Vitu vikubwa vitatu vilivyosababisha kesi ya ugaidi ifutwe na DPP

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Achana na ajabu la kesi ya ugaidi kufutwa!

Kuna vitu havitokei bahati mbaya ama kwa mara moja. Kila kitu kina mchakato wake. Mipango na utekelezaji

Kesi ya ugaidi iliyokuwa ikimkabili mwenyekiti Taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu imefutwa na washtakiwa wote wameachiwa huru kwa amri ya DPP bila masharti yoyote!

Hili lilitegemewa na wengi kutokana na mwenendo mzima wa kesi yenyewe hasa upande wa mashahidi na ushahidi dhidi ya watuhumiwa.

Ukiachana na hilo haya ndio mambo makuu matatu yaliyopelekea hii kesi kuwa na mwisho huu

1. Wito na hitaji la wahisani na wafadhili
Hawa ndio wanatusaidia kuendesha nchi kwenye upande wa pesa. Hawa kupitia balozi zao nchini walihudhuria mahakamani karibia kipindi chote cha kesi..Ni baada ya mahudhurio hayo waligundua tatizo na ukweli uliopo..hawa wakaweka mbinyo kuishinikiza serikali iachane na hii kesi ili waweze kutoa marundo

2. Kuhakikisha kunakuwa na usawa katika ulingo wa kisiasa na wafungwa wote wa kisiasa ndani na nje ya nchi wanahakikishiwa usalama wao, na ama kesi zao kufutwa na kuruhusiwa kufanya shughuli halali za kisiasa. Mkutano wa Belgium na Tundu Lissu ni kama tu ulifanya majumuisho wa hayo yote kisiasa, kijamii kisheria na mahusiano ya kimataifa.

3. Kwa marudio, ushahidi uliojaa matobo ya mashaka. Vithibiti vinavyoacha shaka nyingi. Hofu ya kupigwa kisheria kwenye utetezi.. Hapa walitumika watu mbalimbali kumuomba mwenyekiti aombe radhi ili kuiondolea serikali aibu. Kikao na viongozi wa dini kilitumika tu kukamilisha mpango mzima! Ili iwe kama safe exit ya mamlaka kwenye hii kesi.

Mbowe yuko huru. Lissu anarudi nchini. You can predict the feeling of both sides foes and friends!

Shukrani kubwa ni kwa:
  • Mungu mkuu
  • Viongozi wa dini waliosimama kidete kwenye hii kesi
  • Viongozi wa CHADEMA kwa mshikamano na kusimama imara
  • Mawakili na wanasheria
  • Wanachama, wapenzi, mashabiki na wote waliokuwa na mapenzi mema kwenye hii kesi
Ni mwanzo mwingine mpya. Ni turufu nyingine kwa CHADEMA!

Mungu ibariki CHADEMA!
 
"Kesi ya ugaidi iliyokuwa ikimkabili mwenyekiti Taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu imefutwa na washtakiwa wote wameachiwa huru kwa amri ya DPP bila masharti yoyote!"

Patamu sana hapa - bila masharti yoyote!

Mungu ibariki Chadema.
 
5. Kuepusha kuvuliwa nguo kwa viongozi mbalimbali kama wangeitwa kama mashahidi au kama ushahidi ungetolewa juu yao
1646396351898.png

Kwa makusudi kabisa majina ya mashahidi mengine yakahifadhiwa.

Sipati picha hali ingekuwa vipi mahakamani.
 
Achana na ajabu la kesi ya ugaidi kufutwa!

Kuna vitu havitokei bahati mbaya ama kwa mara moja. Kila kitu kina mchakato wake. Mipango na utekelezaji

Kesi ya ugaidi iliyokuwa ikimkabili mwenyekiti Taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu imefutwa na washtakiwa wote wameachiwa huru kwa amri ya DPP bila masharti yoyote!

Hili lilitegemewa na wengi kutokana na mwenendo mzima wa kesi yenyewe hasa upande wa mashahidi na ushahidi dhidi ya watuhumiwa.

Ukiachana na hilo haya ndio mambo makuu matatu yaliyopelekea hii kesi kuwa na mwisho huu

1. Wito na hitaji la wahisani na wafadhili
Hawa ndio wanatusaidia kuendesha nchi kwenye upande wa pesa. Hawa kupitia balozi zao nchini walihudhuria mahakamani karibia kipindi chote cha kesi..Ni baada ya mahudhurio hayo waligundua tatizo na ukweli uliopo..hawa wakaweka mbinyo kuishinikiza serikali iachane na hii kesi ili waweze kutoa marundo

2. Kuhakikisha kunakuwa na usawa katika ulingo wa kisiasa na wafungwa wote wa kisiasa ndani na nje ya nchi wanahakikishiwa usalama wao, na ama kesi zao kufutwa na kuruhusiwa kufanya shughuli halali za kisiasa. Mkutano wa Belgium na Tundu Lissu ni kama tu ulifanya majumuisho wa hayo yote kisiasa, kijamii kisheria na mahusiano ya kimataifa.

3. Kwa marudio, ushahidi uliojaa matobo ya mashaka. Vithibiti vinavyoacha shaka nyingi. Hofu ya kupigwa kisheria kwenye utetezi.. Hapa walitumika watu mbalimbali kumuomba mwenyekiti aombe radhi ili kuiondolea serikali aibu. Kikao na viongozi wa dini kilitumika tu kukamilisha mpango mzima! Ili iwe kama safe exit ya mamlaka kwenye hii kesi.

Mbowe yuko huru. Lissu anarudi nchini. You can predict the feeling of both sides foes and friends!

Shukrani kubwa ni kwa:
  • Mungu mkuu
  • Viongozi wa dini waliosimama kidete kwenye hii kesi
  • Viongozi wa CHADEMA kwa mshikamano na kusimama imara
  • Mawakili na wanasheria
  • Wanachama, wapenzi, mashabiki na wote waliokuwa na mapenzi mema kwenye hii kesi
Ni mwanzo mwingine mpya. Ni turufu nyingine kwa CHADEMA!

Mungu ibariki CHADEMA!
Lakini hii kesi imetusaidia kujua kuwa tuna viongozi wasio waadilifu, waongo na wanafiki sana. Wanashinda makanisani na misikitini kumbe ni waovu kuliko shetani mwenyewe
 
Shetani mtamtafuta hamtamwona sababu hayupo. Shetani ni viumbe wote waendao kinyume na Mwenyezi Mungu na kundi Lao ni hawa walioandaa na kujihusisha na kesi hii kwa nia ovu.
 
Kukichwa kutapambazuka ..
 
Wasioamini na kuugulia moyoni
1. Dr. Mstaafu mpigwa kibuti
2. Kabwela mwepesi
3.LMB7
4.SKMG
5.nk
Screenshot_20220304-182119.jpg
 
Nakuheshimu sana mtumishi wa Mungu mshana natamani kuonana nawewe sana mana hujawahi kua mjinga au punguani au pumbavu ,toka nakufahamu fanya mpango tuonane. Sema iwe lini
 
Back
Top Bottom