Vitu gani huzingatia unapoingia dukani kununua jeans?

Vitu gani huzingatia unapoingia dukani kununua jeans?

bbwaoy

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2015
Posts
466
Reaction score
468
Unapoingia dukani , kabla hujafungua mkoba, wallet au kunyofoa hela mfukoni kununua jeans, ni vitu gani huwa unavizingatia sana kabla hujasema "yeah, hii jeans kweli kali muhudumu nipe hii"?

Mimi huwa nazingatia vifuatavyo:

1. Size , jeans initoshe kabisa 32 kiuno bila kupwaya.

2. Rangi, niko makini sana na rangi ajabu, napenda nivae jeans ambayo sio ya mng'ao halafu iwe na rangi ya kukaa muda mrefu.

3. Mifuko ya jeans, hasa mifuko ya nyuma na mbele napenda sana mifuko simple na mirefu kiasi kwamba hata wallet ina zama ndani au simu.

4. Mwisho kabisa huwa ni Brand. I don't care kama ni Gucci, Zara, Fear of God, Vans, Diesel, yeezy, so long as vi 3 twaja hapo juu vimetimia hela yangu inatoka bila kinyongo.
 
Back
Top Bottom