Vitabu vya marehemu Ben Mtobwa

Vitabu vya marehemu Ben Mtobwa

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
4,195
Reaction score
2,678
Kwa wale wapenzi wa riwaya za Hayati Ben Mtobwa, ambaye mpaka sasa tumeweza kufikisha riwaya aina 15 zikiwemo riwaya za kipelelezi zinazombeba Joram Kiango kama mpelelezi hodari anayeweza kufumbua mafumbo mengi yanayotukia kwenye jamii.

Mbali na hapo, kuna riwaya za kijamii kama Zawadi ya Ushindi, Pesa zako zinanuka na Dar es Salaam usiku.

Bila kusahau, riwaya za kihistoria kama Kiguu na Njia ambayo inaelezea historia ya nchi yetu kabla na baada ya uhuru. Lakini pia katika kitabu cha Kimbia Helena Kimbia, tutaweza kupata historia ya vita vya Rwanda kwa njia ya riwaya. Mhariri Msalabani ni historia ya Hayati Ben Mtobwa mwenyewe akielezea changamoto alizokutana nazo wakati akijaribu kuendesha kampuni yake ya Heko. Mbali na hapo, utaweza kusoma historia yake yangu anazaliwa mpaka kufa kwake katika sehemu ya pili ya kitabu hiko.

Bei za vitabu ni shilingi elfu Kumi kwa kimoja isipokuwa;
1. Kimbia Helena Kimbia 5,000
2. Kiguu na Njia 15,000
3. Mhariri Msalabani 6,000

Kwa anayehitaji tafadhali tupigie kwa namba 0712504985 au 0763044459.
Ahsanteni na karibuni sana.
20200827_073750.jpg
 
Back
Top Bottom