Miaka kadhaa nyuma niliendaga gheto kwa wanangu jamaa mmoja alikua na birthday.. So ikafanyika kigumu (kipindi hicho viroba havijafungiwa).
Mimi situmii kilevi chochote, ila wana wote wanatumia, na time nimeenda sufuria kubwa la pilau lipo motoni, linasubiriwa liive ili tuufinye. Katika kuvuta muda jamaa wakatoa soda kama 4, nikafunguliwa ya kwanza ile nakunywa bila kujua kumbe wamechanganya viroba vya kutosha, nikaimaliza, jamaa wakanipa ya pili wakawa wananijaza upepo wananiambia we kunywa tu soda zipo za kutosha na mimi bila kushtukia nikazipiga kama nne hivi na zote walikua wananipa zikiwa zimefunguliwa huku zimechanganywa viroba bila mimi kujua.
Hata sikumbuki nililewa saa ngapi ila nilikuja kushtuka kesho yake saa 4 asubuhi, shati lote huku mbele limeloa matapishi, bukta na nguo ya ndani zote zimeloa mkojo, nilipolala napo pameloa kinoma.
Nilivyoamka hadi jamaa wakashukuru maana walijua wameua.