matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Jamii Ina stress kubwa za kiuchumi, kimalezi, kimahusiano na za hisia za kurogwa.
Wafanyamazingaombwe, waganga na matapeli jasiri wameiona hii fursa na kujitengenezea vilinge vya kujitajirisha kupita watu waliopoteza matumaini.
Hivi ni vitu vichache vya kuzingatia kabla hujaamua kuwa mteja wa unabii wa uongo.
1: ANATUMIA MUDA MWINGI KUTAMKA MANENO YAKE KULIKO YA MUNGU
Yeye ndio kiini cha ibada. Asipokuwepo unajisikia mpweke. Hii inajumuisha kuweka picha yake na mke wake kama logo ya kanisa. Hapo hakuna Mungu, mungu ni huyo jamaa.
2: VITISHO
Kama unaona unatishwa kutoa sadaka, kufunguka Siri zako, kuhofu mtu kuliko Mungu, hapo hakuna ibada kwa Mungu. Unaabudu unachokiogopa.
3: UMAKINI WA IBADA AU KIIJI NI ISHARA, MIUJIZA MAAJABU NA MAFANIKIO YA DUNIANI
Lengo kuu la biblia ni baada ya yote watu watoke DUNIANI na wapelekwe Mahali bora kuliko PA Sasa. Yaani nchi mpya. Kipaumbele ni uzima wa milele au ufalme wa Mungu hayo yote ni mengineyo. Ukiona kanisa au huduma inakubwisha mengineyo na kudogosha na kukawaidisha Mambo ya uzima wa milele kwa kisingizio cha miujiza hapo ni PA uongo. Ni pigio la wahuni.
4: Kubagua vitabu. Kusema agano la kale halifai linafaa jipya wakati imeandikwa Kila andiko lafaa kwa mafundisho. Hapo kimbia.
5: MAVAZI YA MTUMISHI NA MIZIKI NA MABURUDISHO YA KIDUNIA
Ukiona MTUMISHI anapenda mizaha na vichekesho, anavaa MAVAZI ya kihuni hata anapokuwa nje ya madhabahu, anaunga mkono MIZIKI ya KIDUNIA iliyopakwa Jina la Yesu, hapo mahala Pana mapepo wengi kuliko Malaika hapakufai.
YAKO mengi, Ila leo ni hayo tu, yafanyie kazi. MTUMISHI sio baba yako baba yako aliye kuzaa ni Mungu. Usiogope kumkimbia kwa ajili ya ustawi wa hatma yako.
Ni hayo tu, mwenye hekima atayafanyia Kazi, mbishi nikutakie kupigwa kwema.