Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Wednesday, July 08, 2009 4:45 AM
Mwanamke mmoja wa nchini Ghana ameamua kufunga ndoa na mbwa wake kwa kuwa hajaona mwanaume mwenye sifa kama za baba yake aliyefariki kwani wanaume wote aliokutana nao wanafukuzia vya ndani ya sketi tu na wala si waaminifu. Emily Mabou, 29, wa mji wa Aburi, Ghana aliozeshwa mbwa mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu katika sherehe ya harusi ambayo iliendeshwa na kiongozi wa dini za jadi wa kijiji na kuhudhuriwa na wanakijiji wengi waliotaka kushuhudia kituko hicho cha mwaka.
Kaka wa mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la David Mabou alisema kuwa familia yake iliisusia harusi hiyo kwa kuwa waliona ni hatua ya kipumbavu ya kupambana na upweke.
"Kwa miaka mingi nimekuwa nikisali nipate mwenza katika maisha ambaye atakuwa na sifa kama za baba yangu. Baba yangu alikuwa ni mwema na mwanimifu kwa mama yangu hakuwahi kumvunja moyo mama" alisema mwanamke huyo.
"Nimewahi kuwa katika uhusiano na wanaume wengi lakini wanaume wote ni sawa na wote wanafukuzia vya ndani ya sketi tu halafu si waaminifu" alisema Emily.
"Mbwa wangu ni mwema na ananitii sana na ana heshima sana kwangu".
Mwanzoni kabla ya harusi hiyo kuanza kiongozi huyo wa dini za jadi wa kijiji aliwaonya wanakijiji wasiizomee harusi hiyo bali wajiunge na Emily kufurahi kwani hatimaye amefanikiwa kumpata wa kumfariji.
Alipoulizwa inakuwaje uwezekano wa kupata mtoto na mume wake huyo mpya, Emily alijibu kwa kusema "Tutachukua watoto yatima na kuwalea".
nifahamishe.com
Last edited by a moderator: