Makusanyo ya kodi za Tanzania hayafikii malengo kwa sababu ya vitu vitatu vikubwa
1. Machinga: Hatuwezi kuwa na kundi la watu wasiolipa kodi na wawe na haki kuliko walipa kodi. Huwezi kuruhusu wamachinga kuuza vitu vipya bila kodi na sehemu yoyote na hata mbele ya maduka ya walipa kodi. Wanachafua mazingira sana sehemu za barabarani na kuongeza gharama za ushafishaji maji na mitaro. Bila kutafuta utaratibu mzuri wamachinga wanapunguza sana makusanyo ya kodi huo ndiyo ukweli. Yaani unaweza kuwa na machinga wako usilipe kodi hata kidogo.
2. Wanunuzi wanaokubali kulipa kidogo na kukwepa kodi. Mtu yeyote anayekubali kununua kitu bila risiti na wale wauzaji wanaotoa vitu kwa bei ya chini kama hutaki risiti inatakiwa wafungwe. Hii itazuia hii tabia yaani nchi nyingine kuuza bila kutoa risiti ni uhujumu uchumi. Huruma huruma inatakiwa kuisha.
3. Madalali wengi wanapunguza kodi na kuzuia teknologia kutumika mfano kwenye magari kungekuwa na utaratibu wa kununua ticket kwa simu pekee ili kodi ilipwe hukohuko lakini madalali wamekuwa na nguvu za kuzuia maendeleo haya. Lakini kuna madalali wa nyumba, mazao .... ambao hawana tija kwa taifa letu. Udalali usio na manufaa nao upigwe marufuku