TulaSawyer
Member
- Jun 11, 2017
- 20
- 41
Habari wanajukwaa!!
Kero yangu ni jinsi mazingira ya vitongoji vinavyokizunguka chuo kikuu cha Mzumbe vilivyo vichafu, inakera kweli, unabaki kujiuliza ustaarabu wa mtanzania uko wapi?! Au hadi aje mtu mweupe (kwa hisani, ndipo mazingira yawe masafi)?.
Kwanza ungedhani Ile kukaa karibu na chuo kikuu maisha yangekuwa na ustaarabu kidogo, huku ni kinyume kabisa. Kwanza biashara holela ni nyingi mnooo, taka zinatupwa popote, makazi mengi yamejengwa holela ( huu ni utamaduni sehemu nyingi za Tanzania, ni maada pana haswaaa).
Hakuna mtaa utapita na ukaona ni kusafi. Mbaya zaidi hii ni wilaya ya Mvomero, kwahiyo hata gari za taka zinazoonekana manispaa ya Morogoro hazifiki huku. Pia sifahamu utaratibu wa ukusanyaji taka kwa wilaya ya Mvomero upoje.
Watoto wetu wanacheza mazingira machafu, jamani inatia kinyaa. Mtu mweusi ni kama amerogwa!!! Kipindi cha mvua Sasa Kuna mitaa huwezi hata kuingia.
Wananchi, hili tunaweza wenyewe, siyo lazima muda wote hadi tuletewe misaada. Ule utaratibu ulioanzishwa na hayati Rais Magufuli kwakweli urudishwe, usafi ni tabia, siyo kitu Cha kujifunza siku Moja. Tuone Kuna haja ya kurithisha vizazi vyetu mazingira masafi.
Inatia aibu kuamini watu waliosoma wanaishi mazingira machafu hivi, elimu yetu haitukomboi kwa chochote. Watoto wanakuwa wanaona uchafu kila siku na Sasa wanajengeka hivyo, na wanakuwa wanaamini hayo ndiyo mazingira sawa kabisa kuishi. Hii haijakaa sawa!!
Asanteni.