Vituko vishaanza bunge maalum la katiba

Vituko vishaanza bunge maalum la katiba

Okinawa

Senior Member
Joined
Nov 16, 2009
Posts
174
Reaction score
29
Kutokana na wajumbe wengine waliochaguliwa kwa kujuana leo kuna mjumbe mmoja aliruhusiwa kumuuliza mgombe nafasi ya Mwenyekiti wa Muda ndugu Kificho na kumuuliza:
"Ndugu mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Muda umetuomba wote tukupe kura za ndiyo, je mimi nikikupa kura yangu utafurahi? ".

Ndugu wananchi hilo ndilo lilikuwa swali la mjumbe huyo. Huyo ndiye watanzania wanamtegemea kutengeneza Katiba kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa. Nilimshangaa yule Mwenyekiti Mwanamama naye kulikubali swali la kijinga namna hiyo.

Watanzania tutegemee vituko vingi kwenye bunge hili. Tatizo kubwa likiwa ni kuteuliwa wajumbe kwa kujuana na kulipa fadhila badala ya kuchagua mtu anayeweza kutengeneza katiba kwa maslahi mapana ya Taifa.

Ni bora tungekuwa na wajumbe 250 wenye moyo wa uzalendo wa kutengeneza katiba kwa maslahi mapana ya taifa hili kwa ajili ya kulinda raslimali zetu zinazoibiwa kila siku kwa mikataba mibovu kuliko hawa zaidi ya 600 ambao wengi wao ni wale wa kushangilia 'ndiyooooo' au kuuliza maswali ya kitoto na kijinga kama alilouliza hule 'mjinga'. Naomba wanamkumbuka jina lake wamtaje hapa hadharani.
 
Ndugu yangu mpendwa, ni vema ukafahamu kuwa hili si Bunge bali ni Bonge la aibu! Ukweli ni kuwa katika watu waliokwenda hapo Dodoma, asilimia kubwa ni wale waliokwenda kutimiza wajibu kuwa nao wapo Dodoma na ndio maana unaona hali kama hii. Sasa hapo naomba ujiandae kuona maswali ya kiupuuuzi zaidi ya hilo, kwani kama watu hawaijui hata hiyo Rasimu wanayoenda kuijadili, unatarajia nini?

Zaidi Vyama vyetu na hasa CCM nayo imeweka kabisa msimamo wak juu ya Muundo wa Muungano, kuwa wao wanataka Serikali mbili na wala sio tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Mzee Joseph S. Warioba. Katika hili tufahamu kuwa wajumbe watakula fedha zetu na pia watamaliza muda wao hapo Bungeni bila kuwa na jibu linaloeleweka.

Kimsingi tunapaswa kuiombea sana nchi yeytu hii ya Tanzania!
 
Mimi nakoelekea ni kuacha kabisa hata kuabudu Mungu inakueje anifanye nizaliwe kwenye nchi kama hii!! Nini kosa letu? Na wapi tulimkosea?
Hata kwenye mambo muhimu hivi anashindwa kutusaidia hata kidogo kama kweli anaupendo na sisi? Mbona wazungu, wachina, waarabu hata wahindi jamani wana afazali, what is it with us?
Swali la kijinga watu ni wajinga.
Zoezi rahisi kabisa la kuhesabu kura siku ya kwanza kura zimezidi! WHAT THE ----! Halafu tunachukulia urahisi rahisi tu nakucheka cheka!
Na huyo mahalu si ndio yule wa Italy!
 
hilo jina tu la KIFICHO ni wazi ilo libabu ni lihuni, lichoyo, likorofi lililopendekezwa ili kutudhulumu watanganyika.

ovyoooo hili libabu jinga
 
Kila uchwao kitokacho nchi hii ni kituko kingine.
Tatizo wenye nchi wanatuona watanzania tu vilaza,kuanzia uteuzi wa wajumbe na categories zao ni uhuni tu.
So much to come......,.
 
Mimi nakoelekea ni kuacha kabisa hata kuabudu Mungu inakueje anifanye nizaliwe kwenye nchi kama hii!! Nini kosa letu? Na wapi tulimkosea?
Hata kwenye mambo muhimu hivi anashindwa kutusaidia hata kidogo kama kweli anaupendo na sisi? Mbona wazungu, wachina, waarabu hata wahindi jamani wana afazali, what is it with us?
Swali la kijinga watu ni wajinga.
Zoezi rahisi kabisa la kuhesabu kura siku ya kwanza kura zimezidi! WHAT THE ----! Halafu tunachukulia urahisi rahisi tu nakucheka cheka!
Na huyo mahalu si ndio yule wa Italy!

Na zilizoharibika ni kama ngapi mkuu?
 
Yani nimesikitika na kucheka at the same time.

@mod inabidi tufungue jukwaa la bunge la katiba ili tukusanye matukio yote huko
 
Kutokana na wajumbe wengine waliochaguliwa kwa kujuana leo kuna mjumbe mmoja aliruhusiwa kumuuliza mgombe nafasi ya Mwenyekiti wa Muda ndugu Kificho na kumuuliza:
"Ndugu mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Muda umetuomba wote tukupe kura za ndiyo, je mimi nikikupa kura yangu utafurahi? ".

Ndugu wananchi hilo ndilo lilikuwa swali la mjumbe huyo. Huyo ndiye watanzania wanamtegemea kutengeneza Katiba kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa. Nilimshangaa yule Mwenyekiti Mwanamama naye kulikubali swali la kijinga namna hiyo.

Watanzania tutegemee vituko vingi kwenye bunge hili. Tatizo kubwa likiwa ni kuteuliwa wajumbe kwa kujuana na kulipa fadhila badala ya kuchagua mtu anayeweza kutengeneza katiba kwa maslahi mapana ya Taifa.

Ni bora tungekuwa na wajumbe 250 wenye moyo wa uzalendo wa kutengeneza katiba kwa maslahi mapana ya taifa hili kwa ajili ya kulinda raslimali zetu zinazoibiwa kila siku kwa mikataba mibovu kuliko hawa zaidi ya 600 ambao wengi wao ni wale wa kushangilia 'ndiyooooo' au kuuliza maswali ya kitoto na kijinga kama alilouliza hule 'mjinga'. Naomba wanamkumbuka jina lake wamtaje hapa hadharani.

Duh!!!! Inasikitisha sana.... Yaani hii nchi hii....
 
Naomba turekebishe kidogo hii "yale ni maoni ya watanzania sio yaliopendekezwa na tume" kuna washenzi wanataka kutia ujinga wao mule aafu wanachekacheka tuu, UKIJUA KWANINI WAKO ZAIDI YA 600 UTAKUA UMEJUA CHAMA GANI KITAPETA.
 
Tungejua tungewanywesha antvirus cyrup kabla yakuingia bungeni. wameshapata wadudu tayari
 
Naomba turekebishe kidogo hii "yale ni maoni ya watanzania sio yaliopendekezwa na tume" kuna washenzi wanataka kutia ujinga wao mule aafu wanachekacheka tuu, UKIJUA KWANINI WAKO ZAIDI YA 600 UTAKUA UMEJUA CHAMA GANI KITAPETA.

Jambo moja linanishangaza, hivi kama muundo wa muungangano haujajulikana itawezekana kujadili mambo mengine maana naona hata watu ambao ni wasomi kabisa wanasema jambo la muungano si muhimu bali kuna mambo mengine muhimu zaidi. Hivi ni kweli. Mimi naamini jambo la muungano ndilo la kwanza, tuishaua tunauwa na muungano w ura gani ndiotuaweza uendelea mbele na mambo mengine.
 
Back
Top Bottom