Kila mtu kwenye haya maisha ana umuhimu wake, ni suala la muda tu umuhimu wa mtu kuonekana. Leo, walewale machinga, tunaowaita wazururaji, ndio wameokoa watu wengi zaidi kuliko wale tunaowalipa mishahara. Kila mtu aheshimiwe, apewe thamani anayostahili na tutumie busara juu yao.