Vitu vinavyokera na kufukuza wateja kwenye biashara

mm kokote ninapohitaji huduma nikikuta kijiwe siingii nipo very selective ofisini unawekaje kijiwe
Kuna dada ana kijiwe cha mihogo kitaa, hapo wamekaa full wagongeaji. Ukinunua tu jua sio yako peke yako.
 
...kuna duka hapa mtaani kwetu kila ifikapo saa 1 usiku kunajaa watu wanakunywa beer, sasa jinsi hivyo viti na meza vilivyopangwa hata naonaga jau kwenda pale usiku. Nafahamu ndio kila mtu ni mteja na ana haki ya kuhudumiwa ila ni Bora angewatengea sehemu pembeni maana hata ukipita pale hata kama hauendi hapo dukani basi hawaachi kukuzingua kibaya huyo Mangi hana choo hivyo hao jamaa wakishikwa na haja hujibanza na kukojoa kwenye fence za watu.
 
Nikivyoona kichwa cha uzi tu nimegungua fasta kuona kama point namba 6 itakuwepo kweli nimeikuta kufanya biashara mtaani inaboa sana wamekaa kwanje wanapiga Story.
 
Hao hata chenji zetu hawarudishagi zote,utasikia mia tano kesho ukija kesho chukua bia ya 1500 lipa 1000 ananuna mwambie jero ulibakinayo jana utasikia utasikia kaka bahili huyu,na matusi juu wanakera wa dada grosali bora hawa mabaa makubwa unajilipia cash hata kama bei kubwa utakua huna kinyongo.sijawahi ona bar kubwa zimwambie mteja sina chenji.
Kuna lingie unakuta labda ni Grocery, mwenyewe au kaunta anapenda gospel au bongo flava lakini wateja wanapenda ndombolo/bolingo. Hapo mtaskilizishwa minyimbo msioitaka weeee mpaka kero yaani.
 
Kuna lingie unakuta labda ni Grocery, mwenyewe au kaunta anapenda gospel au bongo flava lakini wateja wanapenda ndombolo/bolingo. Hapo mtaskilizishwa minyimbo msioitaka weeee mpaka kero yaani.
Huu upuuzi upo kwenye mabasi ya nyanda za juu kusini, gospel mwanzo mwisho tena old gospel za Rose Mhando from Iringa to Dar.
 
Hiyo point 8, imekuja kuwa kero! kuna wafanyabiashara hata bahasha za 100/- hawana madukani wanasubiri uje na mfuko kama vile muda wote utatokea nyumbani au utatembea na mfuko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…