koba lee
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 981
- 1,606
Wasalaam.
Leo mimi na wewe nataka tuanze kujivunia kuzaliwa katika kizazi hiki, nikimaanisha wale amabao tume/wamezaliwa kuanzia miaka ya 1900 – 2000. Kwanini nasema hivi, nasema hivi sababu kuna mambo tumeyashuhudia katika kipindi chetu au hata kama sio kushuhudia basi tumehadithiwa na watu ambao wameshuhudia au kua moja wapo ya matukio/tukio husika. Tofauti kati ya kizazi hiki cha kwetu na vizazi vijavyo ni kwamba sisi tumeshudia lakini vizazi vijavyo vitakua vinasoma katika maandiko ya kihistoria na mashuleni.
Hapa chini ntaorodhesha baadhi ya vitu ambavyo mimi binafsi naviona ni vitu vya kujivunia kua mmojawapo wa mashuhuda wa baadhi ya hivyo vitu.
Naomba uongezee lako ambalo unajivunia kua shuhuda katika kizazi hiki au unahisi nimesahau kuliorodhesha hapo juu.
Asanteni.

- VITA YA PILI YA DUNIA:- Ndio ni vita ya pili ya Dunia, kuna wazee wetu hapa nyumbani waliopigana vita hii katika jeshi la waingereza.Wapo walioishi mpaka miaka ya 2000 mwanzoni kwahiyo kizazi chetu kimeweza kupata historia ya uhakika kutoka kwa wazee wetu hao.
- BABA WA TAIFA (J.K. NYERERE 1921 - 1999):- Nadhani hapa sina haja ya kuelezea chochote.
- UHURU WA TANGANYIKA ( 1961).
- KUFUNGA KARNE (1900-2000)
- KUFUNGA MILENIA (1000-2000):- Hapa ili kufunga milenia nyingine inabidi ipite miaka elfu moja mingine nikimaanisha mpaka mwaka 3000. Sasa hapa kati unadhani ni vizazi vingapi vitakua vimepita.
- UVUMBUZI WA SIMU ZA MKONONI
- SAFARI ZA WANA ANGA KWENDA ANGA ZA MBALI
- RAIS WA KWANZA MWEUSI MAREKANI (OBAMA)
- RAIS WA KWANZA MWANAMKE TANZANIA (MAMA SAMIA)
- UJENZI WA DARAJA LA JUU LA KWANZA TANZANIA (MFUGALE FLYOVER)
- UJENZI WA RELI YA KISASA YA KWANZA TANZANIA (SGR)
- UJENZI WA BWAWA KUBWA LA KUFUA UMEME TANZANIA (JNHPP)
Naomba uongezee lako ambalo unajivunia kua shuhuda katika kizazi hiki au unahisi nimesahau kuliorodhesha hapo juu.
Asanteni.