Black Opal
JF-Expert Member
- Jan 22, 2023
- 233
- 298
Wakuu kwema?
Kuna mambo mengi tufanaya kwa ajili ya wengine huku mara nyingi tukijisahau sisi wenyewe.
Inaweza kuwa unafanya kwa kupenda na wakati mwingine ni kwa kujilazimisha kwakuwa hatutaki kuwakwaza wapendwa wetu, au kuwafurahisha watu wengine, na mara nyingine ni katika kutekeleza tu majukumu yetu ambapo ingekuwa mtu mwingine ungemwambia apumzike na ajijali zaidi, ila ikiwa upande wako unajisahau kujijali kabisa.
Ungekuwa unajionesha upendo na kujijali, kujifurahisha, kujionea huruma ungefanya hayo yote unayofanya? Kipi ungeacha? Kwanini hufanyi hivyo sasa?