Vituko na vioja vya wadada wa benki

Sipingi mawazo yako ila sina hakika kama ulichoandika umekisoma kabla ya kupost, ivi kwenye nyakati hizi unawezaje kumlazimisha mtu kuwa na benki moja? Kwanini niwe na mtu maalumu wakunihudumia? Ukiwa mikoani utasafiri naye? Kinachotakiwa nikuwaonya mimi siwakawizi ukinijibu ovyo nitakushughlikia apoapo sikukawizi maana awa ni vijana wetu lazima tuwasaidie hawajui watendalo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japokua nasisi wateja wakati mwingine tunawakwaza ila wanapaswa tuu kutuchukulia na kutupa huduma nzuri
Ndio kazi yao kuhudumia wateja wenye shida mbalimbali na haiba tofauti tofauyi
 
Sasa huu ndo ujinga wa watanzania.
Yaani hupewi huduma Bora mpaka ujulikane ama ujichekeshechekeshe kwa muhudumu.

Kuna haja gani kutafuta urafiki wa kujipendekeza kwa muhudumu njaa wa benki kisa nipate huduma? Hii nayo ni aina ya rushwa.

Kama huduma ziko standard a watu wanaju kwa nini wako pale ,hakuna haja ya kufahamiana sijui kwa majina ama meneja, labda ishu inayohitaji utatuzi ambao ni some how personal.

Huu ni udhaifu wa watu waoga na wavivu kufuatilia haki zao. Uoga huu huwafanya kujiweka chini ya watoa huduma ili kupata favour.

Binafsi huwa sitakagi ujinga, jambo kubwa huwa ni kutambua wajibu wangu kama mpokea huduma na pia kufahamu wajibu wa mtoa huduma kwangu sihitaji urafiki hapo.

Nikigundua unaniletea nyodo, mbwembwe,urasimu ama upumbavu wowote kinyume cha wajibu wako huwa sikawii kukufanya ujute.

Kujiamini,exposure, uelewa watanzania wengi hawana na ndio sababu ya kuuziwa haki zao .

Watanzania wenzangu ndo maana kila akipewa huduma nzuri anahisi ni mtego ili atoe fedha ama lazima atatoa rushwa ya fedha, mdomo(ahsante) ama vitendo(kujichekeshachekesha)

Hivi hamjui kuwa hawa watoa huduma wapo kazini na wanatekeleza wajibu wao?

Hawahitaji hata ahsante maana wanastahili kulipwa na waajiri wao endapo tu wanafikia malengo ambayo bila shaka ni kutoa huduma Bora kwa wateja.

Hakuna haja ya kusema hata asante kwa mtoa huduma bali wewe mteja ndo unatakiwa uambiwe ahsante kwa kumpelekea pesa ambayo bila hiyo yeye hana mshahara.

Kwa kifupi mi ni sehemu ya waajiri wake, yeye ndio wa kuninyenyekea mimi na kupiga magoti na kuruka kichurachura endapo nitahitaji afanye hivyo.

Siwezi tetemeshwa na mtoa huduma ama kwa lugha nyepesi muhudumu wa idara yeyote maana bila mimi yeye hana ajira.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo maswali jibu wewe maana hamna sehemu nimelazimisha mtu awe na bank moja. Hio ni experience yangu. Pamoja na kusema wahudumu Wana huduma mbovu ila Wabongo wengi pia wako hivyo hivyo,dharau kejeli kwenye kazi za watu, michango ya humu ni ushahidi.
 
Mi nimekutana nalo mara kadhaa kuna simu nilifungua chap chap acount nilitaka kudepost pesa ...baada ya kufungua nikauliza naweza kuweka 30 m wakaanza umezitoa wapi

Nikawajibu ninazo hapa nikaona wananizingua kisa jina la kati la kwangu wameona linafanana na kiongoz flan wakajua may b nataka kutakatisha nikaenda kwa meneger akanisikiliza akawafokea sana wakarudi wamebinua midomo

Nikaondoka zangu

sent from toyota Allex
 
It doesn't cost you an arm and a leg to be humble,friendly and civil.
 
Dogo umeongea pumba kama za bashite kubali kurekebishwa. Kubali huna exposure, mashirika (mostly ya nchi za nje) yanayojua maana ya personal selling yana a very better customer service system ambayo inafocus kuretain exisiting customers na kuattract new customers altogether. Sasa wewe unajisifu kujipendekeza ili upate huduma ambayo ni haki yako.
 
Pole.
 
Wanaangalia kuanzia kiatu chako hadi nguo. Kama umevaa vibaya dharau zinakuhusu. Huwezi amini ukiwa smart sana unaweza kumng'oa mwanamke yeyote hata waziri. Kuna siku mbunge fulani wa kike alitaka kujichanganya kwangu kisa nguo zangu tu.
 
Wanaangalia kuanzia kiatu chako hadi nguo. Kama umevaa vibaya dharau zinakuhusu. Huwezi amini ukiwa smart sana unaweza kumng'oa mwanamke yeyote hata waziri. Kuna siku mbunge fulani wa kike alitaka kujichanganya kwangu kisa nguo zangu tu.
Daaah yani JF kuna kila aina ya viumbe na hivi tunaficha ID zetu basi unajitungia chochote unapost

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Mimi yalishanikuta hayo nime draw kama 500,000/- kuja kucheki bunda 3 za laki laki zina 90 tu. Nikakausha tu kesho yake nikaenda tena makusudi ili nikaangalie tu kabinti kalivyo kazur kezi.
 
Kunyenyekea haki yako ni uoga na ujinga.
Nyie kwa udhaifu wenu ndo mnawapatia hawa nyumbu kichwa na nchi haisongi mbele.

We endelea kujioendekeza kwao , mi sihitaji kunyenyekewa na mtu ninempatia huduma inayonifanya nisavaiv pia sinyenyekeaji watoa huduma hata asante yangu hupati. Mshahara wako unakutosha.

Kujikomba kwa visichana vya benki ndo ustaarabu shekhe?
It doesn't cost you an arm and a leg to be humble,friendly and civil.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yupo mmoja aliacha kuhudumia foleni akaanza kuchat yaan dharau mwanzo mwisho
 
Hata wewe unachoandika hapa naona blah blah na kuleta dharau za mishahara ya watu. Wewe vipi unalipwa bilioni kwa mwezi?
No matter what Effective and Satisfactory Customer service ni Muhimu sana achana na Kujuana na walinzi na mambo ya mishahara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…