Vitambulisho vya NIDA tumepigwa😀😀

Vitambulisho vya NIDA tumepigwa😀😀

RoadLofa

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
1,509
Reaction score
3,313
Ukichunguza vitambulisho vya NIDA vingi vina makosa kwenye vipengele mbalimbali, unaweza kuwa ni ile card inataarifa vizuri kabisa inayoonyesha taarifa zako kama kwenye birth certificate vizuri kabisa ila ile namba ikiingizwa kwenye system inayosoma card yako ikaleta details tofauti kabisa kama jinsia, mwaka wa kuzaliwa na taarifa nyingine

Kwa kifupi wakati wa uandikishaji zile forms tulizokuwa tunajaza nyingi zilikuwa zinapotea au kuchanganywa yaani unakuta form ya katikati imechomoka ila mtu aliyeajiriwa kufanya kazi ya data inputs hajiangaishi anaforge taarifa au anajaza gap kwa taarifa za mtu mwingine.

Ili swala makampuni ya simu yanalifahamu ila hawawezi kusema maana wao wanajali kuingiza pesa kusajili watu kwenye biashara zao

Na ilikuwaje zoezi alikuwa na awamu ya marekebisho,? Inamaana lilifanyika kikamilifu 100%

Ndo maana bank zinazojielewa hawataki kitambulisho cha NIDA pekee kufungua account maana wanajua ivyo vitambulisho vingi vimekosewa taarifa zake

Ombi langu kwa serikali ni kuanzisha zoezi la kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye vitambulisho vya utaifa maana kuna watu wameandikiwa Female badala ya male pia majina yamekosewa baadhi , ilo ni tatizo
 
Mimi namba ya NIDA nikiingiza kwenye hili zoezi la kurasimisha namba za ziada za simu naambiwa "NAMBA YA KITAMBULISHO ULIYOINGIZA IMEKOSEWA"
 
Ni kweli tena ni kweli kabisa, taarifa nyingi zilizopo katika mtandao wao si taarifa sahihi za mhusika.

Serikali iwe ina outsource huduma hasa hizi zinazohusiana na data kwenye makampuni ya Research (data). Nina uhakika 100% anuani za makazi napo kutakuwa na chaos kubwa sana.
 
Tunasubiri bajeti tuanze zoezi upya, kuweni na subira
 
Ni gharama kiasi gani ukitaka kurekebisha hizo kasoro?,changu pia kimekosewa.
 
Wanaleta vya kidigital zaidi,, wanasubiri Fungu litolewe ili wajipigie mikwanja.
 
maendeleo hayana chama

ni jambo la kawaida kuboronga nchini kwetu
 
Kama kuna zoezi limefail na ni la ovyo ni hili. Kwanza wakikuoa namba now kitambulisho kukipata hata hujui ni lini
 
Kwani vitambulisho vilishatoka ?
Mbona mie nimejiandikisha miaka minne iliyopita mpaka leo naambiwa hakijatoka nimebaki na namba tu
 
Kama kuna zoezi limefail na ni la ovyo ni hili. Kwanza wakikuoa namba now kitambulisho kukipata hata hujui ni lini
Kuna jamaa angu ana download vitambulisho unakuwa na kopy kwa 10000 nichek 0715058481
 
Kwani vitambulisho vilishatoka ?
Mbona mie nimejiandikisha miaka minne iliyopita mpaka leo naambiwa hakijatoka nimebaki na namba tu
Kuna jamaa angu ana download vitambulisho vya nida kwa 10000 tu 0715058481
 
Mimi nachozingatia ni namba tu! Bahati nzuri kwenye miamala mambo ni mazuri.
 
Back
Top Bottom