JPM alikuwa chuma kweli,

Ila alizingua sana kuforce kuhamisha makao makuu ya taasisi nyingi aiseee
 
Sahihi kabisa. Kuhamia Dodoma ni wazo zuli ila kule zingeamia Bunge, Mahakama na Mawizara tu. Kuhamishia hadi vitaasisi Dodoma ni ufujaji wa pesa tu na kukosa vipaumbele!
 
Kifupi mleta mada Una akili finyu unawaza tu kufungua nchi nyingine kimizigo sio nchi yako kufunguka kimizigo

Huko SGR inakopita sasa kuna mizigo mingi na biashara kubwa mno ya ndani ya nchi

Mfano makampuni ya Mafuta Yana mizigo mingi kutoka Dar kuyapeleka kote inakopita SGR ,pia Mikoa inakopita SGR kuna uchumi mkubwa WA mazao na mifugo na madini ya kusafirisha kutoka huko kwenda kwingine ikiwemo nje ya nchi

Unapojenga miundombinu huwazi Tu kufungua nchi ya mwenzio cha Kwanza ni kufungua njia yako ndani ya nchi Kwanza nchi ifunguke kila Kona ndipo baadaye uwaze jirani

Wewe unaandika kama vile Sisi tuwagharimie kufungua nchi zao as if Sisi hatuna cha kufungua nchi yetu
.mawazo duni Sana hayo
 
Ukielewa faida ya ujenzi wa reli ni ipi huwezi kuandika mashudu uliyoandika hapa.

Faida ya ujenzi wa reli hii ni kusafirisha mizigo ambapo gharama za usafirishaji huo ndo pesa zitakazoinufaisha nchi.

Sie tukiacha kufanya maana yake anayekwenda kufanya kile tulichopaswa kufanya ndiye atakayenufaika zaidi
 
Back
Top Bottom