Angel Nylon
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 9,164
- 18,402
Habari zenu wanajiko.
Leo ningependa tushee mambo yanayotutokea jikoni, yale ya vituko vituko.
Mie mengi yamewahi kunikuta lkn ntaweka machache tu.
Kuna siku mama yangu aliniwachia niangalie pishi la mseto, sikujua kama kabla haujaepuliwa haukorogwi na mwiko si niukoroge, wacha mseto uungue. Nligombwajeee mpk leo nimejua kama mseto haukorogwi hadi uepuliwe ndo usongwe kama ugali.
Nlikua nkikaa jikoni na mama kupika, pishi kama halijaja vizuri basi hufukuzwa jikoni ati naambiwa macho yangu ndo yameharibu, lol.
Kuna siku nlikuwa nataka kukaanga chips, nkakosea kwenye karai badala ya kuweka mafuta nkaweka siki, si muda jikoni kumejaa moshi na harufu ya ajabu kuja kuangalia kumbe nimebeba chupa ya siki badala ya mafuta.
Usiombe kuumua maandazi ukaweka sukari nyingi, utalala hata siku mbili hayajaumuka, hii mpk leo hii mi mwenzenu mara hubugi step.
Haya wana jiko hem na wengine waeleze vituko vinavowapata jikoni, au vilowahi kuwapata wakati wanjifundisha kupika, au kitu gani hupendi uwapo jikoni.