robbyr
Senior Member
- Apr 8, 2017
- 129
- 221
Kama mtanzania naandika hili machozi yakimwagika. Naumia kwa namna pesa nyingi za watanzania zilivyoteketea kwa kisingizio cha vitambulisho.
Kipindi cha Kikwete pesa zililiwa hadharani. Kipindi cha Magufuli Simba Chawane akasema inakuja mashine kubwa na tatizo litaisha.
Yawezekana limeisha kwa kuweka pesa mfukoni kwani nimepata kitambulisho changu juzi. Maskini wangu wino unafutika. Hivyo havina ubora. Je, nani anahujumu serikali.
Utaratibu wa kutoa umekuwa mbovu, baada ya kulundika vitambulisho basi wameamua kutoa vitambulisho ambavyo vimeenda kujazwa kwenye vijiji na vituo mbalimbali huku kila mtanzania akihaha kupata. Je, kama taifa tumefanikiwa nini?
Jamani hata kutoa vitambulisho vya NIDA tu😭
Sasa hivi hata ukipeleka ombi la kupata kitambulisho au kurekebisha walioachwa kwenye vituo vanataka pesa koz hakuna usimamizi unaoeleweka.
Mheshimiwa Rais naomba utoe tamko na kama kuna uzembe basi watu wawajibike kama nchi nyingine tuache tabia ya kulindana hatutafika.