Vitu vya kufanya Ukiazima Gari la Mtu

Vitu vya kufanya Ukiazima Gari la Mtu

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wakuu habari.

Kwa maisha ya sasa gari imekua kitu cha muhimu sana. Pamoja na kwamba kuna Uber, Taxify, Taxi, Bajaji, Daladala na Bodaboda, bado private car ina-umuhimu wake.

Kwa wasio na magari, inatokea kipindi inabidi uazime ikitokea shughuli ya muhimu sana ambayo public transport haitafaa au itakua gharama sana. Ata wenye magari uwa wanaazima endapo yao mabovu, au yapo chini sana haya wezi faa njia fulani, au hayawezi accomodate idadi fulani ya watu etc.

Sasa kwa ushauri, ukiazima gari kwa rafiki au ndugu yako, fanya yafuatayo:

1. Endesha na kulihudumia ilo gari kama lako. Kua nalo makini usiendeshe rough.

2. Angalia kama linadaiwa na polisi. Tumia *152*75# kwenye simu yako.

3. Unavorudisha hakikisha lina mafuta zaidi kama hamkukubaliana kumpa hela unavorudisha (ata lita 5 zaidi) ya uliyoyakuta. Kwenye gari lita 1 ina thamani sana.

4. Rudisha likiwa safi ata kama ulipewa chafu. Pitisha car wash lisafishwee.

5. Usimuagize mtu mwingine alirudishe.

6. Ikitokea tatizo lolote ata kama dogo, mpigie simu mwambie. Mfano umechubuliwa rangi padogo na Bodaboda mtaarifu. Na jiandae kuchangia au kugharamia repar.

7. Usipitishe muda mliokubariana. Kama ulisema utarudisha jioni hakikisha jioni kurudi mapema. Otherwise toa taarifa mapema.

Ukijitahidi kufanya hayo machache, umejiwekea chance kubwa kuazimwa tena next time.
 
WAMESIKIA NA KUELEWA. Sio mtu unamwazima gari linarudi linanuka SIGARA TUPU, wengine hadi matapishi.

Mtu anaazima gari kila siku, mwisho mwenye nalo ndio anakuwa kama huwa anaazima, MAANA ANAONEKANA NALO MARA MOJAMOJA TU
 
Hiyo namba 2 mwenye gari linamuhusu zaidi baada ya kuazimisha gari.

Aliyeazima akirudisha inabidi uangalie kwanza, inawezekana alipigwa fine, af akasahau/akauchuna kukwambia baadae unakuja kuingia gharama mwenyewe wa kuzilipa.
 
Hiyo namba 2 mwenye gari linamuhusu zaidi baada ya kuazimisha gari.

Aliyeazima akirudisha inabidi uangalie kwanza, inawezekana alipigwa fine, af akasahau/akauchuna kukwambia baadae unakuja kuingia gharama mwenyewe wa kuzilipa.
Sure kaka. Na penalt zao zinavokimbizana. Utakuta imefika mara 2
 
Hata iweje siwezi kumuazima mtu gari langu labda ndugu yangu wa damu moja tu.
 
One last thing usiazime gari kama huna au hujawah miliki ....mi niwe na bajaj nitampa mtu ambae anayo au huwa anaendesha na nina muona ....eg unampa mtu baskeli anachukulia simple tu kapita sehemu kaipiga changer ile afu anakuja kukwambia zile si ni elfu tano tu kumbe mwenyewe huwa hutumii vitu vya dukan . Hapo kashakuingiza hasara ya 25K si bora ungempa tu buku ya boda boda
 
Back
Top Bottom