Nilienda Ubungo kuchukua parcel miaka hiyo, nikiwa na bint flani hivi sasa wale wapiga debe wakadhani tunasafiri, kila tunaekutana nae anatuzonga, sisi tunawaambia hatusafiri ni parcel tunafuata, wanang’ang’aniza tuwaambie ni ofisi za gari gani ili watupeleke hatukuwaambia, sasa wakawa wameungana kama 10 hivi wanatufuata nyuma, basi ikabidi niwape jibu kwamba sisi ni kweli tunasafiri hatufuati parcel bali tunaelekea Zanzibar, ofisi za kikatia tiketi ni wapi?
Aisee, tulioga matusi stendi nzima iligeuka uwanja wa matusi, watu wengine wakabaki wanashangaa na kucheka!