Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
Wakuu habari.
Wengi wetu tunanunua magari used kutoka nje. Hayo magari yanakuja yametembea vya kutosha tu. Mengie hadi kilometa 60,000 hadi 150,000. Ila cha kushangaza ukiyaona bado mapyaa kwa nje.
Likija hapa kwetu, baada ya kilometres 50,000 au baada ya mwaka mmoja, halitazamiki.
Tatizo ni nini? Basi tukumbushane vitu vidogo dogo vya kufanya gari yako ibaki mpya mpya ili ata siku ukitaka kuuza au ku-exchange au ku-upgrade thamani yake ibaki juu.
1. Fanya service kama inavyoshauriwa na usermanual ya gari yako. User manual zinapatikana google. Isome vizur ujue kila service na muda wake. Sio tu Oil na brake tunavyozoea. Kuna vitu vingi sana vya kuchange/replace au safisha.
2. Hakikisha gari ipo safi muda wote. Ndani na nje. Sio kila siku unapelela car wash, weekend unaweza kua unasafisha wewe mwenyewe na mke/mumeo/watoto ikiwa sehemu ya mazoezi. Wakati wa kusafisha pia tumia vitu kama viambaa maji na sabuni vinayoshauriwa na manufacturers.
3. Sio kila siku au kila sehemu lazima uende na gari. Najua hii ngumu sana mwenyewe naonaga shida sana. Especially ukiwa ndio gari ya kwaza hafu hujamaliza nayo ata mwaka mmoja. Ila jitahidi. Sehemu kama Bar, mpirani, au kipindi cha mvua sana unaweza siku moja moja ukaliacha. Hii itakusaidia pia kujua hali ya huko nje. Kuna watu tokea wanunue gari ata daladala hajawahi kupanda tena.
4. Endesha kistaarabu. Husiwe na haraka haraka. Vijana wengi wenye magari kama Porte, Subaru na Altezza huu ni ugonjwa wao. Wanahisi wanachelewa na kupitwa kwao mwiko. Twende taratibu utaepusha ajali kubwa na ndogo.
5. Usiwaamini Madereva wa bodaboda, bajaji na daladala. Hii kwa wakazi wa DSM mfano. Hao jamaa akili zao wanazijua wenyewe. Utakua unapigwa pasi kila siku usipokua makini.
6. Usipark gari kwenye jua kali kwa muda mrefu. Aisee jua la Tanzania mfano DSM linapausha gari hatari. Uwe unajitahidi kuweka chini ya kivuli au nunua covers kwa ajili ya gari yako.
7. Unavoendesha usiwe unaacha madirisha wazi (kushusha vioo). Especially ukiwa mjini ambako kuna vumbi na Moshi sana. Hivyo vitu vinapausha sana gari ndani.
8. Usiogoe kuwakanya abiria wako kama watoto wanaleta vurugu, wanawake wanaoweka miguu kwenye dashboard au wanaokulakula ndani. Hii itasaidia usafi wa ndani ya gari.
Vichache ndio hivyo wakuu. Asante.