Vitu vinavyo mshusha Mama

Vitu vinavyo mshusha Mama

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
1. Kutokujua anataka nini kwenye siasa. Mara anataka demokrasia lakini hataki katiba mpya. Mara anataka katiba mpya lakini baada ya miaka mitatu. Mara anataka chaguzi huru lakini anataka mkwe wa TAMISEMI ndiye aongoze changuzi za mwaka 2024. Mara anatatuma mabadiliko ya tume huru wakati huohuo sheria bado hazijatoa tume huru. Mama unatakiwa usichanganye watu . Utataka Tanzania ya aina gani. Huwezi kuendelea kuwa na vitu nusunusu kama hivi utajitafutia matatizo zaidi tu.Uraisi unataka clarity Mama !
2. Mama hayuko serious kwenye rushwa. Rushwa ziko kila mahali na hakuna jitihada za maana za kuzuia rushwa wala ukali wa namna yeyote. Polisi rushwa zimezidi, miradi rushwa zimezidi, mikataba mfano wa DP world hauko wazi mpaka leo. Sasa wewe una tofauti gani na wala rushwa wengine kama Kikwete. Imefikia wakati mpaka Norway ndiye anahakikisha hakuna rushwa kwenye mikataba inayojadiliwa ya Gas za Mtwara na Lindi. Yaani tunapedwa na familia ya kifalme ya Norway kuliko hata wanasiasa wetu ambao wanatafuta jinsi ya kupewa rushwa na mambo yamegoma hivyo mpaka leo hakuna mkataba wowote!. Familia ya mfalme wamekuita na kukupa ukweli lakini umezungukwa na wala rushwa wakubwa na Kikwete gang ambao ni walafi wakubwa. Dr Matarajio ulimtoa TPDC ili wezi wamweke mtu wao
3. Maridhiano yako hayaaminiki. Je upo serious au ni michezo michezo ya kitoto. Je unataka nchi yetu iwe shindani na wenzetu ambao ni demokrasi kama Kenya, Uganda, Malawi au unataka uongozi wa kifamilia wa Kagame, Museveni kama Magufuli! Jitambue unataka nchi ya namna gani. Bila hivyo utaondoka hapo miezi miwili utaonekana kama ni janga.
4. Maendeleo ni bure bila demokrasia na mfumo mzuri. Unataka nini hasa
5. Kwa rekodi ya Makonda nchi nyingine zinakushangaa kumweka muuaji ambaye hata hajaomba msamaha. CIA wana facts zote. Unaonyesha hauko serious
 
Attachments

  • 750603EF-3B9B-4617-9919-3D3FBDB1B940.jpeg
    750603EF-3B9B-4617-9919-3D3FBDB1B940.jpeg
    52.8 KB · Views: 6
  • 566889E6-83AE-4537-B15D-151B22D96853.jpeg
    566889E6-83AE-4537-B15D-151B22D96853.jpeg
    103.3 KB · Views: 7
Ni hivi yeye huko ikulu alisema Mimi sitaweza ,wenzake wa msoga wakamwambia wewe kaa tu bado watanzania wanaweza kuongozwa na popo,mbuzi na hawana habari maana ukiamka asubuhi utawasikia Simba ameshinda,yanga na var yaani hakuna anayesema nauli zimepanda ,mtoto wangu anakaa chini wao wanamwachia mungu Kwa hiyo mtoa mada ni kwamba mama yupo Tu
 
Mimi mama ananikwaza anavyosema yeye ni mama analea. Uwiiiiii watu wakisikia hivyo ni kama anawafungulia. Nenda mahakamani huko ndo utajua nachomaanisha, walinzi wa haki wanakula milungula wazi wazi na yeye ni kama hasikii.

Wakikosea wanabadilishwa vyeo, ki ukweli namkubali mama kishingo upande siku hizi. Ananivunja sana moyo.
 
Huyo Mama unayemuongelea ndiyo yule aliyesema hadharani wakati ule anahojiwa hadharani na kituo kimoja maarufu cha habari cha nje ya kwamba kiongozi mmoja wa upinzani nchini mwake ni gaidi, na tayari kuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani!!

Halafu mwisho wa siku wananchi tukaishia kushudia tu maigizo!! Kama ni huyo basi tambua fika mumepigwa.
 
1. Kutokujua anataka nini kwenye siasa. Mara anataka demokrasia lakini hataki katiba mpya. Mara anataka katiba mpya lakini baada ya miaka mitatu. Mara anataka chaguzi huru lakini anataka mkwe wa TAMISEMI ndiye aongoze changuzi za mwaka 2024. Mara anatatuma mabadiliko ya tume huru wakati huohuo sheria bado hazijatoa tume huru. Mama unatakiwa usichanganye watu . Utataka Tanzania ya aina gani. Huwezi kuendelea kuwa na vitu nusunusu kama hivi utajitafutia matatizo zaidi tu.Uraisi unataka clarity Mama !
2. Mama hayuko serious kwenye rushwa. Rushwa ziko kila mahali na hakuna jitihada za maana za kuzuia rushwa wala ukali wa namna yeyote. Polisi rushwa zimezidi, miradi rushwa zimezidi, mikataba mfano wa DP world hauko wazi mpaka leo. Sasa wewe una tofauti gani na wala rushwa wengine kama Kikwete. Imefikia wakati mpaka Norway ndiye anahakikisha hakuna rushwa kwenye mikataba inayojadiliwa ya Gas za Mtwara na Lindi. Yaani tunapedwa na familia ya kifalme ya Norway kuliko hata wanasiasa wetu ambao wanatafuta jinsi ya kupewa rushwa na mambo yamegoma hivyo mpaka leo hakuna mkataba wowote!. Familia ya mfalme wamekuita na kukupa ukweli lakini umezungukwa na wala rushwa wakubwa na Kikwete gang ambao ni walafi wakubwa. Dr Matarajio ulimtoa TPDC ili wezi wamweke mtu wao
3. Maridhiano yako hayaaminiki. Je upo serious au ni michezo michezo ya kitoto. Je unataka nchi yetu iwe shindani na wenzetu ambao ni demokrasi kama Kenye, Uganda, Malawi au unataka uongozi wa kifamilia wa Kagame, Museveni kama Magufuli! Jitambue unataka nchi ya namna gani. Bila hivyo utaondoka hapo miezi miwili utaonekana kama ni janga.
4. Maendeleo ni bure bila demokrasia na mfumo mzuri. Unataka nini hasa
5. Kwa rekodi ya Makonda nchi nyingine zinakushangaa kumweka muuaji ambaye hata hajaomba msamaha. CIA wana facts zote. Unaonyesha hauko serious
Mama haeleweki, kauli ya Mh lema anatakiwa kuitafari apewe kadi ya chadema, yeye na Mwanae hawataweza mziki wa watoto wa mjini, ana options moja tu ,leta katiba mpya mezani basi , alafu sie ambao sio machawa wake tumpe njia za kumsaidia , ccm wamejaa wahuni tupu, ujumbe wa mh lema hueshimiwe
 
Naamini kamati zile husika,hazita kosea kuleta mgombea asiyekubalika 2025.
 
au unataka uongozi wa kifamilia wa Kagame, Museveni kama Magufuli!
Yani Magufuli unamweka kundi moja na akina Kagame na Museveni kwenye kutaka uongozi wa kifamilia? Hapa hauko serious.
Kwa 1 mpaka 3 nimekuelewa!
 
Yani Magufuli unamweka kundi moja na akina Kagame na Museveni kwenye kutaka uongozi wa kifamilia? Hapa hauko serious.
Kwa 1 mpaka 3 nimekuelewa!
Huyu mtoa mada ni wale wehu...

Hapo msingi wa mada yake ni Makonda, amejaribu kuficha ameshindwa...

Kumhusisha Magufuli sehemu asiyohusika si kwa bahati mbaya pia...
 
Back
Top Bottom