Mind you, wanasiasa ni watu wajanja sana. Nadhani hata wewe pia umeweka wasiwasi kuwa huenda ameokoka kwa hila. Je alikuwa hawezi kutenda matendo mema akiwa kwenye dhehebu lake la awali? Kuokoka ni matendo.
sina hakika unasoma biblia ipi inayosema kuokoka ni matendo...ila ninayosoma mimi inasema mwanadamu haokolewi kwa matendo ya sheria (dos and donts)...anaokolewa kwa neema kwa imani katika Kristo Yesu....mimi sijaongelea swala la dhehebbu wala sijui alikua ana dhehebu gani.....ninachokiona cha msingi ni kuwa kaamua kumgeukia Yesu...kama ameamua kuhama alipokua anasali (iwapo alikau nako) anajua yeye ni kwa nini na huenda hapakumasaidia kumjua Mungu. ana haki kabisa ya ku-renew maisha yake. mara nyingine inatulazimu kuhama tulipokuwepo ili mabadiliko yetu yawe dhahiri na tupate malisho ya kutuwezesha kukua katika imani....
Kuhusu kuokoka kwa hila, nataka tu nikujulishe kuwa wako wengi walioingia kwenye wokovu kwa sababu fulani na sio kwa misingi ya kuishi sawasawa na mapenzi ya Mungu...na walipoingia tu, Mungu aliwakamatia humohumo na wakabadilishwa mtazamo wao wa awali....kwa uapnde wangu, sioni chochote cha kisiasa kwa maamuzi ya Odinga kuokoka...tena ninapotazama jina la ministry/dhehebu alilokwenda, sioni kama ni dhehebu lenye ushawishi wowote kwa wakenya....
Ni tabia mbaya kuangalia imani za wengine katika mtazamo negative. tunasimama kwenye nafasi za Mungu kuwa wahukumu wa yaliyo ndani ya mioyo ya watu ambayo hatuyajui....ni bora tungejihukumu sisi kwanza.....pia kumbuka hutapata dhambi iwapo utamfikiria mtu mema ingawa yeye amekusudia mabaya, ila ni dhambi kumkusudia mtu mabaya wakati yeye amakusudia mema au hata kama amekusudia mabaya. Tuwe na nia ya Kristi ndani yetu...Alituona tunafaaa ingawa tulikua katika hali ya dhambi na kupotea akajitoa kwa ajili yetu. Huwezi kumsaida mwingine kumjua Mungu na kumuombea iwapo unamuawazia mabaya.
Asante Bwana Yesu kwa kumuokoa Odinga. Tunaomba UMUOKOE NA ROSTAM AZIZ, SOMAIYA, JEETU, LOWASA NA WENGINE WOTE AMBAO KATIKA MACHO YA WANADAMU WANAONEKANA KUWA HAWAFAI TENA. WAPE TOBA YA KWELI NA WAUNGAME JUU YA NCHI WALIYOIKOSEA NA KWA RAIA WAKE.
Najua bado unawapenda sana na kwa vile bado wanaishi, basi unawapa nafasi nyingine ya kutafakari njia zao na kubadilisha maisha yao. waoenshe kuwa bila wewe hawatafika popote.
Liokoe taifa letu na uiponye nchi yetu