Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

asante nimekuelewa vizuri sana
 
swali jingine nisaidie kuelewa ikiwa biashara yangu ikashindwa kufanikiwa tofauti na nilivyotarajia, biashara ikafa hapo inakuaje wataendelea kunidai au utaratibu utakuwaje?
 

nyie mkikimbiwa je?
 
kikao ni lini na wapi nije na elf 10 yangu pia kujifunza
 
swali jingine nisaidie kuelewa ikiwa biashara yangu ikashindwa kufanikiwa tofauti na nilivyotarajia, biashara ikafa hapo inakuaje wataendelea kunidai au utaratibu utakuwaje?

Kuna mambo kadhaa yanafanyika, kwa nia njema kabisa, kabla hujakopeshwa. Kutakuwa kuna jopo (kamati) watakaopitia ombi lako na kujiridhisha kuwa vigezo vya wewe na ushirika kufanya vizuri vimekidhi ukopeshwe na ushirika uwe mbia wako.

Kuna vigezo vya taaluma za ujasiriamali, je vinakidhi? Kama havikidhi na biashara inaonesha ni ya kuleta faida basi utaongezewa ujuzi kwa kupewa mafunzo (crush courses au seminars husika), kwa ufupi kuna vigezo kadhaa inabidi viwe vinakidhi ili ujipatiue mkopo na ushirika wawe wabia wako. Yote ni kuhakikisha unajikomboa na unapata mafanikio na ushirika wanapata mafanikio.

Biashara yako ikifa na ushirika umeingia ubia na wewe ina maana na ushirika umekula hasara pia, kitu ambacho ushirika itajitahidi kufanya isitokee na bahati mbaya ikitokea, tunaongelea kuwa na mifumo ya kulinda miradi mfano, investment insurance.

Napenda uelewe kuwa kila mkopo utaotolewa nao pia ni mradi wa ushirika mpaka deni litakapomalizwa.
 
sasa faida mnaipataje kama hakuna riba?

Tunakua wabia wa mradi wako unaouchukulia mkopo.

Napenda ufahamu kuwa faida inatakiwa kwanza upate wewe na washirika wenzako waliowekeza kwenye saccos ambao ni wote tuliojiunga. Lengo si wakopeshaji kupata faida kwa kukauana mpaka damu kwa njia za riba, lengo ni wabia kujikwamua kiuchumi.

It's a non-interest bearing loan. You don't have to pay the interest so that you don't worry about money growing in your hand. It won't grow, so take your time. Only thing is, if you pay us back fully you get more money. - Mohamed Yunus, father of microcredit and Nobel Peace Prize Winner
 
kikao ni lini na wapi nitakuja na elfu kumi yangu


Kikao cha awali kimeshafanyika tarehe 1-5-2017 na maazimio yaliopitishwa ni pamoja na kuanzishwa ushirika kwa haraka sana, na harakati za kuanzisha ushirika zimeshaanza. Kikao kijacho tutawatangazia hapa hapa JF na kama utakuwa umeshajiunga kwa kulipia kiingilio ha 10,000 basi utajulishwa pia kwa whatsapp na email.
 
Nami naitaji kitafanyikia wapi nije my wasapu 0713329624

Kikao cha awali kimeshafanyika tarehe 1-5-2017, Pwani, Kibaha , Misugusugu, mtaa wa vitendo na maazimio yaliopitishwa ni pamoja na kuanzishwa ushirika kwa haraka sana, na harakati za kuanzisha ushirika zimeshaanza. Kikao kijacho tutawatangazia hapa hapa JF na kama utakuwa umeshajiunga kwa kulipia kiingilio ha 10,000 basi utajulishwa pia kwa whatsapp na email.
 
ok ukitutangazia nitakuja mamy
 
kwaio unataka kuniambia incase biashara ikafa, investment insurance itacover hio effect au bado sijaelewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…