Vitalis Maembe, Carola Kinasha na irene Sanga ndo kina Tracy Chapman wetu

Vitalis Maembe, Carola Kinasha na irene Sanga ndo kina Tracy Chapman wetu

Geka

Senior Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
176
Reaction score
41
Ujumbe uliomo kwenye mashairi /nyimbo zao hauhitaji wavae mavazi ya uchi kuutambulisha muziki wao. Kama unafahamu zaidi kuwa huru kuchangia lakini baadhi ya nyimbo zao ni

Maembe: Sumu ya Teja

Kinasha na bendi yake ya Shada: Maono album

Irene Sanga: Mashairi ya wimbo wa mpoto Mjomba

Tracy Chapman, huyu ni mmarekani na baadhi ya nyimbo zake ni Bang Bang Bang, For my lover, she got her ticket, give me one reason, revolution, mountain o thing
Chapman.jpgCarola-Kinasha2.jpg
 
Pia aina yao ya uimbaji unaweza kufananisha na kina hayati fela Anikulapo Kuti- Nigeria na Mzwakhe Mbuli- Afrika Kusini, Eric Wainaina- Kenya

Bahati mbaya sana, nyimbo za kina Maembe, Ashimba na kina Karola hazipigwi sana hapa nyumbani japo wanabaki kuwa wanamuziki wenye umaarufu nje ya Tanzania
 
Kama Irene Sanga ndio muandishi wa mashairi ya wimbo ule wa Mpoto uitwao MJOMBA basi mie nimemkubali; message ndani ya wimbo ule ni deep sana!!
 
Namkubali sana Carola Kinasha..uyu dada ni zaidi ya kina lady jd..kama unajua muziki lazma utanielewa....unajua hapa bongo kuna tatizo la media kutuchagulia wasanii wa kuwasikiliza,ivyo jamii inanyimwa fursa ya kusikia muziki wa kweli.
 
Kama Irene Sanga ndio muandishi wa mashairi ya wimbo ule wa Mpoto uitwao MJOMBA basi mie nimemkubali; message ndani ya wimbo ule ni deep sana!!

Mrisho mpoto hajawai kuandika nyimbo yoyote anayoghani,nyimbo zake zote anaandikiwa na mtu anaitwa Mgunga Mwamnyenyelwa(kasoro Mjomba na nikipata nauli) ye anachofanya ni kughani tu..inasikitisha sana hajawai kumpa credit uyu jamaa nakubaki kuchukua sifa zote adi za mtunzi.
 
Namkubali sana Carola Kinasha..uyu dada ni zaidi ya kina lady jd..kama unajua muziki lazma utanielewa....unajua hapa bongo kuna tatizo la media kutuchagulia wasanii wa kuwasikiliza,ivyo jamii inanyimwa fursa ya kusikia muziki wa kweli.

Naunga mkono hoja, media nyingi zimetawaliwa na watu wanaopenda midundo wakati wote na hii labda ni tatizo la kimfumo ambalo tumekuwa nalo, fikiria kwa mfano, mara ngapi umehudhuria mashindani ya mashairi/ghani hapa nchini (na wengi hatujui yanafanyikia wapi)

Tumefichwa na akili zetu zimefubazwa (arv) na nyimbo za malavidavi tena ambazo ni pipi-jojo, Natamani watu wa media wangekuwa wanatoa nafasi ya kucheza nyimbo hizi
 
Kama Irene Sanga ndio muandishi wa mashairi ya wimbo ule wa Mpoto uitwao MJOMBA basi mie nimemkubali; message ndani ya wimbo ule ni deep sana!!

Ni wanamuziki wachache sana hapa kwetu wanaosema ukweli hasa linapokuja suala la kutambua mtu aliyeandika mashairi (kuimba ni jambo moja), Mpoto hakuandika mashairi yale aliyoghani na sifa kubwa kabeba yeye.

Tujifunze kwa watu wa taarabu
 
Back
Top Bottom