Elisha Chuma
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 282
- 275
Kwanza niwape hongera ambao tayari wameshafanikiwa kupata vitambulisho vya kupigia kura kwa nchi nzima na niwape pole kwa wale ambao bado hawajapata na pia nnawatia moyo kuendelea kuvifuatilia vina maana sana kwa maisha yako naya kizazi chako cha sasa na cha baadae.
Baada ya kutoa salamu hizo sasa nirudi kwenye mada kuu leo hapo juu, taifa letu linapoteza sana nguvu kazi ya taifa katika vitu ambavyo havina mafanikio na malengo chanya kwa maisha ya mhusika na taifa na kutokana na kupunguza umakini katika hilo sasa hivi tumejikuta vijana wengi wanamaliza mafunzo ya elimu zao lakini hawana kazi wanabaki kuwa omba omba na wadandiaji wa kazi wasizokuwa na weledi nazo.
Leo nitaongelea kwa upande wa wajasiriamali wadogo ambao wanafanya biashara ndogo ndogo kwa minajili ya kupata kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku na wale ambao wanafikira kuingia katika ujasiriamali au biashara.
Asilimia kubwa sana ya vijana wanafeli katika biashara na ujasiriamali kwa kukosea baadhi ya vitu ambavyo walitakiwa wavifahamu mapema lakini wanajikuta vinawarudisha na nyuma na kufeli.
Katika hali ya kawaida unaweza kuona kama hakuna kilichopotea lakini ukiangalia kwa undani utaona umepoteza muda,ufanisi,mali na hata malengo kwa ajili ya kutegemea kitu ambacho haukuwa na malengo nacho.
Baadhi ya vitu hivyo ni pamoja na :-
1- MUDA
Asilimia kubwa sana ya wajasiriamali wadogo wanafeli kutokana na kutokufanya mahesabu ya muda wao na biashara au ujasiriamali wanaoufanya ambapo matokeo yake inakuja kuwa tofauti na malengo sababu kama haujaset muda hauwezi kuwa na malengo thabiti.
Wajasiriamali wengi wamekuwa hawana uwekezaji mzuri katika wakati utakuta mtu anaanzisha ujasiriamali kwa ajili ya kujaribu na inamchukua muda mwingi bila ya kuuhesabu matokeo yake umri na malengo vinapishana anajikuta hawezi tena kufanyia kazi malengo mama anaishia kujishikiza shikiza na vijikazi au kibarua ili mradi apate chochote kitu kwa ajili yake au yeye na familia yake.
Hivyo unapoamua kufanya ujasiriamali amua kufanya na jifunge kibwebwe kupambana na kila kitu na muda uwe ndio wa msingi kwako hata tunaowaita mifano hai walitumia vizuri muda wao kuna walioacha shule,Chuo,kazi nk lakini unaacha tu pale unapoona muda wako na malengo vinapishana iwapo utaendelea kufanya hiki na kusubirisha malengo yako utakuwa unapoteza muda mwingi lakini usimamizi wa muda ni muhimu.
2-MALENGO
Baada ya kuangalia muda sasa tunakuja pacha wake malengo.Malengo katika biashara au ujasiriamali ni muhimu sana lakini kwa wajisiriamali wadogo wadogo wengi wao huwa hawana malengo ila wana matarajio hawaweki malengo kwa ajili ya ujasiriamali au biashara yao wao wanasubiri matarajio ya biashara yenyewe itakavyokuwa unapofanya biashara.
Au ujasiriamali ni sawa na unaingia vitani hauwezi kuingia vitani unategemea vita itaamua mimi napambana tu, halafu uje ushinde kwa kishindo japo kuna wenye bahati vita ikawa ni nyepesi ukashinda lakini kwa vile ushindi wako ni mwepesi huwezi kupata fundisho kutokana na vita hiyo ni rahisi sana kwa wewe kubweteka na ushindi kwa kujiona unaweza kumbe umekutana na mvua nyepesi siku adui akirudi kwa ajili ya vita utashindwa vibaya nimeelezea dhana nzima ya kwann uweke malengo katika ujasiriamali au biashara yako mapema sababu biashara ni vita.