Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Mke alipekua simu ya mumewe akakuta haya majina;
1. Tender one (Mwangalizi mwema)
2. Amazing one (Mtu mwema)
3. Lady of my dreams (Mwanamke wa ndoto zangu)
Akahisi ni michepuko ya mumewe. Akampigia "Tender one" akapokea mama mkwe (mama wa mumewe). Akampigia "Amazing one" akapokea wifi yake (dada wa mumewe). Kisha akampigia "Lady of my Dreams" simu yake ikaita.
Akalia sana hadi macho yake yakavimba kabisa na kuwa mekundu kwani alikuwa akimtilia shaka mumewe. Akamuomba mumewe msamaha kwa kumuwazia mabaya. Kisha akampatia mshahara wake wa mwezi mmoja kama zawadi.
Mke akaenda kumueleza mama mkwe wake kisa hicho. Mama mkwe akafurahi sana jinsi mwanae anavyojali familia yake, hivyo akauza mkufu wake wa dhahabu na kumpatia mwanae hiyo pesa kama zawadi.
Yule jamaa akamshukuru sana mkewe na mama yake kwa zawadi zile, kisha akachukua zile pesa akamnunulia zawadi "mchepuko" wake aliyekuwa amem-save kwenye simu kama "Baraka Fundi Umeme"