Vitu vitatu vikuu ambavyo huumba matokeo ya malipo ya bili yako ya umeme katika jengo lako.

Vitu vitatu vikuu ambavyo huumba matokeo ya malipo ya bili yako ya umeme katika jengo lako.

Transistor

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,061
Reaction score
1,637
Kuna vitu vitatu vikuu ambavyo huumba matokeo ya malipo ya bili yako ya umeme.

1.Muda wa matumizi ya vifaa vyako kwa siku.(Time)

2.Ukubwa wa vifaa vyako kimatumizi( Wattage)

3.Ubovu wa miundombinu ya mfumo wa umeme au vifaa vyenyewe vinavyotumia umeme huo.(Default on appliances or Electrical devices).

Niaatanza kuongelea Kigezo cha Muda.

1. MUDA WA MATUMIZI YA UMEME

Muda wa matumizi ni "variable" Muhimu sana katika kujua kiasi cha umeme utakacho Tumia

Mfano Nyumba A, na Nyumba B zote zina vifaa vinavyo fanana.

Au mpangaji A na mpangaji B wote wana vifaa vinavyifanana.

*Tuchukulie mfano kifaa kimoja ambacho ni Televison (TV).

Ambao mwenye nyumba A ana familia inayoshinda nyumbani mchana na usiku ambao hutazama TV kwa maasaa12, TV ina watt 30

Na nyumba B yeye hana familia ni mtu mmoja tu,mchana anakuwa kazini akirudi nyumbani huangalia Tv kwa masaa 4 tu, TV ina Watt 30

Licha ya kua na vifaa vinavyofanana kwa kila kitu matumizi yao kwa mwezi yatatofautiana.

kuangalia TV kwa mwezi
mzima nyumba A gharama itakua

*Nyumba A itatumia UNIT (30wx12mudax30siku)=Unit 10.8,kwa mwezi

Sawa na kiasi cha (UNIT 10.8 x Bei ya unit moja ya umeme346)=Tsh 3,700

*Nyumba B itatumia UNIT (30wx4masaax30siku)=Unit 3.6, kwa mwezi

Sawa na kiasi cha (UNIT 3.6x Bei ya unit moja ya umeme 346=Tsh 1,245

Hivyo nyumba ya jirani yako au mpangaji mwenzako,inaweza kua na vifaa kama vyako ila mkawa na matumizi tofauti kimuda ikasababisha,mkalipa bili ya umeme tofauti sababu tu ya matumizi yenu kwa kigezo cha muda.

Ndio maana kipindi cha likizo ya watoto nyumba yako bili ya umeme hupanda...hii so sababu kuna hitirafu hapana ni kwasababu matumizi ya vifaa vya umeme yanaongezeka.

Nitaendelea baadae.....Kujadili kuhusu .....wattage.

****************************

Tunapo tazama sababu ya nyumba kua na bili kubwa ya umeme ambayo mwenye nyumba anatilia shaka,Hua pia tunajaribu kuuliza muda anao tumia vifaa vyake,hata kama vifaa vyake vina watt ndogo...

Kwa nyumba ambayo Wahusika au mhusika anahisi ina shida ya kuwa na bili kubwa ya umeme kuliko matumizi....Unaweza kuwasiliana nasi kwa uchaguzi na kujilidhisha,ili kama hakuna tatizo ubadilishe tabia ya matumizi ila kuna tatizo tuweze kulitatua.

Pia kwa nyumba ambayo itakua inaonekana haina shida ya kiufundi lakini matumizi yake yapo juu,tunatoa huduma ya kushauri na kuboresha mifumo ya umeme na vifaa vilivyofungwa,ambapo unaweza punguza matumizi hadi asilimia 40%...

Pia kwa wanaojenga nyumba mpya tunatoa ushauri wa vifaa vya kununua kwa kigezo cha kuepuka kuja kulipa bili kubwa hapo baadae.

Vilevile tunatoa huduma ya kufunga mifumo ya umeme katika nyumba mbalimbali na viwandani.

Transistor

0678147325.
 
Hii dhana ya kama friji ukiliwasha na kuliacha muda bila kulizima inakua aili umeme mwingi ni kweli?
 
Hii dhana ya kama friji ukiliwasha na kuliacha muda bila kulizima inakua aili umeme mwingi ni kweli?
Ni kweli kama tu ni friji ambalo vihisi vyake(Sensors),vinafanya kazi vizuri...

Sensor itakapotambua baridi imefikia kiwango cha kutosha,huliamlisha friji liwe katika "sleeping mode" ambapo huzima compressor automatic na kumaintain baridi iliyopo hadi pale baridi itakapo shuka litaamka tena na kuwasha composer.

Kipindi ambacho friji inakuja katika sleeping mode matumizi yake ya umeme huwa kidogo sana,hadi litakapo washa compressor tena,fahamu kinachokula umeme katika friji mi compressor kwa asilimia 80...

Hakikisha friji lako lina jiwasha na kujizima lenyewe kulingana na kiasi cha baridi kilichosetiwa.

Kama linaunguruma moja kwa moja basi linaweza kua halina gesi,au linavujisha baridi au sensor zake zimekufa,hivyo litakula umeme kuliko kawaida au kipimo chake.
 
Maelezo yako yana make sense lakini inategemea friji linazimwa kwa muda gani. Thermostat kuwasha na kuzima friji haiwezi kuwa sawa na friji linalozimwa 12hrs out of 24hrs. Kuna kipindi nilikuwa siweki chakula kwenye friji kuna vinywaji tu hivyo nikitoka asubuhi nalizima nikirudi jioni naliwasha hadi asubuhi na kwasababu nikizima halifunguliwi jioni nakuta vitu bado vya baridi. Matumizi yangu ya umeme yalishuka sana. Sasa hivi nalazimika kuliwasha muda wote matumizi yameongezeka ingawa kama lingekuwa halijizimi baridi ikifika kiwango, matumizi yangekuwa makubwa zaidi.
 
Nilimjibu kama friji lipo katika matumizi ya kawaida...kama kulizima masaa 12 hadi 24...hilo halipo katika matumizi ya kawaida.
 
Back
Top Bottom