vitu kutembeatembea mwilini ni ugonjwa gani?

Mwana wa Mungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2008
Posts
1,003
Reaction score
85
Halooo, nadhani humu kuna madaktari wengi wazuri. kuna rafiki yangu mmoja, nilimshauri aende hospital, kwasababu anasema, analo tatizo, anaona vitu kama vinatembeatembea mwilini mwake. inavyoonesha, anasema ni kama kitu kama hewa inatembea kwa kutikisatikisa kwenye misuli yake, kama mdudu mkubwa kiasi cha kidole hivi, unaweza kuona kinavyotikisika. nilimwona pia aliponionyesha, kwani utaona mara inatikisika mkononi kwa muda, mara inatikisika mgongoni mara kifuani nk.

It was a little bit funy kwasababu mpaka niliogopa, na mwingine angedhani jamaa amelogwa nk. mimi nilidhani ni mapepo yamemwingia huyo jamaa kwasababu mimi ni mwana wa Mungu you know..hahaha.

nilikuja kufikiri au ni misuli inashitukashituka kwasababu ilishashituliwa labda kwa kupiga chafya au kwa namna yoyote ile. kuna mtu alishawahi kutokewa na ishi kama hiyo? ninini hiyo? how can we help this guy? kama ni mapepo ningefahamu ili nimwambie aende akaombewe tu atapona, manake hata hospital hayatamwondoka.

Please, kama kuna mtu anaefahamu hii naomba comment zenu. God bless you.
 
ukiachilia mbali hiyo hali ya misuli kustuka stuka na vitu kumtembea je jamaa anajisikiaje?
anajihisi kuumwa au?
hiyo hali ilianza lini?
je huyo jamaa ni mfuasi wa dini ?
 
Mwana wa Mungu,
Huyo rafiki yako alipokushirikisha hilo tatizo ulipaswa kumuombea na baadae umshauri zaidi (kwenda hospitali) sasa wewe unamwacha hivi hivi,ujue shetani anachekelea hivyo.

Wataalamu tumsaidie ndugu yetu kama kawaida yetu.
 
hahaha, jamani, hakuna mtu ambaye alishawai kutokewa na kitu kama hicho? hahaha, mbona mnasema aende angaza, hivi virusi navyo huwa vinatembea...mnanifanya nicheke sana.
 
Rafiki yako anaweza kuwa anasumbuliwa na kitu kinachoitwa fasciculations. Kama inavyoelezwa kwenye article hii:


Wikipedia imetoa definition rahisi ya fasciculations kama ifuatavyo:


Hope nimesaidia somehow....
 
Umetusaidia wengi sana kwa jibu lako mkuu.Nakupa tano.
 
aisee asante kwa jibu zuri. Nitafikisha ujumbe, God bless you.
 
aisee asante kwa jibu zuri. Nitafikisha ujumbe, God bless you.

naomba ufikishe na ujumbe huu kwa mgonjwa, muambie asali sana na amwombe Mwenyezi Mungu sana ili amuondolee shari/mkasa uliomkumba, ukweli ni kwamba mapepo yapo na yanavamia watu na kuwasumbua sana watu, mwambie ajitahidi kuishi maisha ya usafi, vitu kama zinaa, ulevi, dhulma na mambo machafumachafu huvutia sana mapepo kuwakumba watu, ni kwa msaada wa Mwenyezi Mungu tu ndo yanaweza kuondoka kikamilifu. akiwa na Imani kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu na akaombana kusali na kutenda yanayompendeza Mwenyezi Mungu, bila shaka atapona tu. usiache kufikisha na ujumbe huu tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…