Vitu 5 vinavyofanya muonekano wako uonekane cheap

Vitu 5 vinavyofanya muonekano wako uonekane cheap

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Unaweza kuvaa vitu expensive au hata vya bei rahisi ukapendeza, lakini kuna vitu ambavyo ukivivaa au ukavifanya hata kama ukiwa umevaa vazi la mamilioni bado unaonekana cheap. Yes na wengi wetu huwa tunajisahau na kufanya haya makosa.

Nywele mbaya
Nywele zinaweza kufanya muonekano wako kutoka kwenye 100 kurudi kwenye 30, ni moja kati ya essentials ambazo unatakiwa kuziwekea umakini sana. Kama ni mpenzi wa nywele za bandia basi hakikisha unanunua zenye quality nzuri, ambazo unaweza kuzisafisha na ku-style mara nyingi uwezavyo kama ni mpenzi wa nywele zako mwenyewe basi jaribu kuwa unaziosha mara kwa mara unasuka na kuzi-style vyema.

Kuvaa rubber band mkononi
Kuna rubber band na culture hizi huwa zinashusha sana muonekano, kwenye rubber band kama umezitoa kwenye nywele hakikisha unaweka kwenye handbag usivae mkononi na swala la culture tunadhani unaweza kuvaa a good bracelet ukapendeza.

Manukato
Kuna kunukia kupitiliza huku kunaweza kuharibu muonekano wako, lakini pia kuna kunukia vibaya napo panaharibu muonekano. Hakikisha unaoga vyema, kuwa na perfume yako ambayo inakufanya unukie kama rich au expensive person that you are. Kumbuka kuvaa nguo za ndani ambazo ni safi pia.

Rangi za kucha zilizo banduka
Unapaka rangi inaanza kubanduka bado unaendelea kukaa nayo, hata uvae nguo za mamilioni kama una chipped nails zinaharibu kabisa muonekano, hakikisha kama rangi ya kucha imeanza kutoka unaitoa yote na kupaka nyingine au kuwa na natural nails zako ambazo umezisafisha vyema

Viatu
Invest in shoes, we repeat invest in shoes yaani kiatu ni number moja kwenye swala zima la kuharibu muonekano, unaweza kuvaa simple outfit ukavaa na kiatu kizuri kikabeba muonekano mzima na unaweza kuvaa outfit nzuri ukavaa na kiatu kibaya kikashusha muonekano from 100 to 0. Nunua viatu vyenye quality, rangi na design nzuri.
 
Mimi nazipenda nywele zangu sana na zinanivutia ninapozitunza na kuweka katika hali ya usafi na kuvutia.

Nikiziona hazijakaa poa , sijaweka Ktk hali nzuri , nyingi sana au mafuta yake yameniishia huwa napiga cap 🧢 na vilemba mwanzo mwisho.
 
Hapo kwenye rangi za kucha unahamasisha wake wetu waendelee kuita vijana wapaka rangi nyumbani na kuwapanulia mapaja.
Mbona kama umemuwekea maneno mdomoni? Mimi nafikiri bora kutokuwa na rangi kabisa kuliko kuwa na rangi zilizobanduka. Ikumbukwe kuwa hajasema kutokua na rangi kwenye kucha kunaharibu muonekano. Ni vyema kusoma/ kusikiliza ili kuelewa kuliko kufanya hivyo ili kujibu.
 
Ahsante kwa miongozo, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
[emoji1428] BUGGY CLOTHES.
[emoji1428] SANDALS
[emoji1428] SCREAMING BELTS
[emoji1428] FAKE BRANDS
[emoji1428]...
 
Usisahau na rangi nzuri za nguo, zisiwe rangi za kung'aa sana sijui yellow aah, na zisiwe pana sana, among my favourite colors😘, mtu akivaa rangi hii aisee namuona classic sana
 

Attachments

  • 20220722_220030.jpg
    20220722_220030.jpg
    103.8 KB · Views: 74
Back
Top Bottom