Vitambulisho vya Taifa Vs Sensa ya Makazi

mbeshere

Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
64
Reaction score
8
Wanajamvi hivi kwanini tupange foleni ya kuandikisha vitambulisho wakati watu wa sensa watapita kila nyumba kumuhesabu mtu na kuchukua baadhi ya maelezo kwanini form hizo zisiwe ndio za NIDA. badala ya kutumia fedha kibao kwa kazi mara mbili au hao NIDA wahesabu na watu moja kwa moja?

nawakilisha
 

Watakaogoma si watakosa vitambulisho??

 
Watakaogoma si watakosa vitambulisho??

Tayari complication zishaanza hapo, vinginevyo lilikuwa wazo zuri sana! Ila hizi ni dili za watu ukiwaambia hivyo hawatakusikiliza wala kukuelewa, kwa hiyo ni kama unapigia mbuzi gitaa!
 

Wewe unataka kuwanyang'anya watu mlo wao. Angalia wasije wakakumabwepande.
 
Hapo ndiyo mtakumbuka nilishawahi toa maoni humu nikaambulia matusi. Tukitaka kitu kizuri chenye tija na tunachoweza kubana matumizi ipasavyo ni lazima tukubali kufunga mipaka hasa kwa mahitaji nyeti na kutumia fedha zetu za ndani katika mambo nyeti. Fedha za senza zingeongezwa kidogo zingetosha kufanya shughuli za sensa na vitambulisho vya taifa. Hapa lazima tujue anayetoa fedha za vitambulisho ni mingine na anayetoa za sensa ni mwingine. Hivyo hamna wa kumlaumu ila sisi wenyewe kwa kutokuwa na vipaumbele.
 
Hivi hujajua hii mnayoita sijui sensa, vitambulisho vya taifa, katiba mpya unajua mwisho wake itazaa nini???? Epa iliyotukuka!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…