BUSH BIN LADEN
JF-Expert Member
- Mar 16, 2019
- 8,447
- 19,425
Mi na rafiki yangu tuliwahi kupewa tenda na mtoto wa mtendaji ya kufanya nyuki wahamie kwenye mzinga wake baada ya kuwa tumejifanya tunajua dawa za kuchoma na kupulizia ili kuwavutia nyuki wahamie kwenye mzinga.. Tumeshakula malipo ya awali ya kama shilingi 40 hivi maana alitupa sarafu za sh 10 kama Mara 4 hivi.. Mda ukazidi kwenda nyuki wamegoma kuhamia jamaa akaanza kumind.. Tukafikiria tufanyeje maana muda si mrefu ulikuwa unaenda kuwa msala, baadae rafiki yangu akaja na plan ilikuwa mission impossible ila hatukua na jinsi tumeshakula hela ya watu.. Lengo ilikuwa ni kuiba nyuki wa kwenye mzinga kwa jirani mmoja hivi tuwahamishie kwa jamaa.. Basi Tukapanga alhamis 1 ndo tufanye tukio, basi kila mmoja akatafuta excuse hatukwenda shule.. Tukawawinda wale majirani wenye mzinga walivobeba majembe kwenda shambani tukastuana tukatimba eneo la tukio jamaa akajitolea kamfuko kake ka sport ka daftari ndo tuwabebee nyuki.. Basi tumefika pale nikapanda na kile kimfuko nikavunja upande mmoja nikazoa lundo nikapakia kwenye kimfuko nikakabana.. Aisee nyuki waliniuma mpaka nikajikuta nadondoka mimi chini na mfuko chini ila kama askari wa miavuli nimefika chini nimeteguka mguu jamaa kapita na kimfuko kakimbia nacho huku kundi lingine la nyuki likimkimbiza kaenda hadi kwenye mzinga wa jamaa kafungua kawamwaga mle kafunika mzinga ulikuwa yale masanduku ya mbao.. Mimi huku nyuma ilibidi nikimbie tu pamoja na maumivu maana nyuki walikuwa wana niuma mpaka basi.. Nikafika sote tunanundu ila kazi tumeimaliza.. wazazi wangu wakaniamshia msala baada ya kuona nimerudi nyumbani nachechemea huku na manundu ya nyuki ikabidi niwaeleze ukweli wakanichapa ila badae mama akanipeleka dispensary.. jamaa hakumalizia malipo maana nyuki hawakukaa mule hata siku 5 maana kumbe malkia wao tulimuacha kwenye ule mzinga tuliouhujum