Kidaya
Senior Member
- Dec 20, 2011
- 108
- 95
Kuni na mkaa ni vyanzo muhimu vya nishati kwa kupikia na kupasha joto, ambapo inakadiriwa kuwa 90% ya watanzania wanategemea kuni na mkaa kwa mahitaji ya nishati (HBS 2020 report). Pamoja na jitihada nyingi zinazofanywa na serikali, mashirika ya kitaifa na kimataifa ya kuhamasisha watu kutumia nishati mbadala kama gesi na umeme, watu wengi wanaendelea kutegemea kuni na mkaa kutokana na unafuu wa gharama na urahisi wa upatikanaji. Mbinu za kitamaduni za uzalishaji wa kuni na mkaa zinasababisha ukataji uliopitiliza wa miti, uharibifu wa mazingira na kuchochea mabadiliko ya tabianchi.
Vitalu vya kuvuna kuni na mkaa ni maeneo maalum ambapo uzalishaji wa kuni na mkaa unasimamiwa kwa kuhakikisha upandaji na ukuzaji wa miti, uendelevu wa misitu na udhibiti katika uvunaji wa miti. Kwa kipindi hiki cha mpito kuelekea matumizi ya nishati mbadala, vitalu vya kuvuna kuni na mkaa vitasaidia uzalishaji endelevu wa kuni na mkaa huku vikikuza uhifadhi wa mazingira kupitia taratibu za uvunaji zilizodhibitiwa na juhudi za upandaji miti. Vitalu hivi vitafanya kazi kama ilivyo kwa vitalu vya uwindaji wa wanyama pori, maeneo yenye vibali vya kuchimba mchanga n.k. ambapo kuna uratibu wa umiliki na uvunaji wa rasilimali hizi za asili kwa maendeleo endelevu.

Malengo ya vitalu vya uvunaji wa kuni na mkaa
Malengo makuu ya vitalu hivi ni:
• Kudhibiti ukataji miti: Kwa kuweka uzalishaji wa kuni na mkaa katika maeneo maalum, inakuwa rahisi kufuatilia na kudhibiti ukataji miti, kupunguza athari kwa misitu na kuzuia ukataji miti usiodhibitiwa.
• Kukuza mbinu endelevu: Kutekeleza mbinu bora katika uvunaji miti na uzalishaji wa kuni na mkaa, ikiwa ni pamoja na mizunguko ya uvunaji.
• Kuimarisha juhudi za upandaji miti: Kuhakikisha kuwa miti inapandwa tena katika maeneo yaliyovunwa ili kurejesha misitu na kudumisha usawa wa kiikolojia.

Faida za vitalu vya kuvuna kuni na mkaa
1. Kupunguza ukataji miti na uharibifu wa misitu
Vitalu vya kuvuna kuni na mkaa vinapunguza tatizo la ukataji miti kiholela kwa;
• Kudhibiti uvunaji wa miti: Vitalu vitakuwa na utaratibu aina fulani ya miti, miti yenye ukubwa na unene fulani ndio ivunwe kulingana na mpango wa usimamizi unaozingatia athari za kiikolojia na kuhakikisha uendelevu. Mbinu hii inayodhibitiwa inapunguza athari mbaya kwenye ya misitu.
• Kuwa na mbinu endelevu za uvunaji miti: Kutekeleza mbinu bora katika uvunaji miti na uzalishaji wa kuni na mkaa kama vile kuvuna baadhi ya matawi ili kuruhusu miti kuchipua badala ya kukata mti wote na matumizi ya tanuru bora za uchomaji mkaa zinazozuia moto na moshi kusambaa na kuathiri miti mingine kwenye msitu.

• Kuhifadhi viumbe hai: Kwa kuzuia ukataji miti kiholela, vitalu vitasaidia kuhifadhi makazi ya aina mbalimbali za mimea na wanyama ili kudumisha mfumo ikolojia.
2. Kuboresha udongo na uhifadhi wa maji
Vitalu vya kuvuna kuni na mkaa vinachangia uhifadhi bora wa udongo na maji kwa:
• Kupunguza mmomonyoko wa udongo: Kudumisha kifuniko cha misitu husaidia kulinda udongo dhidi ya mmomonyoko unaosababishwa na upepo na maji. Mizizi ya miti na mimea mingine inaimarisha udongo, kupunguza hatari ya maporomoko ya ardhi na uchafuzi wa maji.
• Kuongeza utunzaji wa vyanzo vya maji: Misitu ina jukumu muhimu katika mzunguko wa maji kwa kuvuta mvua na vyanzo vya maji visikauke. Kuwa na vitalu vya uvunaji kuni na mkaa kutasaidia kuepuka ukataji wa miti kupita kiasi na karibu na vyanzo vya maji hivyo kuhakikisha mtiririko wa maji kwenye wa mito na vijito.
3. Kupunguza mabadiliko ya tabianchi
Vitalu vya kuvuna kuni na mkaa vinaunga mkono juhudi za kupunguza mabadiliko ya tabianchi kwa:
• Kuongeza uzalishaji wa oksijeni: Kupitia mipango ya upandaji miti na urejeshaji wa misitu upya, vitalu vitaongeza idadi ya mti katika misitu, hivyo kupunguza kiwango kikubwa cha kabonidayoksaidi kitatumiwa na miti hali itayoplekea kuongezeka kwa uzalishaji wa oksijeni.
• Kupunguza uzalishaji wa kaboni: Mbinu bora za uzalishaji wa mkaa ndani ya vitalu hivi, kama vile tanuru bora, hutoa moshi na gesi chache za chafu ikilinganishwa na mbinu za kitamaduni. Hii inapunguza alama ya kaboni ya uzalishaji wa mkaa.
4. Ushirikishwaji wa Jamii na Uwezeshaji
Kuhusisha jamii za ndani katika usimamizi wa vitalu vya kuvuna mkaa kunakuza hisia za umiliki na uwajibikaji tofauti na sasa ambapo wana jamii hawachukui hatua wanapoona mtu anakata miti kwenye misitu. Ushirikishwaji huu ni pamoja na;
• Usimamizi shirikishi: Kuwashirikisha jamii katika michakato ya maamuzi inayohusiana na uanzishaji na usimamizi wa vitalu.
• Kujengea uwezo: Kutoa mafunzo na rasilimali za kuboresha ujuzi katika mbinu za kuandaa miche, kukuza miti, kuendelevu za misitu na uzalishaji wa mkaa.
• Kuimarisha juhudi za upandaji miti: Kuhakikisha kuwa wenye vitalu vya kuvuna kuni na mkaa wana wajibika moja kwa moja kupanda na kukuza miti katika vitalu vyao ili kudumisha usawa wa kiikolojia na hali ya misitu.
5. Upatikanaji wa nishati endelevu: Vitalu vitasaidia kukidhi mahitaji ya nishati ya kuni na mkaa kwa njia rafiki kwa mazingira na uchumi.
6. Faida za kijamii na kiuchumi: Uanzishaji na matengenezo ya vitalu utatoa fursa za ajira na kujipatia kipato kwa shughuli za upandaji miti, ukuzaji, uvunaji, na uzalishaji wa kuni na mkaa.

Maboresho katika utekelezaji wa mradi
Ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huu kwa mafanikio, tunahitaji kuboresha maeneo yafuatayo;
• Umiliki wa ardhi na utawala: Kuanzisha mifumo wazi ya kisheria na sera zinazotambua na kulinda haki za jamii na wadau wanaohusika katika uanzishaji na umiliki wa vitalu vya kuvuna kuni na mkaa.
• Uwekezaji wa awali na ufadhili: Kanzisha na kudumisha vitalu vya kuvuna mkaa kunahitaji uwekezaji mkubwa wa awali wa eneo na miche ya miti. Jamii na wadau wakaoonesha nia ya kushiriki mradi huu wasaidiwe kupata eneo na miche ya kuanzia.
• Ufuatiliaji na utekelezaji: Kuwa na mifumo madhubuti ya ufuatiliaji na utekelezaji, ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia kama picha za satelaiti na drones katika kulinda uvunaji miti haramu na kupita kiasi.
• Elimu na Uhamasishaji: Kufanya kampeni za elimu na uhamasishaji ili kukuza uelewa wa jamii kuhusu faida za vitalu vya kuvuna kuni na mkaa na mbinu endelevu.
Vitalu vya kuvuna mkaa vitasawazisha mahitaji ya kuni na mkaa na uhifadhi wa mazingira nchini. Kwa kudhibiti uvunaji miti, kukuza upandaji miti upya, na kutekeleza mbinu bora za uzalishaji, vitalu hivi vinaweza kupunguza ukataji miti, kuimarisha uhifadhi wa misitu.

Upvote
23