Sanamu la Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere limezinduliwa katika Bustani ya Mashujaa jijini Havana, Cuba na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje wa Cuba, Anayansi Rodriguez Camejo.
Kuzinduliwa kwa sanamu hilo ni sehemu ya kuenzi mchango wa Hayati Mwalimu Nyerere katika kuimarisha ushirikiano wa mataifa hayo mawili.