Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

Mna


Mna nia nzuri ila mmeanza vibaya.SACCOS ni jina linalopatikana baada ya kuandikishwa kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya 2013.Pili hakuna cheo cha katibu wa Vyama vya Ushirika kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Ushirika.

Tatizo kubwa japo limesambaa si kwenu tu na wasimamizi wameruhusu kosa hili liedelee bila kuchukua hatua ni kitendo cha kuruhusu baadhi ya Vyama vya Ushirika kuanzishwa kwa misingi ya dini,madhehebu,Vyama vya siasa au makabila.

Mojawapo kati ya kanuni kuu za Vyama vya Ushirika Duniani ni uanachama wa wazi na wa hiari.Kuwa na vyama vinavyozingatia,dini,dhehebu,kabila au chama cha siasa ni kukiuka kanuni hii.

Ninawashauri kuwa wasilianeni na Afisa Ushirika wa Wilaya yako atakupa maelekezo sahihi ya uanzishaji wa SACCOS.

Kila la kheri.
 

Nimefurahi sana kwa maoni yako, naamini "criticism" yako ni kwa kututakia mema.

1) Hatuwezi "kuandikishwa kwa mujibu wa sheria..." kama hatuna jina na na hilo ndio jina letu tulilojichagulia "Vitendo SACCOS".

2) Hilo la vyama vya ushirika kuwa vya "dini" hatutakuwa nalo kwetu. Bali tutafata misingi ya undeshaji biashara na kukopeshana bila kutoa riba kwa mujibu wa Islamic Finance and Banking sharia. Mfumo ambao kwa sasa unakubalika duniani kote na unafanya vizuri sana hata katika nchi kubwa za Kimagharibi na ni vyema sana kuwa hata hapa kwetu upo na unatumika rasmi sasa hivi.

3) Asante kwa ushauri wa kuwasiliana na "Afisa Ushirika wa Wilaya", mwana JF CHIKIRA MTABARI hapo juu kidogo kwenye post namba 151 katushauri vivyo hivyo na zaidi kidogo, tumekubaliana na ushauri wake na huu wako kwa 100%. Tutafanya hivyo.

Tunakukaribisha sana ujiunge nasi kwa faida ya wengi, tunapenda vichwa vinavyochangamsha na si vile vya "Yes Sir" pekee.
 
Thread subscribed


Jiunge na saccos yetu mpya utakutana huko kwenye whatsapp group yetu vichwa tofauti vina chemsha bongo zao kufanikisha mambo haya mazuri.

Whatsapp 0625249605

Karibu sana.
 
Nafikiri una changamoto ya kujua taratibu za utoaji wa mikopo. Nakuahairi tembelea ofisi za saccos wakupe maelekezo ya namna ya utoaji mikopo usikurupuke. Tena mbali zaidi hata maana yenyewe ya neno saccos hujui
 
Nafikiri una changamoto ya kujua taratibu za utoaji wa mikopo. Nakuahairi tembelea ofisi za saccos wakupe maelekezo ya namna ya utoaji mikopo usikurupuke. Tena mbali zaidi hata maana yenyewe ya neno saccos hujui

Tungefurahi sana ungejiunga nasi ili utuelimishe, tunahitaji sana watu kama wewe wenye uelewa wa kuelewa kuwa sisi hatuijui "maana yenyewe ya neno saccos". Ninakuhakikishia, sisi hatujui kweli na tungependa uje kutuelewesha kwenye ushirika wetu, tupo tayari kulipia mafunzo yako utakayotupa, mradi uhakikishe una course materials zinazoeleweka.

Karibu sana.

Whatsapp 0625249605
 

Mnanifurahisha sana mnavyojibu professionally. Lazima aingie mitini.
 
Nimesoma maelezo yenu kwa kina nimeshawishika. Hata kama mimi sitanufaika lakini naamini kuna mtanzania mwenzangu atanufaika kwa mimi kujiunga kwenye hii SACCOS, count me inn. Ungetupa uratibu kwa walio nje na Tanzania wanajiungaje? Asante.
 
Nimesoma maelezo yenu kwa kina nimeshawishika. Hata kama mimi sitanufaika lakini naamini kuna mtanzania mwenzangu atanufaika kwa mimi kujiunga kwenye hii SACCOS, count me inn. Ungetupa uratibu kwa walio nje na Tanzania wanajiungaje? Asante.


Nimeona watu wawili kutoka nje wametumia Money Transfer - Send Money Online | WorldRemit na zimefika.

Unatuma 10,000 kwa namba +255756803528 Jina litatoka Mohamed Abdallah.

Nakushukuru sana kwa wazo lako jema, ninauhakika hata wewe utafaidika sana. Kwa kuwa upo China kuna vitu vingi tumeanza kuulizia kutoka huko, kwa uenyeji wako unaweza ukawa ndio macho ya SACCOS yetu mpya huko. Tukishakuunga nitakupa majina ya vitu ambavyo SACCOS inaviulizia huko.
 
Huu mfumo nausoma tuu kwenye matangazo siufahamu .....ningependa kushiriki kujifunza.


Sasa tumeanza rasmi kujiunga na kuunda ushirika wetu utaofata mfumo wa Islamic Finance.

Karibu ujiunge nasi kuunda ushirika wa kipekee Tanzania.
 
okay. Ngoja niangalie uwezekano wa kutuma kwa hiyo service sijawahi kuitumia kabda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…