Visenti
JF-Expert Member
- Jul 24, 2008
- 1,025
- 329
Kuna ofisa mmoja ni kiranja katika idara ya serikali, kwa nia nzuri na uzalendo ofisa huyo alimlima karipio kali kulingana na kanuni mmoja wa watumishi kwa utovu wa nidhamu, kumbe huyo jamaa ni ndugu wa mh. waziri wa wizara husika, akaenda kumweleza nduguye (mh. waziri), mh huyo akamtwangia simu kiranja papo kwa papo na kutoa vitisho vikali, siku mbili baadaye yule kijana akarudi ofisini kwa kiranja na kumkabidhi barua iliyosainiwa na mh.waziri ikimpa maelekezo kiranja ku-withdraw hilo karipio na kumsafisha kijana. kiranja akasalimu amri na kuwa mpoleee. sasa wana JF kinachofuata hapo ni uwezekano wa kiranja huyo kuchakachuliwa/kuwa victimized, je afanyeje ili kujihami kama atadhuriwa hapo baadaye? maana hawa waheshimiwa wana nguvu za kufanya lolote.