Vitu vinavyofukuza Wateja kwenye biashara yako

Remtuz

Senior Member
Joined
Mar 11, 2019
Posts
105
Reaction score
222
Moja ya kitu ambacho kinakimbiza wateja dukani kwako ni kupokea mteja huku umekaa. Kinaua mood ya wateja wengi sana. Mteja ni kama mgeni,a napokuja dukani kwako uchangamfu wako ndiyo utamfanya kununua. Hembu jiulize umeenda kwa rafiki yako, umefika anakukaribisha anakuacha sebuleni anaenda kupiga stori nnje na watu wengine utaruudi?

Sasa una duka mteja anakuja umekaa, anaulizia kitu flani umekaa unamuonyeshea kwa mkono tu au unamuambia ingia uangalie! Ndugu yangu labda kama unauza Oxygen kwamba nisiponunua nitakufa sirudi. Mteja akija kwako kwanza nyanyuka huku ukimkaribisha, akiulizia nguo flani nenda ishike, hata kama hutaki kuishusha lakini mgeukie muulize ni saizi gani, kama ni sahani muulize unataka rangi gani na chochote kile.

Unaponyanyuka kuna mambo mawili yanatokea, kwanza anahisi unamhehsimu, anaanza kujiona kuwa kumbe na yeye ni wa muhimu anaheshimiwa, lakini pili anaanza kuona aibu, anaona kuwa huyu nisiponunua nitakua nimemsumbua. Lakini pia kuna kitu cha tatu kinatokea na hiki ni chamuhimu zaidi, unaponyanyuka unamlazimisha kukaa dukani kwako kwa muda zaidi ili kuangalia vitu vingine.

Labda nikupe mfano tu, mteja kaja anaulizia una Lotion za Nivea, wewe huna kabisa, sasa kwa mtu ambaye hajui Biashara atasema sina akiwa kakaa anaendelea kuchezea simu yake akifuatilia sijui kama yale magari ni ya Zari au kakodi! Lakini kwa mfanyabiashara anajua kabisa kuwa hana Nivea ila atanyanyuka, ataenda kwenye shelfu la Lotion ataangalia kisha atasmea “Hizo zimetuishia ila tuna Nice and Lovely….”

Anageuka kidogo anamuangalia ngozi yake anauliza “Unapaka ya ngozi kavu au …” hapo mhusika hata kama haitaki lakini lazima akae kujibu lile swali kwakua umeuliza kistaarabu, ataangalia angalia na kutafuta kingine na hata asiponunua siku hiyo atarudi tena kwakua ulimuonyesha ukarimu. I;a mtu anakuja dukani, unakuta lijitu limenuna, au yuko bize na simu utafikiri kachanjiwa unaingia na kutoka hata hageuki halafu unaishia kusema “Huyu si mnunuaji?”

Yaani huwa nashangaa mtu mwingine analalamika wiki hajauza lakini anakuja huyo mteja mmoja anaacha kuweka simu pembeni akamhudumia unaacha kunyanyuka kumhudumia vizuri mpaka atamani kurudi tena! Kusimama mteja anapokuja kuna nguvu kubwa sana katika kumrudisha mteja, usijali ni wa namna gani simama tu hizo dakika tano ataona umemheshimu, fanya hivyo utanishukuru baadaye utakapotengeneza wateja wakudumu!... Tuangalie na. Wauzaji wa kuwaajili kutuuzia maduka yetu vinginevyo tunaweza kuwa tunalaumu mambo hayaendi cjui mauzo hamna kumbe wachawi ya biashara zetu ni sisi wenyewe kwa kuweka wauzaji wasioelewa wajibu wao kwani ukinyanyuka ukamskiliza mteja kwa dakika 2 au 5 unapyngukiwa nn kama ni smartphone yako au WhatsApp au Facebook si utaikuta*??? Karibu kwa maoni yako tujengene.
 
Kwa upande wa kusimama wakati wa kuzungumza na mteja mimi sioni shida.....lugha nzuri na sauti rafiki ndio muhimu.

Jambo ambalo halipendezi ni kumpuuza mteja anapoingia kwenye duka lako......unajikeep busy na habari zingine as if huyo mteja hakuhusu.

Kwa mfano mimi nikiingia katika maduka makubwa kama shopping malls na supermarkets huwa sipendi mtu anifuate wakati sijaomba msaada wowote maana muda huo ninakuwa nafanya window shopping na kuperuzi. Sitaki mtu aje pembeni au nyuma yangu akinifuata fuata na kunipa lile jicho la "unataka kununua nini, kama haununui kitu unafanya nini sasa hapo"
 
Me mtu akinifuata fuata nakosa kujiamini kabisa

Sio wateja wote wanapenda Jaliwa hivyo,mwingine anakuja na wazo lake mwenyewe toka huko..mfano: Anaweza akaja na wazo anataka simu ya SAMSUNG J1 ACE unamwambia hiyo simu hamna...unamshauri anunue TECNO PHANTOM yani atavyokuona unaleta ushawishi wa biashara kumshawishi achukue simu MBOVU,kumbe umemshauri simu nzuri sana ila yeye atona ni lugha zenu wafanyabiashara hata kitu kibaya Mtakisifia.

So mi nadhani mteja akija ni unamkaribisha,unamwacha aangalie atakacho,kama ni mnunuaji ATAULIZA ila wengine huangalia tu na hawataki ulizwa (mimi ni mmoja wapo nisie penda ulizwa ulizwa,we niachee nikitaka nitakuuliza) nadhani cha muhimu kwa mteja ni anapokua dukani kwako/sehemu ya kazi Hata kama unafanya kitu ACHA tulia kaa tayari kujibu atakachouliza.

Maneno maneno mengi kwenye biashara sio mazuri sana pia...Mpe tu attention yako mteja ila mwache atafute atakacho akiona hamna akiondoka mwambie KARIBU TENA..kwa upole na ukarimu.

Mteja utaetakiwa uanze mshawishi ni yule aliye point Bidhaa flani na akawa na nia kabisa tatizo tu HELA yake ni ndogo Huyo Ruksa yani ni mtashushana kwa uongo,maneno yote mpaka achukue..ila kabla mteja hajafanya selection yake MUACHE la sivyo utamkera mteja..(hasa mteja mimi)
 
Huwa naona kama nafukuzwa nikiwa naulizwa nataka nini ninapokwenda dukani kuperuzi bidhaa gani itanifaa......

Naweza nikawa napesa ila bado sijaridhia kununua......sasa inabidi niweke akili yangu sawa na kujiridhisha.....sasa akitokea mtu wa kunihoji hoji maswali hovyo huwa napata wakati mgumu sana......
 
kitu kingine mtu akiuliza ukimwambia huna ukiwa umekaa kuna ubaya gani.
kuna wateja wengine wana mambo ya ajabu.unaweza ukawa umekaa nje ya duka.akaja akakwambia "ingia dukani kwako"unamuuliza unataka nini si useme labda hicho kitu hamna.
mwingine alikuja kuuliza kitu nikamwambia bei."akasema hyo sio bei yake wenzio hawauzi hivyo"
yaani mteja anakuja na bei yake.
MIMI UWA NAMJIBU TU BASI SIUZI.
 
BIASHARA HAITAKI HAMAKI YA AINA HII MKUU.

WATEJA NI WA KUVUMILIWA NA KUNYENYEKEWA SANA.
 
yaani mteja kaja mara moja. alafu anakuletea maringo na kejeli.
Watu wa hardware tuna wateja wetu wa kudumu. Wanaokuelewa na unaowaelewa.
Sio mtu ndo mara yake ya kwanza alafu anataka akupangie bei.
 
Wacha weee
Huyo mteja wa kudumu alianzaje?

Ni bora kusmile na kupuuza kuliko kujibu shombo.

Unaweza kuona umefanikiwa sana kwa hao wateja wako kumbe ungejirekebisha ungekuwa na industry na siyo hardware tena
 
Kwa upande wa kusimama wakati wa kuzungumza na mteja mimi sioni shida.....lugha nzuri na sauti rafiki ndio muhimu.

Jambo ambalo halipendezi ni kumpuuza mteja anapoingia kwenye duka lako......unajikeep busy na habari zingine as if huyo mteja hakuhusu.

Kwa mfano mimi nikiingia katika maduka makubwa kama shopping malls na supermarkets huwa sipendi mtu anifuate wakati sijaomba msaada wowote maana muda huo ninakuwa nafanya window shopping na kuperuzi. Sitaki mtu aje pembeni au nyuma yangu akinifuata fuata na kunipa lile jicho la "unataka kununua nini, kama haununui kitu unafanya nini sasa hapo"
[emoji3][emoji3]alafu ndo tabia zao uko supermarket
 
Mteja hata umbebe mgongoni.
Kama sio mstaarabu atakutemea mate TU.
hata yeye mteja anatakiwa awe na kauli nzuri kwa muuzaji.
Kama Leo kaja mmoja anataka mirunda ya laki saba lakini yeye ni dalali kamleta mteja. Anataka katika kila mrunda nimpe 500 kwa mirunda 150.nimpe 75,000.nikamwambia sifanyi huo ujinga. Akaniambia nampeleke duka lingine nikamwambia mpeleke. Wa kaondoka.
wateja ukiwanyenyekea sana watakushika kalio
Wacha weee
Huyo mteja wa kudumu alianzaje?

Ni bora kusmile na kupuuza kuliko kujibu shombo.

Unaweza kuona umefanikiwa sana kwa hao wateja wako kumbe ungejirekebisha ungekuwa na industry na siyo hardware tena
 
Huko ni kuendeleza utumwa na utwana haramu karne ya 21, hasa katika biashara ya soko huria na ushindani wa kuvuta wateja kwa ndumba hata, ukimlamba miguu mteja kama hataki kununua atakuacha tu umekodoa macho bila kununua chochote. Kumbuka siyo kila mtu anayekuja katika biashara yako ni mteja, wengine ni watweza, ujakubeza na kupeleleza udhaifu wa meza.
 
Moja ya kitu ambacho kinakimbiza wateja dukani kwako ni kupokea mteja huku umekaa. Kinaua mood ya wateja wengi sana. Mteja ni kama mgeni,a napokuja dukani kwako uchangamfu wako ndiyo utamfanya kununua. Hembu jiulize umeenda kwa rafiki yako, umefika anakukaribisha anakuacha sebuleni anaenda kupiga stori nnje na watu wengine utaruudi?

Sasa una duka mteja anakuja umekaa, anaulizia kitu flani umekaa unamuonyeshea kwa mkono tu au unamuambia ingia uangalie! Ndugu yangu labda kama unauza Oxygen kwamba nisiponunua nitakufa sirudi. Mteja akija kwako kwanza nyanyuka huku ukimkaribisha, akiulizia nguo flani nenda ishike, hata kama hutaki kuishusha lakini mgeukie muulize ni saizi gani, kama ni sahani muulize unataka rangi gani na chochote kile.

Unaponyanyuka kuna mambo mawili yanatokea, kwanza anahisi unamhehsimu, anaanza kujiona kuwa kumbe na yeye ni wa muhimu anaheshimiwa, lakini pili anaanza kuona aibu, anaona kuwa huyu nisiponunua nitakua nimemsumbua. Lakini pia kuna kitu cha tatu kinatokea na hiki ni chamuhimu zaidi, unaponyanyuka unamlazimisha kukaa dukani kwako kwa muda zaidi ili kuangalia vitu vingine.

Labda nikupe mfano tu, mteja kaja anaulizia una Lotion za Nivea, wewe huna kabisa, sasa kwa mtu ambaye hajui Biashara atasema sina akiwa kakaa anaendelea kuchezea simu yake akifuatilia sijui kama yale magari ni ya Zari au kakodi! Lakini kwa mfanyabiashara anajua kabisa kuwa hana Nivea ila atanyanyuka, ataenda kwenye shelfu la Lotion ataangalia kisha atasmea “Hizo zimetuishia ila tuna Nice and Lovely….”

Anageuka kidogo anamuangalia ngozi yake anauliza “Unapaka ya ngozi kavu au …” hapo mhusika hata kama haitaki lakini lazima akae kujibu lile swali kwakua umeuliza kistaarabu, ataangalia angalia na kutafuta kingine na hata asiponunua siku hiyo atarudi tena kwakua ulimuonyesha ukarimu. I;a mtu anakuja dukani, unakuta lijitu limenuna, au yuko bize na simu utafikiri kachanjiwa unaingia na kutoka hata hageuki halafu unaishia kusema “Huyu si mnunuaji?”

Yaani huwa nashangaa mtu mwingine analalamika wiki hajauza lakini anakuja huyo mteja mmoja anaacha kuweka simu pembeni akamhudumia unaacha kunyanyuka kumhudumia vizuri mpaka atamani kurudi tena! Kusimama mteja anapokuja kuna nguvu kubwa sana katika kumrudisha mteja, usijali ni wa namna gani simama tu hizo dakika tano ataona umemheshimu, fanya hivyo utanishukuru baadaye utakapotengeneza wateja wakudumu!... Tuangalie na. Wauzaji wa kuwaajili kutuuzia maduka yetu vinginevyo tunaweza kuwa tunalaumu mambo hayaendi cjui mauzo hamna kumbe wachawi ya biashara zetu ni sisi wenyewe kwa kuweka wauzaji wasioelewa wajibu wao kwani ukinyanyuka ukamskiliza mteja kwa dakika 2 au 5 unapyngukiwa nn kama ni smartphone yako au WhatsApp au Facebook si utaikuta*??? Karibu kwa maoni yako tujengene.
...Somo jema la Customer Care mkuu. Asante.
 
Kwa upande wa kusimama wakati wa kuzungumza na mteja mimi sioni shida.....lugha nzuri na sauti rafiki ndio muhimu.

Jambo ambalo halipendezi ni kumpuuza mteja anapoingia kwenye duka lako......unajikeep busy na habari zingine as if huyo mteja hakuhusu.

Kwa mfano mimi nikiingia katika maduka makubwa kama shopping malls na supermarkets huwa sipendi mtu anifuate wakati sijaomba msaada wowote maana muda huo ninakuwa nafanya window shopping na kuperuzi. Sitaki mtu aje pembeni au nyuma yangu akinifuata fuata na kunipa lile jicho la "unataka kununua nini, kama haununui kitu unafanya nini sasa hapo"
...ama yule anayekufuata huku unahisi kabisa kuwa body language yake ni kama 'inakuambia' kuwa inataka kuhakikisha kuwa hufany uhalifu wa kudokoa kitu! Wanaudhi!![emoji57][emoji57]
 
Sisi tunao deal na wateja wa instagram tunasimama wapi?
 
Back
Top Bottom