Quartz360
Senior Member
- Mar 27, 2023
- 133
- 317
TANZANIA TUITAKAYO
MWANZO
Vijana ni hazina kwa taifa lolote lile duniani, taifa lisilokuwa na vijana wengi hukosa nguvu kazi hasa katika shughuli za uzalishaji mali, vijana wana nguvu, maarifa mapya, uthubutu na nia ya kuweza kuleta mabadiliko pale tu watakapopewa kipaumbele cha kuonyesha uwezo wao. Nchini Tanzania zaidi ya 50% ya watu wako chini ya miaka 35 kutokana na takwimu za sense ya watu na makazi ya mwaka 2022. Hivyo ni wazi kuwa taifa lina rasilimali watu ya kutosha kutoka kwa vijana, lakini wingi huo wa vijana umekuwa ni tatizo kubwa nchini kwetu kwani vijana wengi wamekuwa hawajiingizi katika shughuli za uzalishaji mali kama vile biashara kwa sababu mbalimbali wanazoona wao kuwa nikikwazo kwao kuweza kufanya biashara, hivyo ili tuweze kuwatengenezea vijana mazingira rafiki ya kufanyia biashara hatuna budi kuwa na mikakati shirikishi itakayovutia vijana kuingia katika fursa ya biashara .
KIINI
Serkali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo haina budi kufanya yafuatayo ili kuweza kuwavutia vijana kujiingiza kwenye sekta ya biashara na hatimaye kuweza kuwa na nguvukazi iliyo hai katika uzalishaji mali ndani ya jamii yetu, mikakati hii haina budi kufanywa;-
1. Kwenye kila kata kuundwe mamlaka husika itakayosimamia maslahi ya wafanyabiashara. Katika maeneo yaliyo mengi watu wengi hasa vijana wamekuwa wakishindwa kujiingiza kwenye biashara kutokana na changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara hasa kusumbuliwa na mamlaka mbalimbali na kukosa msaada wa kisheria, hivyo kwenye kila kata iundwe mamlaka maalumu itakayosimamia maslahi yao kikamilifu, japo kuna vyama vya wafanyabiashara maeneo m,balimbali lakini vimekuwa si msaada sana kwa wafanyabiashara walio wengi kwa kukosa sauti ya kimamlaka itakayowasaidia kupaza sauti zao.
2. Vijana wapewe elimu ya kodi pamoja na fedha. Mtu yeyote yule huweza kukosa uthubutu kwa kutokuwa na elimu sahihi juu ya jambo analotoaka kulifanya, hivyo katika kuwavutia vijana kujiingiza kwenye biashara ni vyema mamlaka husika ikaanzisha mafunzo ya mara kwa mara kwa mfano kila baada ya miezi sita ndani ya mwaka kuwepo kwa mafunzo ya wafanya biashara yenye lengo la kuwapa ujuzi juu ya masuala ya ulipaji kodi, elimu ya kifedha, malengo katika biashara zao, ubunifu, masoko na namna ya kuongeza thamani katika bidhaa ama huduma zao. Mafunzo hayo yaweze kutolewa na wataalamu wabobezi katika masuala ya kodi, fedha na biashara. Kwa kufanya hivyo, vijana wengi watakuwa na uelewa thabiti juu ya namna ya kuanzisha na kuziimarisha biashara zao kwa manufaa makubwa wakizingatia kanuni na taratibu zilizopo.
3. Mikopo kwa vijana isipewe kwa vikundi maalumu. Ni bora serikali ibadili mawazo juu ya namna ya kuwasaidia vijana, kwa sasa kwenye kila halmashauri kuna fedha iliyotengwa kwa ajili ya makundi maaalumu kama 10% ya mapato ya ndani ya halmashauri husika, ambapo vijana ni moja ya wanufaika, lakini namna ya utoaji wa hii mikopo imekuwa ni changamoto kubwa sana, malalamiko yamekuwa ni mengi juu ya wanufaika wa mikopo hiyo, namna ya kuipata mikopo hiyo, usimamizi na malengo ya mikopo hiyo, na hivyo kuleta manufaa kwa watuy wachache huku wengi wakibaki bila msaada. Hivyo ni bora serikali ianzishe mamlaka yenye kusimamia mikopo kwa wajasiliamali wagodo, mikopo hiyo itolewe kwa mtu mmoja mmoja kwa kuzingatia kanuni na taratibu zitakazo wekwa , mikopo hiyo iwe ni ya riba nafuu ikiendana na utoaji wa elimu sahihi kwa mtu husika, hivyo serikali ni vyema ikalifikiria hili kwani litaleta chachu ya vijana kuweza kujiingiza kwenye biasahra ama kupata mikopo nafuu ya kuweza kuboresha biahsara zao. Vilevile kuwepo na mikopo maaalumu kwa vijana wote wenye mawazo ya kibiahsa ra yenye kuleta mageuzi makubwa katika nchi yetu hasa katika sekta ya elimu,afya,kilimo na teknolojia, vijana hawa wapewe usaidizi wa karibu, waendelezwe, wapewe elimu bora, mazingira wezeshi Pamoja na mitaji ili waweze kufanikisha utekelezaji wa mawazo yao katika jamii, hii itachochea mawazo yenye ubunifu na mageuzi makubwa katika taifa letu kwenye siku za usoni.
4. Sera ya kutokulipa kodi ndani ya mwaka wa kwanza kwa biashara mpya hasa ndogondogo itekelezwe kikamilifu. Serikali imekuwa ikigusia juu ya suala la kutowatoza kodi vijana wote wanaoanzisha biashara mpya ili kuweza kulinda ukuaji wa biashaara zao lakini sera hii imeshindwa kutekelezwa kikamilifu kwani mpaka sasa biashara zote mpya zinazoanzishwa na vijana zimekuwa zikikutana na vikwazo kutoka mamlaka mbalimbali hasa katika masuala ya ulipaji kodi kwenda TRA na hili kufanya biashara zao kufa, kwani biahsara zinakuwa bado hazijaweza kusimama imara kudhalisha mapato ya kutosha, hivyo kuweza kujiendesha kwa hasara, lakini kama sera hiyo itasimamiowa kikamilfui hakuna kijana atakaye kuwa mzito kuanzisha biashara kama rasilimali fedha atakuwa nayo.
5. Kuwe na utaratibu maalumu wa ulipaji wa kodi na kupunguza kodi zisizo za lazima ili kulinda ukuaji wa sekta ya biashara. Vijana wengi wanaogopa kuanzisha biashara kutokana msururu wa kodi kutoka kwenye mamlaka, usumbufu na changamoto zingine zinazohatarisha ustawi wa biashara katika taifa letu, ni vyema mamlaka ya mapato Tanzania ije na mbinu mpya ya namna ya kufanya makadilio ya kodi, madai ya kodi na namna ya utoaji wa vibali. Kuna biashara nyingi huweza kufungwa ama kufa kila mwaka kutokana na hatua zinazochukuliwa na mamlaka husika katika suala la ulipaji wa kodi, japo mamlaka husika ina jukumu la kukusanya kodi kwa manufaa mapana ya taifa letu lakini ni bora pia ifikirie juu ya ustawi wa biashara za watu wake, iandae mifumo mizuri ya makadilio ya kodi yenye faida shindani kwa pande zote mbili, kuondoa kodi zisizo na ulazima, kuja na mbadala wa kufungia biashara za wafanyabiashara zitakazo punguza tatizo la kufa kwa biashara nyingi katika nchi yetu.
MWISHO
Serikali bora ni ile inayofanya kazi kwa maslahi makubwa ya watu wake, serikali bora ni ile inayosikia kilio na hoja za watu wake, hivyo serikali isikie pia kilio cha watu wake katika sekta ya biashara, kuwepo kwa sera bora za ufanyaji wa biashara, sheria zisimamiwe kimakilifu, uadifu uwepo na mazingira bora ya kufanyia biashara yaimarishwe, hii tu haitahamasisha vijana wa kitanzania kujiingiza kwenye biashara bali hata watu kutoka nje ya nchi watavutiwa kuja kuwekeza nchini kwetu.

Upvote
3