Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Leo nimepata habari kwamba vitambulisho vya Uraia ndivyo vitatumika kupigia kura mwaka 2020 na vitambulisho vya kupigia kura vya sasa havitatumika. Hata sasa taasisi mbali mbali zimeanza kutumia vitambulisho vya Uraia kama ni vitambulisho rasmi badala ya vile vya kupigia Kura.
Kutokana pia na kukosewa kwa picha kwenye vitambulisho hivyo, imeamriwa kwamba Namba za vitambulisho hivyo zitolewe kwa wahusika wakati tatizo la kuweka picha kwa usahihi likirekebishwa.
Hii maana yake ni kwamba Jina la Juma Omary litarudi kwa mfano na namba ya kitambulisho chake bila ya picha yake. Kwa maana nyingine itatakiwa mtu kukariri namba yake bila ya kuwa na kitambulisho kwa kuwa picha nyingi haziko kwenye majina ya wenye vitambulisho.
Kama ni kweli na hizo picha hazitarekebishwa mpaka mwaka 2020, na kwa kuwa inaonekana hakuna mpango wa kuboresha daftari la wapiga kura, basi kuna uwezekano mkubwa sana mwaka 2020 tukapiga kura bila ya kuwa na vitambulisho na wala kuwa na picha za wapiga kura.
Hii habari kama ni kweli basi wapinzani wanatayarishiwa bao la mkono na safari hii itakuwa ni tatu bila!