Vita ya Nishati yanukia Afrika

Vita ya Nishati yanukia Afrika

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Rais SSH anasema mgawo wa umeme unaoendelea hivi sasa JMT hautokani na hali ya hewa (ukame) bali ukarabati wa mitambo na miundombinu ya usambazaji, inabidi mitambo mingine izimwe isifue umeme ili iweze kukarabatiwa.

Waziri wa nishati Januari Makamba (wa wakati huo) alikaririwa akisema gridi ya taifa inahitaji ukarabati wa thamani ya Tzs.1tr.

Eng. Boniface Gissima Nyamohanga Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco alinukuliwa na mtandao mmoja wa habari akisema mwaka 2023 taifa linazalisha MW 1900.

Kwa macho ya kila mtu, hivi sasa na upungufu huu, hizo MW zinazalishwa? Alisema 65% ya hizo MW zinatokana na gesi asilia (siyo umeme wa maji).

Naamini tumeshuka chini ya MW 1650 za awamu ya 5 ambayo nayo ilikuta MW 1226.

Tusipoharakisha JNHPP tutapoteza soko la umeme nje ya nchi kwa sababu wafuatao wanajiandaa kuuza huko umeme:-

1. Ethiopia wamejenga Bwawa la zaidi ya MW 6600, wanazalisha MW 4430 ktk vyanzo 14, wanatafuta MW 14,000.

2. DRC wanajenga Bwawa la MW 15,000 wanaweza kuangaza Afrika Kusini mwa Sahara nzima.

3. Bwawa la Cahora Bassa linazalisha GW 5.15 wanaweza kuangaza Afrika nzima.

4. JMT tunachechemea na Bwawa la MW 2115.

5. Global Gateway ya EU inawekeza kuvuna upepo wa Kalahari Namibia kufulia umeme wa GW nyingi kutosha kulisha Afrika kufuatia Kalahari kuwa na utajiri mkubwa sana wa upepo.

Tukumbuke principle ya biashara ya anayewahi sokoni ndiye anayedhibiti soko.

Matokeo yake Afrika inaenda kuingia kwenye vita ya nishati kugombania soko.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Tukichukulia poa, tunaachwa nyuma na wenzetu
 
Back
Top Bottom